VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Saturday, October 29, 2005
MJADALA UNAENDELEA
Majuzi nilianzisha mjadala kuhusu huu muziki tunaouita wa kizazi kipya.Nikagusa wengi.Nashukuru kwamba wengi tunakubaliana kwamba mashua ya mziki huu ina matundu makubwa sana.Safari haielekei kuwa safari. Mojawapo ya maoni yaliyotolewa ambayo yamenigusa ni kutoka kwa dada yetu mmoja anayeishi Uingereza anaitwa Fatma Karama.
Nimeamua kuyaweka hapa ili wote tuyaone,mjadala uendelee

"Kwakweli Tanzania kuna tatizo kubwa sana, vijana wengi hawajipendi, hawajithamini wala hawajichunguzi wakajijua wao ni akina nani. Wengi kazi yao ni kuiga tuu, watu wamekuwa walemavu wa akili.Watu hatujifunzi kulingana na makosa ambayo yamekwisha tokea, umeona huyu yule na yule ametoka na staili ya kizungu hajawika, hajapendeza na wala hajauza rekodi zake kimataifa nawe unarudia hivyo hivyo.Halafu kila siku wanajiuliza kwanini nyimbo zetu haziuzikiiiii eti tatizo ni soko upuuzi mnene. Tanzania inanguo nyingi tuu za kupendeza sana kama wale waman'gati jamani mananguo zinazopendeza mpaka unachoka. nguo zipo, masoko yapo, lakini hatutaki kufanya research kabla ya kufanya kazi. Kila mtu anayeingia kwenye muziki Tanzania swali lake ni hilo hilo. Nyimbo zitauzika vipi wakati nyie wenyewe hamjikubali, hamjitaki, mnajidharau, hamjitukuzi. Mnataka kutukuza tuu wageni. Ndo maana nyie vijana hamchukuliwi ng'oo kutumbuiza kwenye matamasha makubwa makubwa. Watabakia haohao kina bi kidude nao wakichoka kabisa ndo basi tena tumebaki olaa. kama mwingine Mtanzania hapa uingereza anitwa Christopher Saprapasen namtaja ili ajibadilisha na aache tabia za kitumwa. siku moja akanisikia nasikiliza nyimbo za kitanzania akaniambia heee, ndo nyimbo gani hizo hebu weka hip hop bwana eti anajifanya black-british tayari. nikamwambia mtumwa mkubwa weee, nikamuuliza umepitia mlango gani kuingia hapa? haya toka upesi kabla sijakurusha dirishani. "
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 3:56 AM | Permalink |


Maoni: 6


  • Tarehe: 1:24:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Ndesanjo Macha

    Fatma kawa mkali kabisa. Namuunga mkono asilimia zote zilizopo duniani. Hatujijui, hatujipendi, hatujiamini. Tutabaki tukiota ndoto za muziki wetu kukubaliwa kimataifa hadi siku nani hii atakapokuja mara ya tatu...(hiyo sentensi ya mwisho nimepiga dongo fulani kwa kinamna...)

     
  • Tarehe: 4:41:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Awali ya yote: Bi Fatma,

    Nimesoma maoni yako na kalipio lako kali kwa huyo kijana Saprapasen nimebakia nacheka kutwa nzima. Asante sana dada.

    Jana nilipita dukani nikakusanya CD tatu za Taarab: Culture Musical Club (Waridi), Ikhwani Safaa Musical Club-1905-2005 A Hundred Years of Taarab in Zanzibar (Zanzibara 1) na 1965-1975 Golden Years of Mombasa Taarab (Zanzibara 2). Katika cd ya Waridi ya Culture Musical Club kuna nyimbo na 3 Njoo iliyoimbwa na Mzee Makame Faki nimeisikiliza mara kadhaa tangu nitoke dukani na leo sasa hivi ninayo hapa ofisini nitaichomeka niisikilize mara nyingine na nyingine na nyingine tena na tena na tena.

    Jamani nyie! hawa watoto wa kizazi kipya hawajui wanazinyima nini roho zao kwa kusikiliza makelele yale wanayoyasikiliza. Kizazi kipya muziki gani ambao haupigiki mluzi? Muziki unajengwa na nguzo tatu mdundo (rhythm), melody (sauti), na vikolombwezo (harmony)kwa wataalam wengine wanaongeza maneno (lyrics). Kizazi kipya ni muziki unaojengwa na mdundo na maneno. Midundo ya miziki ya kizazi kipya wala haina ustadi, midundo yake yote ni ya kawaida iliyotengenezwa kwenye vinanda. Baadhi ya nyimbo za kizazi kipya zina maneno mazuri lakini nyingi ya hizo ni upuuzi mtupu. Hata kama wana ujumbe mzuri wanapungukiwa lugha ya picha ya kumkuna msikilizaji. Ukisikiliza sauti ya miziki hiyo ambayo huwa inatengezwa na vinanda hupati shauku wala ashki ya kuiimba wala kuucheza.

    Soko la muziki linajengwa kwa uzuri wa muziki. Muziki kama sanaa nyingine huwa inalenga kugonga milango ya fahamu (to appear and appeal pleasant to the senses, in music especially the ear). Miye siongei Lingala lakini ni mshabiki mkubwa wa Hayati Franco Luambo Luanzo Makiadi na Hayati Pepe Kalle, siongei Kijaluo lakini namsikiliza D O Misiani na Shirati Jazz, hata wakati nilipokuwa sijui Kiingereza nilipenda miziki ya Osibisa, kina Slim Ally and Hood Boys, Stevie Wonder, Jackson 5, na wengineo. Kwa sababu miziki hii iligonga milango ya fahamu zangu. Nakumbuka kulikuwa kuna kipindi RTD kilikuwa kinaitwa Ombi Lako baadhi ya waombaji katika kipindi hicho walikuwa wanafafanua vizuri sana kwanini wanaoomba miziki waliyokuwa wanaoomba. Kama mtakumbuka wengine walikuwa wanasema " Ndugu mtangazaji naomba kibao cha Mayasa cha Dar International, Wana Super Bomboka kilichotungwa na Jabali la Muziki Marijani Rajabu Mwana wa Manyema- kwa sababu kibao hicho kinanipa raha sana kwa ujumbe wake mzito na vyombo vilivyopangwa vizuri. Nikiusikia wimbo huu hata nikiwa nakula huwa naacha kula. Tafadhali naomba sana usinitie kapuni.." Ukimsikiliza mwombaji huyu utaelewa kwamba muziki wa WanaSuper Bomboka umemgonga fahamu zake. Tofauti na sasa ni kwamba miziki haigongi fahamu isipokuwa inasilibwa kwenye fahamu kwa kuisikia kila mahali kuanzia kwenye radio, madisko, maonesho, televisheni, magazetini na kwenye matangazo mbali mbali. Kwa hiyo wengi wa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya hawakunwi na muziki bali ni maamuma wa vyombo vya kuongoza akili (thought controlling facilities). Bwana Mwandani analiita suala hili maopiamu: yale madawa ya kuzorotesha uwezo wa akili kufanya kazi yenyewe.
    Haya mauzauza(kwa maneno ya swahiba wangu Mchungaji Christopher Mtikila) ya kiazi kipya yamezagaa dunia nzima lakini wenzetu wamejua kuchambua kati ya pumba na mpunga.
    Kuna nchi kama Kameruni wao walikuwa na mpango mahususi wa kitaifa wa kuinua miziki yao kwa hiyo miziki ya kiajabu ajabu ikawekewa vikwazo. Ukisoma historia ya kukua kwa muziki wa Reggae utakuta kwamba wale mashababi wa nywele ngumu na macho mekundu walikuwa wanatumia hadi mitutu kuondoa maopiamu kwenye redio za Jamaika. Kaburu na ubaya, unyama, na upuuzi wake wote hakuruhusu maopiamu yaingie kutibua muziki wa Afrika ya Kusini. Pamoja na kuwapa nafasi wanamuziki wa kizazi kipya Mwingereza kila siku anabadilisha jina la paketi "The Beatles Love Songs" "The Best of The Beatles" "The Beatles Anthlogy" The Beatles this The Beatles that" Rolling Stones This Rolling Stones That. Hawa kizazi kipya hakuna hata mmoja atakayeitwa kuonana na Malkia Mtukufu Elizabeth asiye na jina ukoo wala mume.
    Marekani na nchi zote za ulaya zina miziki yake ya kitaifa. Ukienda kwenye madisko ua karaoke unaweza kucheza na kuimba usiku mzima nyimbo za nchi hiyo bila kukuta hata nyimbo moja ya kigeni.

    Masalaam, watakabahu, ni miye maridhiya,

    F MtiMkubwa Tungaraza

     
  • Tarehe: 10:37:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    jamani Fatma ana vituko sana nimecheka kweli leo, alafu mjue huyu binti anaakili sana kitu ambacho watu wamekipigia kilele miaka nenda rudi yeye kakipatia ufafanuzi mara moja kwenye maoni yake. hamuoni ni ajabu jamani.

     
  • Tarehe: 8:47:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mloyi

    Umevuka mtego wanaoingia wenzako!
    huo ndio mtego wao mkubwa. Wanakusema ili uwe kama wao. sijui kama wao ni werevu au wajinga kabisa. Nitajitahidi kuiga msimamo wako

     
  • Tarehe: 9:09:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    WE FATMA KARAMA WACHA UONGO SAWA NA TABIA YAKO YA KUCHAFUA MAJINA YA WATU.. MIMI NI CHRIS SAPRA.. KITU CHA KWANZA MIMI SIO MPENZI WA HIP HOP WALA HAIJAWAI KUTOKEA KUPENDELEA HIP HOP, PILI THIS CONVERSATION NEVER HAPPEN NOT I CAN RECALL. 3RD WE NEVER USED TO TALK THAT MUCH MPAKA ULIVYOKUJA KUISHI KWANGU YET WE NEVER REALLY TALK MUCH.

    KWELI UNGENITOA DIRISHANI KWENYE NYUMBA YANGU SI INGEKUWA HATARI KWELI...

    THE MOST IMPORTANT THING YOU SHOULD KNOW ALL THOSE STUFF YOU HAVE WRITE (VIJANA WENGI HAWAPENDI, HAWAJITHAMINI WALA HAWAJICHUNGUZI WAKIJUA WAO WAKINA NANI).. UKWELI THOSE WORDS DOES APPLY TO YOU AS WELL.. WEWE SIO INNOCENT AND YOU KNOW IT VERY WELL OR I CAN SAY WE BOTH KNOW IT. SASA DADA WACHA USIPENDE KU-POINT FINGERS TO OTHER PEOPLE ANZA KUJIANGALIA WEWE KAMA UPO REALLY DIFFERENT FROM ALL THOSE YOU HAVE WRITTEN, WELL HONGERA SANA BUT I DOUBT THAT..

    C SAPRAPASEN

     
  • Tarehe: 9:15:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    WE FATMA KARAMA WACHA UONGO WAKO SAWA NA TABIA YAKO YA KUCHAFUA MAJINA YA WATU..
    MIMI NI CHRIS SAPRA..

    KITU CHA KWANZA MIMI SIO MPENZI WA HIP HOP WALA HAIJAWAI KUTOKEA KUPENDELEA HIP HOP, PILI THIS CONVERSATION NEVER HAPPEN NOT I CAN RECALL. 3RD WE NEVER USED TO TALK THAT MUCH MPAKA ULIVYOKUJA KUISHI KWANGU, YET WE NEVER REALLY TALK MUCH.

    NA KWELI UNGENITOA DIRISHANI KWENYE NYUMBA YANGU?!?! SI INGEKUWA HATARI KWELI...

    THE MOST IMPORTANT THING YOU SHOULD KNOW; ALL THOSE STUFF YOU HAVE WRITE (VIJANA WENGI HAWAJIPENDI, HAWAJITHAMINI WALA HAWAJICHUNGUZI WAKIJUA WAO WAKINA NANI).. UKWELI THOSE WORDS DOES APPLY TO YOU AS WELL..
    WEWE SIO INNOCENT AND YOU KNOW IT VERY WELL OR I CAN SAY WE BOTH KNOW IT. SASA DADA WACHA KUPENDE KU-POINT FINGERS TO OTHER PEOPLE ANZA KUJIANGALIA WEWE NA KAMA UPO REALLY DIFFERENT FROM ALL THOSE YOU HAVE WRITTEN, WELL HONGERA SANA BUT I DOUBT THAT..


    C SAPRAPASEN

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker