VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Saturday, August 27, 2005
Upo Tayari Kuipigania Tanzania?
Ni rahisi sana kuvua shati,kujipiga kifua,kusimamisha mishipa yote ya fahamu,kulia kwa hasira na kudai kwamba u-mzalendo wa kweli wa nchi,taifa au itikadi fulani. Wengi wetu tukitukanwa kuhusu nchi yetu ya Tanzania( wengi tunasakamwa juu ya umasikini wetu na kuwa ombaomba wezi-viongozi wetu walaumiwe) tupo tayari kuanzisha ligi za mabishano tukitetea utanzania wetu na utaifa wetu. Inasemekana kwamba ukitaka mtanzania apambane na wewe barabara basi tukana nchi yake,sema mbovu kuhusu Hayati Mwalimu Nyerere n.k Katika vipimo vyote vya uzalendo nadhani kikubwa na kigumu kushinda vyote ni kile cha kujitolea maisha yako kwa ajili ya kulipigania taifa lako. Kuingia msituni,kumsaka adui ili kutetea nchi yako.Sio kuingia msituni kupigana na raia wenzako kisa wao ni wa kabila tofauti na lako,kisa wao ni wa chama tofauti cha kisiasa na kile ambacho wewe ni mwanachama wake.

Majuzi nimekaa na kuangalia historia mbalimbali kuhusiana na vita ambavyo taifa la Marekani limewahi kupigana tangu liasisiwe na Columbus. Marekani imepigana na karibuni kila pande ya dunia.Vingi ya vita hivyo vimechochewa na uongo ambao viongozi wake wamekuwa wakiwaambia wananchi wake ili kupandisha mori wakapigane.Baada ya muda fulani wengi wanagundua kwamba sababu waliyopewa dhidi ya vita haikuwa ya kweli.Lakini washapigana na kwa bahati mbaya wanaendelea kupigana vita hizo za uongo mpaka sasa.Nashangaa kwanini watu kama hawa wanaendelea.Wapi akili zao? Ukitaka kujua zaidi vita ngapi wameshapigana hawa jamaa na madhara ambayo wamepata soma hapa.
Tanzania imewahi kupigana vita moja ambayo ilikuwa ni mfano tosha wa uzalendo.Vita vya Tanzania na Uganda(Mimi hupenda kuviita vita vya Tanzania na Idi Amin) vilikuwa ni mfano mzuri sana. Vilikuwa sio vita vya jeshi letu na jeshi la Idi Amin tu bali vilikuwa vya kila mwananchi.Watanzania wengi walijitolea.Wakafundhishwa kushika mtutu na kwenda uwanja wa mapambano.Wengi walipoteza maisha yao (Walale pema Peponi) kwa ajili ya kutetea taifa letu. Ujumbe ukafika,wazalendo wakaonekana!
Pengine ni vigumu na inawezekana sio sahihi kulifananisha taifa la Marekani na nchi changa kama yetu ya Tanzania.Bali uzalendo unabakia kuwa uzalendo,hali na mazingira zinaweza tofautiana lakini uzalendo unabakia. Hivi sasa Marekani ipo kwenye vita huko Iraq.Ingawa kasi ya wananchi wake(hususani vijana) kujitolea kujiunga na jeshi lao wakapigane huko Iraq inapungua bado wengine wanafanya hivyo.Kasi imepungua kwa sababu wengi sasa wameanza kuamini kwamba sio kweli kwamba kuna mtu yeyote ambaye anaonea gere uhuru wao,utaifa wao wala chochote walichonacho. Hivyo ndivyo walivyokuwa wakiambiwa ili wajiunge na jeshi wakapiganie nchi yao.Vita kama vile vya Vietnam vilikuwa ni kinara cha mfano wa jinsi vijana walivyojitokeza kujiunga na jeshi lao ili wakapigane.Hivi leo mmarekani(kijana wa wakati ule)ambaye hakuenda kupigana Vietnam haonekani kama hodari na uzalendo wake hutiliwa mashaka.
Swali moja ambalo ndio kichwa cha habari hii linaumiza kichwa changu(kinaniuma haswa) Leo hii watanzania wangapi wapo tayari kuipigania Tanzania endapo (mungu epushia mbali) vita yoyote dhidi ya nchi yetu itaibuka?Wangapi wanaipenda Tanzania kwa moyo wa dhati wa uzalendo halisi kama ilivyokuwa miaka ya 1979?Jibu ni kwamba wachache.Huo ndio ukweli.Wengi wamechoshwa na wizi na ubinafsi wa viongozi.Wengi wamekata tamaa ya maisha. Iweje nikalipiganie taifa ambalo viongozi wake hawaoni kama mimi pia ni sehemu muhimu ya taifa hilo? Kama wanaona mbona wakatafuna pesa zote za misaada ambazo zinalenda katika kumkomboa masikini?Nikapiganie taifa langu au nikapiganie matumbo yao na yale ya wanafamilia zao, tumalize vita waendelee kutafuna ruzuku? Wakinilaume kwamba mimi sio mzalendo na mimi nitawauliza,uzalendo wao ni wa kuomba misaada kwa hali na mali ili watunishe misuli yao ya ufujaji mali ya umma?
Wakati wa vita ile ya Uganda,kiongozi,kipimo halisi cha uzalendo tulikuwa naye.Leo hii tunaye kweli? Yuko wapi ajitokeze basi.Atuambie bayana kwamba yapi ya kizalendo kweli ambayo ameyafanya katika mwezi huu uliopita tu? Ametoa shilingi ngapi au muda wake kiasi gani kusaidia masikini wanaozidi kujaa Tanzania?Naomba niishie hapa.Machozi yananilengalenga.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 11:41 AM | Permalink |


Maoni: 0


   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker