VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Wednesday, January 02, 2008
KHERI YA MWAKA MPYA.MAAZIMIO?

Kheri ya mwaka mpya msomaji wangu. Nimekuwa kimya kidogo,naelewa.Mambo yalikuwa mengi mwishoni mwishoni mwa mwaka.Familia,watoto,ndugu,jamaa,kazi,maisha ya ughaibuni nk.Msururu wote huo,kwa njia moja au nyingine,unahitaji atensheni yangu.Silalamiki lakini,nasema tu.Ndio hali halisi ya maisha.Ukishazaliwa mtoto wa kiume tena ndio inakuwa balaa.

Vipi wewe? Sherehe za xmas ulizisheherekea vipi?Mwaka mpya umeuanzaje?Hapa nilipo ni baridi mtindo mmoja.Wakati mwingine unatamani uishi ndani ya friji ili ujue moja.Huu ndio ule wakati wa korodani kunyweeea.Kama huna nguvu ya ziada,kazi kwako.Unaweza paniki ukakimbilia kale ka kidonge kanakoanzia na herufi V.Nyakati nyingine huwa najiuliza kama ulikuwa mpango wa Mungu watu waishi upande huu wa dunia.Nasema hivyo nikizingatia jinsi zama hizo zilivyokuwa.Hakuna nguo za sufi kama tulizonazo hii leo,hakuna magari yenye vileta joto kama hivi leo.Hakuna nyumba zilizo na majiko ya humo kwa humo.Sasa waliishije hao watu wa mwanzo huku?

Kwa upande mwingine,hainishangazi kusikia zile habari za kisayansi na historia kwamba fuvu la kale kabisa lilipatikana kule Tanzania.Naam..kule kunafaa kuishi,ndio mpango wa Mungu.Ajabu sisi wenyewe hatujui uzuri wa kwetu.Tukiona vinaelea tunadhani vimeshushwa..kumbe.Ndio maana profesa mmoja aliwahi kuuliza Waafrika Ndivyo Tulivyo? Wengine wakamjia juu...sijui walikuwa wanafikiria nini.Hata hivyo kwetu kunabakia kuzuri.Kwetu unaweza ukalala mzungu wa nne na wala usikauke kwa baridi kali.Tatizo mbu watakavyokutandika..utakoma.Hutorudia tena.

Sasa usije ukadhani sipendi kabisa kuishi huku.Ama!Ughaibuni kuna raha zake.Karaha nazo zipo lakini wenzetu wanajitahidi sana kila siku kuzidhibiti.Mpaka kahawa unaweza kununua ukiwa umekaa ndani ya gari yako tu.Kama sio uvivu ni nini hicho?Halafu wenyewe wanashangaa kwanini wananenepeana kama viboko.Kila unachokiona kwenye luninga ni kuhusiana na unene vs wembamba.Mwaka mpya unapoanza kama hivi,mamilioni ya watu(hususani wanawake) wanadhamiria kupunguza uzito wao.Yaani huku mwanamke asiye na nyama au minofu ndio anayevutia zaidi.Haingii akilini hii..au sio? Kama nakuona vile.Huku ughaibuni husikii kitu umeme umekatika wala maji.Ukifungua bomba...hayoo..meupee.Umeme ukikatika inakuwa ni breaking news.Utawasikia wazungu..can you believe this?Nami nawajibu..I know..I can’t believe this!Kichwani nawaambia..mngejua kwetu umeme unakatika kutwa mara sita na wakati mwingine unakaa hata wiki bila kurudi na bila kusikia neno lolote achilia mbali samahani kwa wahusika,mngebana ngenge.

Enewei,nakutakia kheri ya mwaka mpya.Tusukume sote gurudumu la maendeleo...hata kama limekwama kwenye lindi la tope zito.Kabla sijasahau,umesikia ahadi kutoka kwa wapinzani nchini Tanzania?Wamesema huu ni mwaka wa kupigania katiba mpya nchini Tanzania.Katiba iliyoandikwa na wananchi na sio hii yenye harufu mbaya ya kikoloni na sisi kwa ujuha wetu tunaishia kuweka viraka tu kila kukicha! Wapinzania wanataka pia tume huru ya uchaguzi.Hii ya sasa ndio kama hivyo ilivyo.Haina meno,jaji wa serikali ndio mwenyekiti wa tume.Kwani hujasikia yaliyotokea huko Kenya?Mwenyekiti wa Tume anasema eti alipomtangaza mshikaji wake Mwai Kibaki kuwa mshindi alikuwa “under pressure”.Msalie mtume,hivi lini tutastaarabika sisi?Wenzetu wakitushangaa eti tunakasirika,tunawaita wabaguzi na wachimba chumvi.Mitusi inayotutoka huku mishipa yote ya fahamu ikiwa imetutoka,sio ya kawaida.

Kheri ya mwaka mpya msomaji.Kama unapenda uandishi wa namna hii niambie niendelee.Nimechoka ule uandishi wa kiprofesa.Simple 2008.Ndio azimio langu.

 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 11:28 AM | Permalink |


Maoni: 9


  • Tarehe: 9:40:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    jeff umenivunja mbavu ile mbaya maana nilikua nacheka kwa sauti ya juu, my wife wangu akaniuliza vipi mbona unacheka sana,mi nikashindwa kumueleza habari za korodani.

     
  • Tarehe: 2:54:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Jeff, hichi kiswahili cha mitaani sijui umekipatia wapi but i really enjoyed it.. Nice one.. Naona ya kimprofesa waaachie wenyewe... Luv it..

     
  • Tarehe: 4:51:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Hello Jeff
    Habari yako imetulia, nimefurahi na kucheka, Nakutakia mafanikio katika kazi zako zote unazofanya pamoja na post mpya kwenye blog.
    Pembroke/ON

     
  • Tarehe: 8:24:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    umenikuna mzee wa pori (mshitu wa vusangi).tatizo lako habari zako raha utamu lakini chache. acha uvivu jeff.

     
  • Tarehe: 8:25:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    umenikuna mzee wa pori (mshitu wa vusangi).tatizo lako habari zako raha utamu lakini chache. acha uvivu jeff.

     
  • Tarehe: 1:27:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger mjengwa

    Nimecheka sana mkuu. Kwa muda mrefu sana sijatembelea blog yako. Nikasema hapana ngoja kwanza nije hili nipate dozi, da nikakutana na hizi.

    Yaani nimcheka sana na hii story. anyway kuhusu hii style, jibu endelea nayo mimi nimeipenda at least naweza kucheka. Kwa maana habari za nyumbani tz huko, kama hauko makini kichwani unaweza kuingia mtaanni na bunduki kuwatafuta kina JK,Werema,EL,RA etc yaani wanachefua kwa kweli.

    Mkuu heri ya mwaka mpya na wewe.

     
  • Tarehe: 4:12:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous vimax canada

    thanx for sharing nice blog information

     
  • Tarehe: 4:39:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger poker

    PROMO DELIMA
    poker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya

    Bonus yang kami sediakan :
    * TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
    * Bonus referal sebesar 10%

    Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
    Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
    Come join and be a winer with us !!

    Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
    Livechat_____: delimapoker
    BBM__________: 7B960959
    Facebook_____: Facebook
    Phone number_: +85595678845
    pendaftaran___http://www.delimapoker.com/?ref=19860605

     
  • Tarehe: 11:30:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger walicaden

    WinStar World Casino And Resort - JetXtra
    The resort features nearly 5000 slot 춘천 출장샵 machines, a full-service spa, 사천 출장마사지 an indoor pool, and 남원 출장안마 a casino. Guests can indulge in 안양 출장샵 a swim in a nightclub. The 창원 출장안마 hotel also

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker