VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Monday, October 17, 2005
ETI TUMUENZI NYERERE!
Wiki kama ya leo mwaka 1999 Tanzania na bara la Afrika lilimpoteza shujaa wake mkuu Mwalimu Julius K.Nyerere. Tanzania imeihalalisha siku ya tarehe 14 kila Octoba kuwa siku ya Mwalimu Nyerere.Kinachofanyika katika siku hii ni kumkumbuka au kukumbushana juu ya yale ambayo Nyerere aliyaamini,kuyakemea nk.Misingi ya uongozi bora huchimbuliwa tena kwenye siku hii. Lakini kubwa limekuwa ni lile la kujaribu kuangalia kwa undani juu ya sifa zake za uongozi na utumishi wake kwa umma ili iwe changamoto kwa viongozi wengine watarajiwa na wale waliopo madarakani.Kinachofanyika ni hotuba na hotuba,makongamano na makongamano,warsha na warsha.Shughuli zote hizi zinatiwa baraka na matumizi ya jina la hayati Mwalimu Nyerere.

Pamekuwepo na makundi mawili katika haya.Moja ni lile la watu wa hali ya chini ambao wanamkumbuka Nyerere kwa uchungu huku wakiamini kabisa angelikuwa hai bado basi mambo yasingekuwa kama yalivyo.Kundi lingine ni lile la wenye nacho ambao wanaomba mungu usije ukatokea muujiza huyu bwana akafufuka kwa sababu walipo sasa yeye asingeruhusu kabisa wawepo.Wanajijua wenyewe,sitowataja majina.

Nimekuwa nikifuatilia unafiki wa wanasiasa na viongozi wetu mbalimbali pindi wanapoombwa kumzungumzia Nyerere.Utasikia juu ya sifa zake za uadilifu,unyenyekevu,utu wake ,uelewa wake,uchapa kazi wake,uungwana wake na jinsi ambavyo aliichukia rushwa na sifa kem kem ambazo baba wa Taifa ametangulia nazo.Kinyaa kinakuja pale utakapomsikia kiongozi huyo huyo akiwaasa wenzake juu ya kuiga mfano wa Mwalimu katika uongozi wao.

Hivi kweli jamani,ni kiongozi gani hivi leo anaweza kusimama na kusema kwamba yeye anajaribu japo kwa robo tu kufuata mfano wa Nyerere? Hawa wanaokuambia hadithi hizi si ndio wale ambao mifukoni mwao,pale pale waliposimama kuna kitita cha fedha ya rushwa ambayo ametoka kuipokea muda mfupi kabla hajafika hapo kuhutubia?Si ndio hao hao wanaosisitiza juu ya kilimo wakati hawajui hata swahibu moja la ukulima huo usio na masoko wala pembejeo?Hivi kweli kuna sababu ya kusimama kwenye jua kuwasikiliza wanafiki hawa wakimuongelea Nyerere? Tunamkumbuka Nyerere au tunakumbushwa juu ya uchungu wa kuondokewa na kiongozi kama yeye ambaye alikiri pale alipokosea?Ambaye aliwapenda wananchi wake kuliko alivyojipenda yeye mwenyewe!
Utasikia tumuenzi ,tumuenzi baba wa Taifa.Hivi huna aibu wewe uliyesimama mbele hapo ukituambia upuuzi kama huo?Nani wa kumuenzi Mwalimu zaidi,sisi wananchi wa kawaida au wewe kiongozi madarakani?Tunaambiwa tudumishe yale mazuri ya Mwalimu.Tunataka kuyadumisha lakini tutafanyaje wakati uongozi unanuka rushwa na janaba la uhuni?
Hivi kweli Mwalimu huko alipo anawaona wanafiki hawa?Tuambieni ukweli,kwamba mmeshukuru kwamba mwalimu amefariki dunia ili pasiwe na mtu wa kuwasemea mbovu? Hakuna tena zile memo kwamba unaitwa Msasani kwa mzee! Tuache unafiki jamani.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 2:33 PM | Permalink |


Maoni: 9


  • Tarehe: 3:07:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    "I find the great thing in this world is not so much where we stand,
    as in what direction we are moving: To reach the port of heaven,
    we must sail sometimes with the wind and sometimes against it, but
    we must sail, and not drift, nor lie at anchor."

    Oliver Wendell Holmes, Jr.
    oscars

     
  • Tarehe: 4:14:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Indya Nkya

    Umegonga kwenyewe. Unafiki, unafiki, unafiki. Nakuambia acha kabisa. Kungekuwepo na mashndano ya unafiki basi ndio Tanzania tungeweza kuchukua kombe la dunia.

     
  • Tarehe: 7:45:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    ukweli ni kwamba walikuwa wanamuona huyu babu gundu na wamefurahia sana kifo chake. kwa sababu wote wlioko madarakani ni waroho tuu wa pesa za wananchi na kazi yao kuwaza ngono wakishaweza kukwapua hizo pesa ili waweze wakawarukie wakina dada wakiwa ni viongozi wenzao au watakaowakuta pale mtaani haijalishi ni wachafu kwakeli kama huyo Rais mkapa na mke hawatosheki na chakula wanakula wanajitapisha wanarudi tena mezani. na hawa viongozi wengine kazi zao kupambisha moto ushoga wanaenda kuokota mashoga alafu wanajifanya wanawake mashoga wakubwa kama yule balozi wa Tanzania nchini uing..... na mwingine yule sal... Ahm....sal laana ya mungu iwashukie wanafiki wakubwa.

     
  • Tarehe: 6:08:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    ukweli ni kwamba walikuwa wanamuona huyu babu gundu na wamefurahia sana kifo chake. kwa sababu wote wlioko madarakani ni waroho tuu wa pesa za wananchi na kazi yao kuwaza ngono wakishaweza kukwapua hizo pesa ili waweze wakawarukie wakina dada wakiwa ni viongozi wenzao au watakaowakuta pale mtaani haijalishi ni wachafu kwakeli kama huyo Rais mkapa na mke hawatosheki na chakula wanakula wanajitapisha wanarudi tena mezani. na hawa viongozi wengine kazi zao kupambisha moto ushoga wanaenda kuokota mashoga alafu wanajifanya wanawake mashoga wakubwa kama yule balozi wa Tanzania nchini uing..... na mwingine yule sal... Ahm....sal laana ya mungu iwashukie wanafiki wakubwa.

     
  • Tarehe: 8:39:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    ebwana ee alafu unakumbuka kipindi kile wakati kijana wa mkapa anaoa ee yeye na mkewewakapigana virungu mama akavunjika mkono na baba akatenguka mguu eti wakadai walikuwa wana bishania ukumbi oungo mtupi ni maliwalizoibia wananchi zilitaka kuwatoa roho si unajua mchimba kisima anaingia mwenyewe. jamani yule mama hata lili jengo refu kubwa walilokuwa wanakaa wafanyakazi wa posta pale mjini karibu na IFM si mnalifahamu eee hana hata haya mbaya sana ni bora kwanza watoke madarakani kwa sababu alishaanza kuharibu nchi yetu na ukabila yeye mwenyewe hatuelewi hata ni kabila gani maana Tanzania hatuna wanawake wenye sura mbaya hivyo. yaani ni waizi wametuibia nchi kwa kweli. huyu naye anayekuja madarakani kwa tiketi ya CCM aache uzinzi jamani maana huyu jamaa ni chupi mkoni , eti anadai hachagui habagui atayemzika hamjui sasa kama raisi mwenyewe akiwa hivyo sijui wananchi wake tuweje.
    Na yule mwingine Sumaye pamoja na pesa zote alizoiba pamoja na kutaifisha majengo akishirikiana na wafanyabiashara mbalimbali bado anavaa soksi zilizotoboka, siku hiyo bwana akawa na mkutano na watu fulani hivi etii akavua viatu ili awkw viguu vyake kwenye meza ile kuweka hivi soksi zimetoboka jaaaamani. sasa hivi amefedheheka na kusawajika akifikiria ataenda kuibia wapiiii??
    hivi na yule mapuri nani alimpa cheo, jamani yule baba anamdomo hivi mlishamfatilia?? kwakweli anavisa sana hawa wote kama nyenyere angekuwepo watu wangekuwa wapole ndio hawa wamemuua mzee maana siku ile Mkapa akitangaza kifo mzee alikuwa anacheka cheka siwadanganyi si wote tuliona au mme sahau.
    yaani Tanzania imeibiwa haiko tena kama ingekuwa nchi inaweza kuizwa kila mtu apewe chake atumue ingekuwa poa sana kwa sababu hata hii Tanzania mnaiongelea sijui ni Tanzania gani??? Tanzania haipo limebaki kopo.

     
  • Tarehe: 1:19:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Mazuri ya Nyerere? Alikuwa msemaji mzuri aliyeweza kuutetea uongo ukafanana na kweli.Aliwatisha viongozi waliokuwa chini yake na kuwafanya wamwabudu kama mungu wao. Alikuwa na nguvu ya kushawishi akaitumia vibaya kuwashawishi watu wahamie kwenye vijiji vya ujamaa. Alikuwa msomi aliyengangania sera zake hata kama sera hizo zinaonyesha kila dalili ya kushindwa. Kwa hili alikuwa mpumbavu. Ni wapumbavu tu ndio wasiobadili mawazo.

    Ubaya wa Mwinyi? Alibambikizwa uongozi ambao hakuwahi kuuota. Alifanywa kama robot inayofanya kile inachoamriwa kufanya, Mpaka siku alipofanya kosa la kujiamulia mambo kama rais wa nchi, ndipo Nyerere alipomkemea hadharani kwamba anaongozwa na mkewe.

    Huo ndio uliokuwa ubaya wa Mwinyi AL HaJI. Napatwa na kichefuchefu ninapowasikia watu wakisema Nyerere alileta amani Tanzania. Aliileta kutoka wapi? Watanzania walikuwa na amani ambayo haikuwahi kupotea hata siku moja. Nyerere aliwaogopesha watanzania na wala hakuwaunganisha kama alivyotaka ulimwengu uelewe

    . Kwangu mimi Nyerere ni mtu aliyekufa bila kufanya kile alichofikiri kuwa alikiamini. Hakuwa na mawazo yake mwenyewe, bali alijikita zaidi katika kuwaiga akina Mao na wakomunisti wengine duniani. Baada ya miaka mitano Nyerere hatakumbukwa kwa lolote Tanzania, na huo ndio utakaokuwa ushahidi wa kutosha kwamba waovu wanapokufa na mambo yao yanakufa. Mpaka sasa nawasikitikia akina Mkapa kwani wanatumia mawazo yaliyokufa ya Nyerere kuiongoza Tanzania ya walio hai. Ndio maana ninasema kuwa CCM imezeeka na haifai kuiongoza Tz.
    Munishi.

     
  • Tarehe: 1:23:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    hivi unajua watanzania wana ujinga sana hebu amkeni huyu nyerere hamfai hata kumtaja ndo amewafanya muwe hapo mlipo leo hii. yAANIA AMEWARUDISHA NYUMA NA NYIE BADO MNAKUBALI KUKAA NYUMA.

     
  • Tarehe: 1:25:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Huyu Idya anasema keli unafiki kweli kwa sabaabu huyo madaraka ni rafiki yenu basi mnaogopa kusema ukweli kupingana nae mtu anapaswa kueleweshwa kama wote mnakuwa wanafiki sasa itakuwaje.

     
  • Tarehe: 3:45:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Twende na wakati! Asema Ochieng

    Nyerere aliwanyonya watanzania bongo zao wakawa hawafikiri.Waliimba zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM. Hiyo ilionyesha kuwa wao wenyewe walikuwa hawafikiri. siyo ajabu wakimuona Munishi akifikiri na kuandika maoni yake, wanamtuma Hospitali akapimwe akili.



    Nyerere "aliwabrainwash" Watanzania wote.Tunashukuru Munishi kutufahamisha hayo. Unaonekana wewe ni mmoja wa hao ambao bongo zao zilikufa na Nyerere. Wewe ndiye unayetakiwa kwenda na wakati.Ujue kwamba kutoa maoni siyo kosa la jinai kama Nyerere alivyowafundisha.

    Ochieng Nairobi

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker