VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Sunday, September 25, 2005
KWANINI SISI ZAIDI?
Ningali najiuliza kuhusu suala hili.Majibu ninayoyapata na kujaribu kuyafikiria mimi mwenyewe bado hayaniridhishi.Hivi ni kwanini ukimwi unatumaliza zaidi waafrika wakati ufedhuli,uhuni,ufisadi na uchafu wa kila aina unafanyika zaidi huku nchi za magharibi?Mbona wao hawafi kama sisi?
Najua wengi tunapumbazwa na kisingizio cha umasikini.Uongo.Umasikini umeshamiri dunia nzima,hata hapa magharibi.New Orleans mliyoiona ipo hapa hapa Magharibi. Umasikini wa hali ya juu kabisa ule.Huku ndio nyumbani kwa umalaya.Ukitaka mwanamke au mwanaume wa kulala naye unaangalia kwenye kitabu cha orodha za simu rasmi kabisa,pana kona yao.Wanaita "escort".Huku ndio nyumbani kwa madanguro ya kila aina,kuna kona zinaitwa za kuchua(massage) .Kinachofanyika huko ni zaidi ya massage.Usenge umehalalishwa na kutambuliwa kisheria.Talaka zimeshamiri huku na sababu inayoongoza ni ukosefu wa uaminifu,uhuni na umalaya.Usije ukaniambia kwamba wao wanatumia sana kondomu.Siamini kwa sababu matumizi ya kondomu yanahubiriwa zaidi huko Afrika,sio huku.Huku suala la kondomu ni kama haliwahusu vile.

Msukumo wa shughuli zote hizi ni umasikini na ukosefu wa ajira.Sitaki kuongelea tamaa za mwili kwa sababu hilo ni suala la binadamu wote.Kwa hiyo suala la umasikini ni la dunia nzima.Nimewahi kuwaambia kwamba huku pia kuna ombaomba wa kila aina.Usishangae.
Naendelea kujiuliza,sasa kama uchafu wa kila aina una makazi rasmi huku kwanini moto uwakie Afrika zaidi? Kuna mkono wa mtu? Kuna ajenda ya siri jamani? Kondomu zinazoletwa huko ni thabiti kweli? Hivi mnakumbuka wakoloni walikuja kutafuta nini barani Afrika enzi hizo?Sote tunajua kwamba hawakuondoka kwa kupenda. Leo hii tukimalizika kwa ukimwi ,hawatotaka kurudi bila vipingamizi vingi? Si unaona wanavyotaka kwa udi na uvumba kurudi? Ubinafsishaji na utandawazi ndio mbinu yao hivi sasa.
Majuzi nilihudhuria kikao cha masuala haya haya.Jamaa akatupa lawama kwenye mila na tamaduni zetu.Ndoa za mke zaidi ya mmoja.Nikamuuliza kama mume mmoja ana wake wanne na wote hawatoki nje ya ndoa hiyo,ukimwi utaingilia wapi?Kizunguzungu.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 2:18 PM | Permalink |


Maoni: 2


  • Tarehe: 4:18:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Indya Nkya

    Msangi hili suala linatisha. Linaleta maswali mengi sana. Lakini hadi leo asili ya virusi bado ni kitendawili. Vilitoka wapi? Kuna falsafa nyingi sana. Je kirusi cha HIV kinasababisha UKIMWI. Bado kuna ubishi kisayansi. Ni mchanganyiko wa mambo mengi mno. Wanasayansi sasa wameondoka maabara na kuamia jukwaani kubishania UKIMWI kwa sababu maelezo ya kisayansi hayatoshelezi. Msome Peter Duesberg guru la Molecular biology huko Carlifonia Berkely ambaye sasa kanyimwa pesa za utafiti kwa sababu ya kutaka uthibitisho wa kisayansi kuhusu HIV. Huyu alikuwa mtarajiwa wa kupata nishani ya Nobel lakini alivyoanza kuhoji kashughulikiwa. Soma www.virusmyth.com na www.duesberg.com

     
  • Tarehe: 8:48:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Alafu wanasema virusi vinaletwa na Waafrika wenyewe eti waafrika wanalala na manyani.. jamani wanatufedhehesha utakuta wazungu wanapita mitaani afrika wanawagaiya watoto weusi pipi zile pipi mimi nikimbizanaga na wale watoto na wanyanganya kwa sababu najua zin madhara makubwa sana ndani yake. hivi ninyi mnaokaa huko maghaibuni mmeshaona waaafrika wanaopita mitaani wakiwagaiya watoto wakizungu pipi?? nina hakika itakuwa ni nima kubwa kwa huyo mgawaji mweusi.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker