VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Friday, August 12, 2005
WATANZANIA WALIO NDANI NA NJE
Kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikifuatilia malumbano mbalimbali kwenye mtandao kati ya watanzania walio nje ya nchi na wazalendo waliopo nyumbani Tanzania. Mimi nipo nje ya Tanzania.

Malumbano au mijadala ambayo nimeifuatilia kwa karibu sana imekuwa zaidi ya kutupiana lawama,kashfa na hata jazba. Ningeweza kupuuzia malumbano hayo lakini hisia zangu zinaniambia kwamba matokeo yake ni vita ya chini kwa chini ambayo inaua uzalendo au kujenga uzalendo ambao hauna maana wala msaada wowote kwa nchi yetu.
Wengi waliopo nje ya nchi wamekuwa waongo. Hawasemi ukweli juu ya hali halisi. Wanaofanya hivyo wanaonyesha Ulaya na Marekani kama paradise ambapo kila kitu ni kizuri na hamna mateso na machungu yoyote yale. Hawa watakudanganya kwamba wana kazi nzuri, wamesoma sana na wana matumaini makubwa sana ya siku za mbeleni za maisha yao na ya wanafamilia zao. Hata siku moja hawatakuambia kwamba jana alilala njaa au juzi alitolewa kwenye chumba anachopanga kwa kushindwa kulipa kodi, kazi zake ni za kubangaiza au kwamba hana ajira rasmi. Hatokuambia ukweli kwamba shule alisoma muhula mmoja tu na kwamba chuo alichokuwa akisoma ni mojawapo ya vile vyuo hewa ambavyo havitambuliki popote duniani. Atakuambia uongo kwamba ana miliki gari la kifahari bila kukuambia ukweli kwamba hata hilo la kawaida analomiliki amekopa tu na analipa taratibu hali ambayo inamtoa jasho kweli kweli. Hatokuambia kwamba kwa sababu ya elimu yake ndogo na uzoefu finyu wa kazi basi hufanya kazi nzito za kubeba maboksi na vitu vizito usiku wa manane ambapo wataalamu wamelala nyumbani na familia zao.

Uongo huu hivi sasa umezaa chuki iliyopo. Maendeleo ya kitechnologia yanawezesha mambo mengi kuwa hadharani. Waliopo nyumbani na waliopo huku sote tunaanza kujua ukweli kirahisi zadi ingawa wengi Tanzania wanabakia gizani kwa sababu mtandao bado haujaenea ipasavyo. Uongo huo unaoanza kuyeyuka umejenga tama mbaya sana miongoni mwa watanzania haswa vijana. Ndoto zao zinakuwa za kuja Ulaya na Marekani tu. Hawa hawafikirii jambo lingine lolote. Ukiwauliza wanajiona kwamba wao ni wapiti njia tu katika nchi yao wenyewe. Wengi hawataki kusoma, wengi hawataki kutafuta ajira ya aina yoyote. Kisa na mkasa, wako bize wakijiandaa kwenda Ulaya au Marekani. Wengi wanasema shule ya Tanzania ngumu sana na kudai kwamba Ulaya au Marekani unapata digrii kama mchezo tu. Nawaelewa, si ndugu na marafiki zao waliopo majuu wamewadanganya kwamba wao wameshapata digrii. Akijiuliza ndugu yake au rafiki yake alikuwa mjinga wa kutupwa, leo ana digrii! Kumbe uongo mtupu.

Waliopo Tanzania nao hawapo Tanzania kwa sababu wanapenda kuwapo Tanzania. Vijana wangapi kati ya kumi ni wazalendo wa kweli hivi leo na ambao hawako tayari kuiacha nchi yao kukimbilia Ulaya na Marekani? Tuambiane ukweli jamani, ni mmoja au wawili kati ya kumi. Wengi wananitumia barua pepe na kuniambi niwafanyie mpango wa kuja huku. Wanasema wako radhi kuja huku na kufanya kazi za aina zozote. Lakini utaratibu mgumu wa kupata viza ndio kikwazo sana katika kutimiza ndoto zao. Waombaji wengi wa viza kutoka nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hunyimwa.

Matokeo yake ni kuanza kwa chuki ambayo naiona hivi sasa. Wengi wakishanyimwa viza hujenga chuki na nchi zilizowanyima viza hizo. Utasikia mtu akikwambia “mimi Marekani sitaki kabisa kuisikia”. Ukichunguza unaambiwa kwamba majuma machache yaliyopita huyu bwana alinyimwa viza ya kuja Marekani. Kinachosikitisha ni kwamba chuki yake hiyo inakuwa sio tu dhidi ya Marekani bali inahamia hata kwa watanzania wenzake waliopo Marekani. Hapo ndio utaanza kuitwa msaliti, mkimbizi na majina kadha wa kadha. Lawama zinatolewa kwamba waliopo Ulaya na Marekani sio wazalendo. Wazalendo ni wale waliopo nyumbani wakijaribu kujenga nchi zao. Imefikia hatua ambapo hawa waliopo huku wanaambiwa hawana haki ya kukosoa mambo mbalimbali yanayoendelea nchini mwao kwa sababu hayawahusu. Kama wana uchungu sana na nchi yao kwanini basi wamekimbilia na kutokomea mashariki ya mbali?

Jambo ambalo makundi yote haya yanasahau ni kuhusu uzalendo halisi na nani ni adui wetu mkubwa. Uwe ndani au nje ya nchi. Uzalendo halisi ninaoutamani mimi ni kwamba waliopo ndani ya nchi wasiwe na jazba dhidi ya walio nje ya nchi. Halikadhalika waliopo nje ya nchi wasiwe na chuki na dharau dhidi ya wenzao waliopo nchini na nchi yao kwa ujumla. Waliopo nchini wajue kwamba wapo pale kwa sababu maalumu. Kujenga taifa lenye nguvu kiuchumi, kidemokrasia, kisiasa na kijamii. Waliopo nje nao wajue kwamba kuwepo nje ya nchi hakuna maana kwamba kuipa kisogo nchi yao. Kama ulizaliwa na kukulia Tanzania utabakia kuwa mtanzania kwa maisha yako yote. Makaratasi na pasi za kusafiria havibadilishi utanzania wako. Ndugu , marafiki na jamaa zako wanabakia Tanzania. Vizazi vyako vinabakia Tanzania. Kuponda na kukosoa mabaya kuhusu Tanzania bila kusifia japo mazuri machache au kutoa mapendekezo ya msingi jinsi ya kutatua matatizo hakuna msaada kwa yeyote yule. Mchango wako unahitajika..sio kwa kashfa na majivuno hewa. Mchango wa kweli.Hivyo basi adui yetu anakuwa huyu anayekuambia kwamba ukiwa Ulaya na Marekani uige utamaduni wa hapa kwa maana ule wa kwako ni mbovu. Wajinga hukubaliana na hili na hapo ndio unapata watu ambao wanaichukia nchi yao wakiwa nje na hata wakibakia ndani mwake.

Binafsi nakubaliana na utaratibu wa kale kabisa. Kwamba wapo wachache ambao wataenda nchi za magharibi kusoma na kujifunza mbinu mpya. Hawa wanatakiwa kurudi nchini mwao ili kutumia ujuzi walioupata kwa manufaa ya nchi zao na vizazi vyao. Wengi wamekuwa hawafanyi hivyo kwa kuchelea mifumo mibaya ya kiuongozi na kiutendaji katika nchi zao. Changamoto inakuja kwa viongozi hawa tunaotaka kuwachagua hivi karibuni kujiuliza kwamba kwanini wasomi hawarudi kujenga nchi zao. Ni ukosefu wa uzalendo tu au kuna lingine? Nchi zetu zinahitaji wasomi wa aina zote, wa ndani na nje ya nchi ili kuendelea zaidi. Sasa chuki dhidi ya nchi yako au wananchi wenzako kwa sababu tu hawapo au wamebaki nchi inasaidia nini? Sote inabidi tujifunze uzalendo halisi. Tujue nini maana ya kuwa watanzania. Tusipinge uhuru wa kuelezana ukweli kwa jazba. Kila tunaloambiwa tulitafakari na kulichuja. Kama ni la msingi na linafaa tulifanyie kazi.Tupendane tujenge nchi yetu.Uwe nje au ndani ya Tanzania haijalishi.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 1:22 PM | Permalink |


Maoni: 2


  • Tarehe: 9:17:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

    Nimepita kwa mara ya kwanza kiundani katika blogu yako kaka. Nashukuru kwa kuusema ukweli huu. Ni rahisi kulaumu ukiwa umekaa jukwaani, lakini kabumbu kulicheza huchezwa uwanjani, kama namba haupati, haidhuru toa mchango kilabuni kilabu kiendelee, au kama uko mbali japo kwa njia ya posta. Hakuna Yanga damu, wala mamluki, wote yanga tu.

     
  • Tarehe: 8:21:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    Kaka msangi! umeongea meengi sana kuhusu uzalendo! kimsingi mimi mzee wangu alikuwa na kichwa kizuri sana na aliombwa abaki ufaransa afanye kazi alipoenda kusoma shahada za uzamili lakini akakataa mshahara mnono ili aje amsaidie nyerere kujenga nchi! jambo jema, lakini ubinafsi miongoni mwa viongozi ndio umeua uzalendo miongoni mwa wananchi! hatukatai kiongozi mzuri anatokana na jamii nzuri lakini kiongozi mbinafsi ana uwezo wa kuathiri jamii kwa kazi ya mwanga! je kwani sio siri kuwa Tanzania katika moja ya vigezo vya kuitwa umasikini kidunia ni nchi ambayo madaktari hawatoshi? vifo vya kina mama wajawazito ni vingi? je umeona jinsi wahishimiwa sana walivyowanyanyapaa madaktari pale muhimbili? kama mimi ni daktari nina weza kweli kuwa na uzalendo? kingine ambacho ni cha hatari sana, hawa wahishimiwa wanapata support toka kwa fukara wa maisha na mawazo ambao bado ni wengi sana (bado moshi wa mwenge u mwingi kwenye mapafu yao). kama ni umasikini mbona majirani zetu wnaweza kuwashika vyema madaktari wao? kimsingi kilichoua uzalendo ni kukusekana kwa uhuru miongoni mwa wananchi! mie mara za mwanzo nikitembelea nchi za watu, nilikuwa nabishana nao kuwa sisi sio masikini kwani japo hela ni ndoko lakini kwa shilingi 250 (robo centi) ya dola familia inakula kutwa!. baadae nilipoanza kujifunza system zinapofanya kazi niligundua kuwa nilikuwa nachensha! je ni vema kumlalia mkulima wa nyanya? ataendeleaje?atasomeshaje mtoto? awamu ya pili ikawa ni kujisikia aibu kuwa kwanini tuna hali mbaya hivyo wakati mazingira yalikuwa na still ni mazuri kutuwezesha? ndo chanzo cha kudiffer na mwalimu!! sasa basi ni kweli ukiingia kwenye chat room za taznaia utagundua wale waliomo kwenye Tanzanian church wanaona kuelimishwa ni tusi na kuendelea kufa kiume na Tanzania! ni tofauti kidogo kwani nimeona mfano kwenye cat room za wenzetu wa nchi jirani, kuchat na mtu aliye exposed zaidi huwa ni fursa ya mwananchi aliye ndani kujiendeleza na hatima yake kubadili maisha yake na ya wale wanaomzunguka! ndio maana nasema makala hizi zikisomwa mara kwa mara zitawakomboa watu waliomilikiwa na tanzanian churh!

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker