Monday, September 05, 2005
UNATUMIA INJINI GANI?
Leo Canada na Marekani ni siku ya kazi.Mei Mosi yao huwa ni jumatatu ya kwanza ya mwezi wa tisa.Nimepata muda mzuri wa kujisomea masuala mbalimbali zaidi kutoka kwenye mtandao.Nimetafuta kila habari ambayo nilikuwa napanga kuitafuta siku za karibuni.Katika kutafuta jambo kwenye mtandao wengi tunatumia injini za kutafuta(search engines).Najua walio wengi hutumia google au yahoo? Mimi huchanganya zote hizo na zingine kutumia mbwa wangu.Na wewe unatumia wako?Kama sivyo basi jaribu hapa na uone kama anakufaa.Mapumziko mema kwa waliopo huku na kazi njema waliopo sehemu nyingine za dunia ikiwemo Tanzania.
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 4:16 PM
|
Permalink |