VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Thursday, August 18, 2005
Canada kuna ombaomba?
Majuzi rafiki yangu mmoja amenitumia barua pepe na kuniuliza swali ambalo siku za nyuma katika makala zangu za kila jumapili kwenye gazeti la Tanzania Daima nimewahi kuliongelea.Kwa faida ya wengi nimeona niliweke wazi tena jambo hili na hivi sasa kwenye blogu yangu. Jamaa ameniuliza kwamba "hivi hapo Canada unaweza kukuta ombaomba mtaani?"
Ukweli ni kwamba jiji la Toronto kama yalivyo majiji mengine mengi ya America ya kaskazini ambayo nimepata bahati ya kuyatembelea yamejaa yana ombaomba wengi tu.Nilipokuja Canada kwa mara ya kwanza wakati huo Umoja wa Mataifa ukiwa unaisifia Canada kuwa sehemu namba moja nzuri kwa binadamu kuishi ilikuwa vigumu kuamini kwamba wale jamaa waliopo Yonge Street na Bay ni ombaomba. Ndio maisha yao na hawana jinsi nyingine ya kuishi na mbaya zaidi ni kwamba hata pa kuishi hawana.Kwa maana hiyo hawa ni "homeless" jambo ambalo ni tatizo kubwa sana hivi sasa hapa Canada. Basi ndio kusema kwamba kama kampeni ya Makamba kuwafukuza kina Matonya jijini Dar-es-salaam ingefanikiwa Dar-es-salaam ingekuwa haina ombaomba wakati Toronto ingebakia ikiwa na lukuki. Nilichokigundua pia ni kwamba wengi wa ombaomba wa Toronto hawana mapungufu yoyote ya kiumaumbile. Ni watu ambao wangeweza kabisa kufanya kazi na kujitunza.Haya rafiki zangu,ndio dunia yetu hii.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 8:13 PM | Permalink |


Maoni: 1


  • Tarehe: 10:03:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Reginald S. Miruko

    Nashukuru kwa mengi. Mosi, kwa maoni yako kwenye blogu yangu juu ya vijana. Nitajitahidi kukujibu haraka na kukupa orodha yao kamili.
    Pili, kwa mada hii ya ombaomba Canada. Hata mimi sikuwa najua kama wapo, kumbe ni uginjwa wa dunia, lakini 'nakutaarifu rasmi' ombaomba wa Dodoma wanazidi wengine wote kwa wingi na mbinu. Wanaomba kwa staili ya kulazimisha na wakati mwingine wanaweza kuchagua nyama kwenye sahami "naomba hiyo...."

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker