VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Thursday, November 24, 2005
ETI HATUPENDI KUJISOMEA?
Kuna waraka mmoja umenifikia baada ya kuanza kusambazwa kwenye mtandao. Kimsingi, nia ya mwandishi nadhani ilikuwa ni kuamsha vita dhidi ya watu weusi wa Marekani. Nina uhakika huyu mwandishi alikuwa ameshanunua silaha tayari kwa vita yoyote. Anadai anakemea kuhusu ujinga, uchoyo na ufujaji mali na ubinafsi walio nao hawa ndugu zetu. Nilipouona kwa mara ya kwanza niliupuuzia nikiamini kwamba kwa sababu mimi sio mmarekani mweusi hata wa kufikia, basi halinihusu hili. Kama ni tsunami basi haikufika kwenye mwambao wangu.

Lakini haukupita muda mrefu sana nikawa nasikiliza mhadhara mmoja uliokuwa unatolewa na Dr. Naim Akbar juu ya historia ya mtu mwafrika. Huyu jamaa kwa kweli ni bingwa wa ushawishi na sio ushawishi hewa bali ule wenye mantiki na mtizamo ninaoupenda. Wa kutumia hoja nzito nzito kama vile silaha za maangamizi. Tafadhali tembelea hiyo tovuti yake na fanya mpango wa kumsikiliza kama bado hujafanya hivyo. Alichofanya mwanazuoni huyu ni kunikumbusha wazi wazi kwamba hawa wamarekani weusi ni kaka na dada zetu. Kama wamepotea au wanatangatanga nyikani haina maana kwamba sio wenzetu. Wengi wao huwa wanatudharau sisi tunaotokea barani Afrika. Nadhani nipo mbioni kuwasamehe kwa dhambi hii. Wengi wamewahi kuniambia kwamba mababu zetu waliwauza mababu zao na ndio maana hawaoni sababu ya kujipendekeza kwetu.

Lakini swali la msingi likabaki kichwani kwangu.Je huyu mwandishi ambaye ana kila dalili za kuwa mbaguzi wa rangi ana hoja yoyote ya kweli katika shutuma zake? Sasa huu ni utaratibu wangu mpya, namsikiliza kila mtu,najaribu kutopuuzia mambo juu juu tu.Nayachunguza kwanza. Fuatana nami.

Mwandishi huyo mbaguzi amezungumzia ule msemo kwamba ukitaka kuficha kitu mtu mweusi asikione basi kifiche kwenye kitabu. Hatokiona kwa sababu hapendi kusoma,hajishughulishi na vitabu. Hivi sasa tunaishi kwenye dunia ya mawasiliano na habari. Weusi tuna nafasi sawa na wenzetu weupe ya kusoma na kufanyia uchunguzi kila kitu. Ni kweli kwamba hatupendi kusoma sio vitabu vilivyoandikwa na wazungu tu bali hata weusi wenzetu? Mapinduzi ya kiuchumi na kijamii tunayoyahitaji yatatoka wapi bila kujitahidi kusoma na kufanyia kazi tunayoyasoma? Hivi ni kweli kwamba watu weusi tunapenda starehe tu bila kuzifanyia kazi? Je sisi ndio masoko ya bidhaa za wazungu?Tunatumia tusichonacho? Tunapigia debe kuandikwa upya kwa historia yetu, tunasema tuiandike sisi wenyewe.Je itasomwa na nani?Ambazo zimeshaandikwa na watu kama Dr.Naim Akbar zinasomwa na nani?

Sikupenda kukumbushwa juu ya uvivu wetu wa kujisomea lakini baada ya kutafakari nikaona kuna ukweli wake. Au unabisha?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 7:59 PM | Permalink |


Maoni: 4


  • Tarehe: 9:56:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Jeff tazama mfano mdogo tu wa maandishi haya unayoandika, je wadhani hadhira yako ni ipi kama si ile ile siku zote na inaweza kuwa inapungua? Huu ni ugonjwa mkubwa, plae Chuo Kikuu Mlimani siku hizi kuna tabia ya wanafunzin kukopiana maandishi na utakuta wanakopiana neno kwa neo wanafunzi zaidi ya 20 lakini bado profesa anatoa maksi zinazotofautiana! Usaliti huo wa moyo...yafanye haya huku kama chuo hakijaota mbawa?

    Nifunge domo langu kwanza ili wajitokeze wengine na yao!

     
  • Tarehe: 3:08:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Indya Nkya

    Utamaduni wa kujisomea unaanzia wapi? Unajengwaje? Makene suala la Vyuo vikuu ni nyeti sana. Unajua wengi tunasoma ili tufaulu mitihani. Tupate vyeti. Hujawahi kukumbana na huu msemo toka kwa mwalimu wako: Unapata wapi muda wa kusoma ambayo hujafundishwa? Ukiendelea hivyo utafeli!1

     
  • Tarehe: 7:10:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

    Hao wanaokopiana chuo kikuu mie nikipata kufundisha pale nitakuwa mnoko sana. Nitawapa misahafu mirefu mirefu kwa maksi chache mpaka wataelewa... Haya twende kwenye hoja:

    Ndugu mnaokaa ughaibuni, hivi katika tazama tazama zenu mnawaona watu wengi wa kawaida huko majuu wanaopenda kujisomea masuala mazito mazito? Au ni wasoma hadithi za upelelezi kama za Wili Gamba?
    Wanaweza kukumbuka na kujua mambo yao, pamoja na sababu nyingine, kutokana na vipindi vyao vya televisheni na vyombo vyao vya habari. - masomo ya shule za msingi yanaonyeshwa kwa undani kila asubuhi, jioni vipindi vya ushujaa wa mashujaa wao vimejaa -Wamarekani weusi kuijua Timbuktu mpaka wakanunue vitabu - ukiangalia sanaa zao hao wabaguzi...nazo ni mambo hayo hayo, huko marekani kila mtu anajua habari ya first and fifth amendment... sijui kama wamesoma katiba yao...
    Pengine hatupendi kujisomea,sitabisha sana, lakini wanaoendesha maendeleo ya huko ni wasomi na wafanyabiashara wabunifu kadhaa.Sio watu wowote tu. Wanasayansi walioko hapo NASA kuna wachina, wahindi, na waafrika, manesi waafrika ndio wamejaa kwenye mahospitali, wote wamesoma vitabu... na huko kwenye bonde la Silikoni kwenye makompyuta ndipo wageni walipojazana.
    Wasomi, mkijumuishwa na wanablogu wote wa kiafrika ughaibuni... nyote nyie mnapenda kujisomea.
    Huyo mwandishi mmbaguzi anatupiga madongo kinamna...
    Anataka tuamini matusi anayotukana, na tukiamini tu tumekwishaa!
    Tumeshaamini mengi waliyosema na ndio maana tunakwisha...
    Haidhuru, nalotaka kusema ni kuwa ugonjwa mkubwa sio kutopenda kujisomea tu bali pia ni ugonjwa wa "kuamini kuwa tumeshindwa - au hatuwezi" haswa jambo analotaka kutufanyia huyo mwandishi.

     
  • Tarehe: 8:55:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Egidio Ndabagoye

    Hii inasikitisha sana.Kweli hatuna utamaduni wa kujisome vitabu.Padre Karugendo alisema kuwa ..."ukienda katika maduka ya vitabu utakuta vitabu vimejaa vuumbi..." havinunuliwi.Ukitaka kuutafuta umaskini basi jaribu biashara ya kuuza vitabu.Ndio maana watanzania tulio wengi hatuna uwezo wa kupambanua hoja.
    Makene,hili sula la vyuo vikuu kama alivyosema Indya ni nyeti mimi niko huku naona... ni kitu cha kawaidaa sana kunakiliana kazi walizotupa wahadhiri.Kila siku hili jambo linanikera sana kusomea mitihani! na kusoma yale tu yanayofundishwa darasani na hii ya kusoma magazeti ya 'udaku'? Hapo nitapigwa

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker