Kwa takriban siku moja na nusu blog yangu ilikuwa na matatizo ya kufunguka. Pole na samahani kwenu nyote mliopata usumbufu,shida na karaha mlipokuwa mkijaribu kunitembelea. Naamini kwamba hivi sasa imetengemaa na moto ni ule ule.
Simon Kitururu, asante kwa kunikumbusha kuhusu tatizo la kutofunguka kwa kutumia ile blog yangu ya kizungu. Ahsante sana.
Kaka Jeff,blogu yako lazima nipitie kila siku.Nimefurahi kuona imefunguka.Jah live.