VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Wednesday, June 07, 2006
MAONI YAKO,KERO ZAKO!
Ahadi ni deni.Huu ni msemo wa kiswahili wenye maneno machache sana lakini yenye maana na upana wa aina yake.Ukiahidi kitu usinune pindi unapoanza kufuatwafuatwa kwa mtindo wa mdaiwa. Pengine kwa kuzingatia msemo huo serikali ya JK imetimiza ile ahadi ya kuanzisha tovuti ambayo wananchi wataitumia kueleza maoni yao,kero zao,majungu yao nk. Hii ni mojawapo ya ahadi kemkem zilizotolewa wakati wa kampeni na ambazo niliwaomba wananchi kila leo kuchukua kalamu na karatasi na kuziandika chini ili zisije sahauliwa na ili iwe rahisi kuwakumbusha watoa ahadi. Hivi mpaka hivi leo,mbunge wako au diwani wako ameshatimiza ahadi zake ngapi?Unakumbuka?

Habari hii nzuri nimeikuta kwenye tovuti ya Miruko aliyepo kule makao makuu ya nchi yetu.Makao makuu ya kwenye vitabu na risala. Hata sijui kwanini watanzania tunapenda kudanganywa waziwazi namna hii,huku mabilioni ya kutumika katika ndoto hewa. Makao makuu kuwa Dodoma haiwezekani,kwanini tusikubali tukaepusha matumizi yasiyokuwa ya lazima?Kunani Dodoma?

Nina maoni na maswali kibao kuhusiana na tovuti kama hii.Lakini machache ni je,serikali itasikia lipi jipya ambalo halijulikani mpaka leo?Je wapiga filimbi hao(huku wanaitwa whistle blowers) watalindwa kwa sheria zipi/namna gani?Kumbuka kuandika maoni kama anonymous haina maana kwamba huwezi kupatikana ulipo.Je serikali haitatumia tovuti hiyo kujua na kuwateketeza kirahisi maadui zake?(serikali zetu zina sifa mbaya ya kutotaka kuambiwa ukweli hata siku moja) Je nguvu kazi ipo ya kutosha kupitia mashushushu wa nchi kufuatilia kwa karibu kero na maoni ya wananchi?Nikisema fulani ana utajiri ambao haujulikani kaupata vipi,nikatoa na ushahidi wangu pale,faili litafunguliwa?Mangapi yatafunguliwa nk?Maswali bado ninayo kibao lakini ngoja niishie hapa. Uwanja huu wa maoni na kero unaweza kuupata kwa kubonyeza hapa.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 10:54 AM | Permalink |


Maoni: 3


  • Tarehe: 11:40:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Ninavyofahamu Jeff ni kuwa hii tovuti sio ya serikali bali wapenzi wa Kikwete. Kuna majaribio yanayofanywa na serikali nyingi kujenga uhusiano wa karibu kati ya wananchi na viongozi kwa kutumia teknolojia za serikalipepe (egovernment). Nadhani kama Kikwete anataka kufanya hivyo au mtu yeyote anataka kufanya hivyo ni vyema akajua kuwa kuna mifano mingi ya kujifunza toka katika nchi mbalimbali na taasisi mbalimbali za kitafiti. Serikalipepe ni jambo ambalo, ingawa litachukua muda kuiva, lina nafasi yake fulani katika miaka ijayo.

     
  • Tarehe: 4:49:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Egidio Ndabagoye

    Nakubaliana na Ndesanjo kuwa hii i tovuti ni ya wapenzi wa Kikwete.Kulikuwa na malumbano katika gazeti fulani la kila wiki kuhusu ni hipi tovuti ya Kikwete(kutolea maoni ya wananchi).Sasa mmoja wa watu aliitoa Tovuti hii.Nami nikaipandisha mtandaoni.Mimi Nimeshagundua kuna mkono wa mshikaji mmoja katika tovuti ile

     
  • Tarehe: 2:43:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Rama Msangi

    Wakati nilipokuwa huko Makao makuu ya kwenye risala na makabrasha, kipindi wana-CCM wanachukua fomu za kumpata atakayechukua nafasi ambayo kwa sasa anayo JK, nakumbuka kilichotokea siku yeye JK alipokuwa anachukua fomu. Kuwa tofauti na hali ilivyokuwa kwa wagombea wengine katika kuulizwa maswali, huyu yeye aliulizwa maswali ambayo kwa mtu yeyote mwenye kujua maana ya ushabiki, upenzi na umamluki, angeligundua kuwa kulikuwa na kitu fulani ndani yake.

    JK ni mtu ambaye hutumia kikamilifu kila fursa anayoipata (Opportunist nyie huko Ulaya mnawaita) na ndio maana haikunishangaza sana pale niliposikia kuwa siku hiyo alipandikiza watu wake kwa ajili ya kumuuliza maswali fulani kwakuwa alikuwa na yake ambayo katika mazingira ya kawaida asingeliweza tu kusimama hadharani na kuanza kuyatoa.Hili nalo bilashaka ni moja ya hizo hizo fursa ambazo anataka kuzitumia kwa lengo lake fulani ambalo huenda mimi na wewe hatulijui.

    Kuna mambo mengi ambayo mtu unaweza kujiuliza kuhusu hili jambo, lakini naomba tu niulize moja kati ya maswali mengi: KERO YA RUSHWA IKO WAZI KWA KILA KIONGOZI, JK ALITAMKA HADHARANI KUWA ANA MAJINA YA WALARUSHWA, LAKINI AKASEMA ANAWAPA TENA MUDA WA KUJIREKEBISHA, KUNA UMUHIMU GANI WA MAONI AU KERO ZA WANANCHI IKIWA TUNAKWAMBIA TUNAUNGUA UNASEMA KUWENI NA SUBIRA MOTO HUENDA UKAPUNGUA WENYEWE?

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker