YESTERDAY HAS GONE FOREVER!TOMMOROW WILL NEVER ARRIVE,BUT TODAY IS YESTERDAY'S TOMMOROW WITHIN YOUR REACH.WHAT ARE YOU DOING WITH IT?
Tuesday, August 09, 2005
AFRIKA NI NCHI MOJA?
Hapa katika nchi za magharibi Afrika huzungumziwa kama nchi moja tu na siyo bara kubwa tu lenye nchi lukuki.Nimekuwa nikijiuliza maswali mbalimbali juu ya hili lakini kubwa limekuwa juu ya faida na hasara za nchi za magharibi kuliona bara la Afrika kama nchi moja tu.
Wananchi wengi wa hapa huniuliza wewe unatokea Afrika eeenh?Hii inakuwa wazi zaidi pale ninapokuwa nimevaa mavazi ya kiafrika ambayo kwa kweli nayapenda. Mimi hukataa kusema ndio natokea Afrika na badala yake husema hapana natokea Tanzania. Wengi hawaijui Tanzania hivyo swali linalofuatia huwa samahani ipo wapi hiyo nchi? Nimejifunza kutabasamu na kumwambia tafadhali nenda kwenye atlas yako halafu utafute wapi Tanzania ipo. Kwa sababu ya kutabasamu kabla ya kujibu wengi hufanya hivyo.Nisingetabasamu wangesema ni mkorofi na sio ajabu ningeitwa mbaguzi wa rangi.
Sasa mtu huyu akienda kwenye ramani ya dunia au kwenye mtandao atapata mambo mengi kuhusu Tanzania.Na akipata mazuri kama milima,mabonde ya kuvutia na mbuga nzuri za wanyama basi huenda akataka kuitembelea Tanzania. Mtalii huyu,uchumi unafaidika.
Afrika haina sifa nzuri mbele ya watu weupe.Wengi inapozungumziwa Afrika huona cheche za vita vya kidini,kikabila n.k.Picha ya lolote jema la Afrika haipo kabisa. Kwa msingi huo biashara kama ya utalii ambayo ni muhimu kwa uchumi wetu inakuwa ya kubahatisha.Kwani ni kweli kwamba nchi zote za Afrika zina vita?
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba sisi waafrika tuliopo ughaibuni tuna kazi ngumu ya kuzitambulisha nchi zetu binafsi kabla ya kuzizika kwenye umoja wa bara la Afrika.Mbona Ulaya inazungumzwa kwa nchi mpaka nchi?Nani atasema Ufaransa ni Ulaya tu? Ufaransa ni Ufaransa halafu baadaye ndio mojawapo ya nchi za Ulaya. Kwanini Tanzania isiwe Tanzania kabla ya kuwa Afrika?
Msangi,
ReplyDeleteKaribu uwanjani. Tuko pamoja. Uhuru!
Karibu..aaiithee..Umeanza kwa neno zito na inaoneka mwelekeo wako uko makini..
ReplyDeleteBADO NAWEKA MTAZAMO MAKINI!!
Ndugu yangu karibu sana. Lakini unanishangaza kidogo unaoshangaa hawa jamaa zetu wa huko ulipo sasa kuchukulia bara la Afrika kama nchi moja. Unajua kwanini?? Kwasababu wanaona hata sisi tumejijengea utaratibu huo huo, tena basi kuanzia ngazi za chini kabisa. Hukuwahi kusikia maneno ya "Ile ni nyumba ya fulani" na mengine kama hayo? Hivi huwa nyumba hizo zinaundwa na mtu mmoja kweli??
ReplyDeleteShukrani kwa wote walionikaribisha.Naamini siku moja tutafanikisha.Tuendelee kupeana changamoto kwa uhuru bila jazba na chuki.Elimu haina mwisho!
ReplyDeleteKaribu sana kwenye ulimwengu wa blogu bwana Jeff Msangi. Naona unahoja nzito na za msingi sana katika kuleta mapinduzi halisi ya kifikra katika Dunia hii ya utandawazi hasa kwa sisi kutoka ile nchi ya Danganyika kule africa mashariti.
ReplyDeleteKariu sana Jeff. Tunatarajia mengi toka kwako.
ReplyDeleteKariu sana Jeff. Tunatarajia mengi toka kwako.
ReplyDelete