Sehemu ya Yonge Street ilipo Zanzibar ya Toronto.
Zanzibar ya Toronto
Mojawapo ya mambo au sehemu zenye vituko na shughuli za kila aina hapa Toronto ni mtaa unaoitwa Yonge Street. Huu ni mtaa mrefu kuliko yote duniani! Una urefu wa kilomita 1896.Ukiufuata mtaa huu unafika mpaka Marekani. Hakuna jambo ambalo halipo au halifanyiki katika mtaa huu. Biashara haramu zote zinafanyika mtaa huu, karibuni matukio yote ya kijangili na ujambazi yanafanyika katika mtaa huu.Kali ya yote ni sehemu iitwayo "ZANZIBAR". Sasa kama mnavyojua visiwa vyetu vya Zanzibar vinapendeza sana na ni kivutio kizuri sana cha biashara ya utalii.Lakini pia vinajulikana kwa maadili mema ya kidini na uungwana.Asilimia 95% ya wakazi wa Zanzibar ni waislamu na washika dini. Mambo ni tofauti kabisa na sehemu hii inayoitwa Zanzibar hapa Yonge Street-Toronto.Hapa ndipo nyumbani kwa "shetani".Kila aina ya ufuska unaoujua wewe unafanyika hapa sehemu iitwayo Zanzibar. Wengi wa watu niliowauliza kama wanajua visiwa vya Zanzibar vilivyoko Tanzania walisema hawajui! Jamaa mmoja akaniambia kwamba kama kuna sehemu ambayo ni Zanzibar original basi angependa kuitembelea.Nikamuuliza kwanini akaniambia sasa kama hapa wanaiga tu huko kwenyewe si kutakuwa zaidi ya hapa? Sikupata muda wa kumueleza zaidi kuhusu Zanzibar kwenyewe.Juhudi zangu za kumpata mmiliki wa sehemu hii ili anieleze chanzo au sababu za kupaita Zanzibar hazikuzaa matunda.Nitaendelea kumfuatilia.
Kaka lazima tujichunguze kwanza sisi Watanzania kwa ujumla... yawezekana sisi ndio kipimo cha "ushetani?" labda wanamaana ni viongozi wetu.