VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Monday, October 24, 2005
MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NA UTUMWA WA KIAKILI
Siku chache za nyuma niliandika juu ya kuchipuka kwa umaarufu wa muziki wa kizazi kipya. Pia niliandika kuhusu umuhimu wa kuunga mkono muziki huu unaoitwa wa kizazi kipya ama Bongo Flavor. Kilio changu kilikuwa tuwaunge mkono wanamuziki hawa wa kizazi kipya kwa sababu sio tu kwamba wanatuburudisha bali pia wanatupa utamaduni mpya kupitia muziki. Leo hii inatia raha kuona kwamba shughuli zetu hazitawaliwi tena na muziki kutoka Congo,muziki kutoka Marekani nk. Kiufupi tunakuwa na chetu wenyewe ingawa kimsingi tumeiga kutoka kwenye utamaduni wa muziki wa hip hop ambao ni maarufu sana Marekani miongoni mwa jamii ya watu weusi(black Americans au African-Americans). Tatizo linalojitokeza ni hili la kutojua tusimame wapi,tuendelee kubuni nini na vipi ili mwishoni tusimame na kilicho chetu.Tunapoelekea inaonyesha hatutafika na ndio maana nimeona niandike kuhusu suala hili hivi leo.

Nilipoandika hapo siku za nyuma nilitoa ombi kwa watu kununua cds au kaseti halali na kuachana na ule mchezo wa kurekodi ovyo ovyo bila kuzingatia jasho la msanii. Hoja yangu ilikuwa kama tunataka muziki huu uendelee na pengine baadaye kuwa mhimili na kitambulisho cha vijana wetu duniani kote basi lazima tuunge mkono ili ukue.Njia pekee ya kuweza kufanikisha hilo ni kununua kazi halali za wasanii hao. Sina uhakika kama ombi langu lilisikika au la lakini ninachojua ni kwamba karibuni nitaondoa ombi langu kwa washika dau kwa sababu hatukuzi tena utamaduni wetu mpya bali tunaendeleza umasikini wa fikra na mawazo. Tunazidi kumpa kiburi mtu fulani anayeitwa mmarekani. Ukitaka kuniita mpinga umarekani namba mbili sitakataa kwa sababu naamini matatizo mengi yaliyopo kwenye jamii zetu yana mchango mkubwa wa marekani.Kwani wewe huna habari kwamba kuna watu wanatumia madawa ya kulevya kwa sababu wanaamini huo ni umarekani?Kwani hujui kwamba kuna watu ni mashoga kwa sababu ni umarekani?Hujui kuna kusuka kwa sababu ni umarekani?Orodha ni kubwa sana.

Baada ya kuandika na kutoa maombi yangu nikabakia kuwa mpenzi na mnunuzi mkubwa wa muziki huo. Nanunua muziki halali kwa taarifa yako.Ingawa mpaka hivi sasa nabakia kuwa mnazi wa muziki huu nakatishwa tama na jinsi wasanii wenyewe wanavyotaka kuutangaza muziki huu. Ninashindwa kabisa kuelewa kwamba kwanini muziki huo unazidi kuonekana wa kimarekani siku baada ya siku? Ile chachu ya muziki wa kizazi kipya niliyokuwa naipigia debe inaniangusha kwa kasi ya nyota inayodondoka.Sina jinsi bali kukemea kwa sababu nikikaa kimya mtakuja sema namuogopa mtu.

Majuzi nimeletewa baadhi ya dvd za muziki huo.Jambo moja ambalo lilikuwa wazi kabisa ni kwamba kila msanii wa muziki huo kutoka nyumbani anajaribu kuiga utamaduni wa mtu mweusi wa marekani kwa udi na uvumba.Nimeona katika hizi video watu wamevaa vilemba( tena vya bendera ya Marekani!) hereni ,wamesuka,wakavaa masuruali makubwa makubwa,wakaghani kama vile kina 50 Cent,kina Jay Z nk. Kitambulisho kwa muziki huu unatokea Tanzania hakipo kabisa! Nimejaribu kuwaonyesha watu mbalimbali video hizi na kila mmoja anaponirudishia dvd zangu ananiambia suala moja."Ingependeza zaidi kama wasingekuwa wanajaribu kuiga utamaduni wa kimarekani." Ni dhahiri kwamba kila mtu analiona hilo na halitii mvuto wowote kwa kweli.

Nimejaribu kutafuta kama kuna mwanamuziki wa kizazi kipya anayeendana na utamaduni wa kiafrika bila mafanikio.Nia ilikuwa ni kualika mwanamuziki kutoka Tanzania kwa ajili ya Tamasha la kila mwaka hapa Toronto linaloitwa AfroFest. Sasa nitaanzia wapi kama kila nimuonaye anajifanya mmarekani kuliko hata wamarekani wenyewe? Hivi kweli kuna maana yoyote kumleta mpaka hapa mwanamuziki kutoka Afrika ya Mashariki kisha akuonyeshe jinsi gani alivyo mahiri wa kumuiga Jay Z,50 Cent,Lil’ John nk? Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Ukweli ni kwamba kama wanamuziki wetu wanataka kuuza kimataifa basi ni lazima wajifunze utamaduni mpya.Tuliiga mtiririko wenyewe wa hip hop,sio lazima tuige mavazi na video zao.Kwa mtaji huu hamna mzungu au mmarekani atakayetaka kununua muziki wetu.Kwanini anunue wakati anapata kitu hicho hicho,kwa lugha yake na kwa bei nafuu zaidi kama anataka muziki wa aina hiyo? Lazima wanamuziki wetu wawe wabunifu.Kuiga kidogo sio mbaya lakini hili mnalofanya hivi sasa halitowafikisha mahali popote.Ila kama nia yako ni kuendelea kupata jina kubwa wakati huna senti mfukoni basi endelea na utaratibu wako wa kuwa mtumwa wa kiakili na kimtazamo.

Najua kuna huu utamaduni wa watu weupe siku zote kupenda kutuona sisi waafrika tumevaa majani,ngozi za wanyama tukikata viuno na kuona huo ndio utamu wenyewe.Sina hakika kama sisi wenyewe tunapenda kuonekana hivyo. Lakini kama hatupendi basi hatuna budi kuboresha muziki wetu kwa kubuni na kujivunia mavazi yetu,(sio ngozi na majani) miondoko yetu nk. Hapo ndio muziki wetu na wanamuziki wenyewe wataingia kwenye ulimwengu wa muziki kimataifa.

Nimewahi kusoma kwenye magazeti na mitandao mbalimbali inayowapa sifa hewa watanzania kwamba hivi sasa mwanamuziki fulani anakuwa wa kimataifa kwa sababu amealikwa kufanya maonyesho Marekani,Canada,Uingereza nk. Kwangu mimi kama unakuja hapa kutumbuiza watanzania waishio hapa basi wewe bado sio wa kimataifa. Utakuwa wa kimataifa pale muziki wako utakapouzika kwa watu wa jamii na tamaduni zingine,pale utakapopanda jukwaani kutumbuiza mashabiki wa tamaduni mchanganyiko. Kuna umataifa gani kuja kunitumbuiza mimi na rafiki zangu tuishio hapa Toronto? Kupanda ndege ndio umataifa ndugu zangu?

Hivi kuna ugumu gani wa mwanamuziki fulani wa bongo flava kuamua kuvaa mavazi ya kiafrika tu?Mbona yanapendeza na kukubalika dunia nzima? Hivi kujiita msanii,kioo cha jamii ndio kuturudisha nyuma kwenye lindi la utumwa mamboleo?Hapa Canada mavazi ya kiafrika ni ghali kuliko nguo za aina zote. Unaona sifa gani kuvaa nguo iliyoandikwa Toronto,New York,Washington nk wakati hujawahi hata kufika sehemu hizo? Unapata nini kutangaza utamaduni wa mkoloni wa Ulaya na Marekani. Au unamlaumu kwa nguvu Nyerere na wenzake waliomtimulia mbali mkoloni? Kama sivyo mbona unajaribu kwa udi na uvumba kumuenzi?Hivi ukionekana na nguo iliyoandikwa Dar-es-salaam, Morogoro,Mwanza,nk ni ushamba?

Utumwa mbaya kabisa wa akili huanzia hapo.Unapoona kwamba chako sio bora bali cha mwenzio.Unapoona kila kizuri ni cha mzungu. Jogoo lililonona ni la mzungu,kuku mweupe ni wa kizungu,nyumba nzuri ni ya kizungu nk. Kama huthamini mavazi yaliyotengenezwa nyumbani kwetu Tanzania kwa kuyanunua na kuyavaa,kama huthamini bidhaa za kwetu,kama huthamini mazao ya kwetu unalalamika nini kuona hali ya uchumi inazidi kuwa mbaya? Kwanini unaenda kununua machungwa yaliyotoka Afrika ya Kusini wakati yale ya Lushoto ni bora zaidi? Kweli raisi anafaa kulaumiwa katika hili?Wewe kama mwananchi unasaidia vipi kukuza uchumi wa nchi?Wanasiasa ni waongo,wanafiki,wauza nchi na wewe je?

Wenzetu wa Afrika ya magharibi wanaheshimika kwa kushikilia tamaduni zao ingawa sio wote wafanyao hivyo na sio kwamba tamaduni zao zote ni nzuri. Mavazi yao yanathaminiwa dunia nzima. Je hawapendezi katika mavazi yao?Upuuzi huu wa kutothamini mavazi fulani ndio hupelekea siku nyingine ukialikwa kwenye tafrija fulani unaambiwa kwamba vazi rasmi ni suti nyeusi.Si wanajua kwamba huna chako cha kujivunia au unacho ila hukitaki? Nani anaweza kumualika raisi Obasanjo na kumuambia lazima avae suti? Kataa! Shati la kitenge au wax sio nguo?Kwanini uvae suti nyeusi vazi ambalo sio lako,usikubali kuwa mtumwa wa kiakili ndugu yangu
.Jivunie chako.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 1:48 PM | Permalink |


Maoni: 17


  • Tarehe: 4:40:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Indya Nkya

    Pole Msangi. Nimeshawahi kubishana sana na baadhi ya watu kuhusu hicho kinachoitwa muziki wa kizazi kipya. Hoja yangu ni kwamba kama nataka CD ya Hip Hop kwa nini nisichukue ya mwanamuziki wa Marekani ambayo imepigwa na kurekodiwa vyema kuliko ya Mtanzania yenye mapigo yaleyale lakini kwa lugha ya kiswahili na ambayo ubora wake si mzuri? Kipya kwenye huo muziki ni lugha ya Kiswahili tuu. Ukienda nje ya nchi ukitafuta CD za Tanzania huzioni. Watu wanataka kitu kipya ambacho ni tofauti kabisa na nchi nyingine. Wanaangalia mapigo na si lugha. Acha sasa wanaiga kuvaa nakadhalika. Hatari

     
  • Tarehe: 10:50:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Ndesanjo Macha

    Msangi, hii makala imekaa kisawasawa. Natamani wangeelewa unachoongelea hapa. Kilichofanya Hukwe Zawose akawa mwanamuziki anayejulikana kimataifa (kwa tafsiri ya "kimataifa" uliyoitoa ambayo nimekubaliana nayo) ni jambo unalozungumzia: kutumia utamaduni wake kama silaha katika ulimwengu wa muziki wenye ushindani mkubwa. Ndio maana unaona CD zake nyingine ni bei ghali kuliko hata wanamuziki wakubwa wa Marekani wenye majina na kila kitu. Utofauti, wengine hawajui, ni mtaji. Unaona Fela aliamua kabisa kuanzisha muziki wake. Remmi naye akawa na namna yake akawa anachukuliwa kuhudhuria matamasha ya WOMAD na Peter Gabriel. Sikilizia akina Keita, Oryema, Ndour, na wengine wa kule Magharibi. Makala poa Jeff.

    Na hoja ya Nkya nayo nakubaliana nayo: kama nataka muziki wa kimarekanimarekani kwanini nisinunue uliotoka Marekani kabisa?

     
  • Tarehe: 4:25:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Indya Nkya

    Nilijaribu kuvinjari madukani kutfanya utafiti kuhusu muziki wa Tanzania. Nakuhakikishia nimeikuta CD ya Zawose tuu. Sasa uliza ni watanzania wangapi wanamfahamu Zawose. Utashangaa. Utumwa huu sijuhi utaisha lini jamani!!

     
  • Tarehe: 11:43:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger patashika

    kwakweli Tanzania kuna tatizi kubwa sana, vijana wengi hawajipendi, hawajithamini wala hawajichunguzi wakajijua wao ni akina nani. wengi kazi yao ni kuiga tuu watu wamekuwa walemavu.watu hatujifunzi kulingana na makosa ambayo yamekwisha tokea, umeona huyu yule na yule ametoka na staili ya kizungu hajawika hajapendeza na wala hajauza rekodi zake kimataifa nawe unarudia hivyo hivyo Alafu kila siku wanajiuliza kwanini nyimbo zetu haziuzikiiiii eti tatizo ni soko upuuzi mnene. Tanzania inanguo nyingi tuu za kupendeza sana kama wale waman'gati jamani mananguo zinazopendeza mpaka unachoka. nguo zipo, masoko yapo, lakini hatutaki kufanya research kabla ya kufanya kazi. kila mtu nayeingia kwenye muziki tanzania swali lake ni hillohilo. Nyimbo zitauzika vipi wakati nyie wenyewe hamjikubali, hamjitaki, mnajidharau, hamjitukuzi. Mnataka kutukuza tuu wageni. Ndo maana nyie vijana hamchukuliwi ng'oo kutumbuiza kwenye matamasha makubwa makubwa. watabakia haohao kina bi kidude nao wakichoka kabisa ndo basi tena tumebaki olaa. kama mwingine Mtanzania hapa uingereza anitwa Christopher Saprapasen namtaja ili ajibadilisha na aache tabia za kitumwa. siku moja akanisikia nasikiliza nyimbo za kitanzania akaniambia heee, ndo nyimbo gani hizo hebu weka hip hop bwana eti anajifanya black-british tayari. nikamwambia mtumwa mkubwa weee, nikamuuliza umepitia mlango gani kuingia hapa? haya toka upesi kabla sijakurusha dirishani.

     
  • Tarehe: 3:08:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Nani kawambia kuwa huo ni mzki wa kikazi kipya! Hoja hii niliifungia lakini nadhani nianze na wewe, Jeff je unaamini huo ni mziki wa kizazi kipya na una maana gani kusema hivyo? Naomba kwanza nifahamishw hili kisha nitachangia baadaye tena

     
  • Tarehe: 3:10:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Nani kawaambia kuwa huo ni mziki wa kizazi kipya! Hoja hiyo nilikuwa nayo nikaitunza lakini naona sasa yafaa nihoji nanyi mnieleze kabla ya kuanza kuwatafutia staili ya kuwabainbisha twapaswa kuhoji hili jina wanalijiita!

     
  • Tarehe: 8:08:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Boniface,
    Ninaposema muziki wa kizazi kipya ninaangalia zaidi umri wa wanamuziki wenyewe.Naelewa kwamba kimsingi mfumo na staili ya muziki huu sio mpya tena hususani tutakapoangalia historia yake.Natumaini tupo pamoja.

     
  • Tarehe: 9:06:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Egidio Ndabagoye

    Hii ni mada lazima niitafutie utafiti kwa hawa wanamuziki nina marafiki zangu ambao wanaimba miziki hii

     
  • Tarehe: 7:59:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    hgiu

     
  • Tarehe: 2:03:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Nimekuelewa Jeff, lakini fikra mpya licha ya kuwa kuna wakati hujengwa na mhimili mkongwe lakini zapaswa kuratibiwa ili kuumba umbo ambalo halikuwahi kusadifu mboni za macho ya hadhira mpya.

    Mtazamo huu haukutumika tangu awali na ulifanya muziki huo kupewa hadhi ya umbo jipya lakini ukitazama mantiki yake inabaki kuwa kazi zilizonakshiwa lugha mpya tu!

    Si jambo la kushangaza sana maana niliwahi kufuatia baadhi ya nyimbo za vijana hao na kubaini kuwa kuna zile walizotafsiri na kisha kujipatia hakimiliki ya kuuza katika soko la Tanzania.

    Kunahitajika fikra za king'amuzi na pia mtazamo wa thamani ya soko. Kama hili likiangaliwa twaweza fika, maarifa huambatana na lengo maridhawa la maarifa hayo kwa mhusika. Kama lengo ni kuwaburudisha watanzania kwa kutafsiri nyimbo za akina P. Diddy ili wazielewe vema basi wamefika lakini kama wana taswira ya kufika soko la ng'ambo kuna kazi wanatakiwa kufanya.

     
  • Tarehe: 2:50:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Awali ya yote: Bi Fatma,

    Nimesoma maoni yako na kalipio lako kali kwa huyo kijana Saprapasen nimebakia nacheka kutwa nzima. Asante sana dada.

    Jana nilipita dukani nikakusanya CD tatu za Taarab: Culture Musical Club (Waridi), Ikhwani Safaa Musical Club-1905-2005 A Hundred Years of Taarab in Zanzibar (Zanzibara 1) na 1965-1975 Golden Years of Mombasa Taarab (Zanzibara 2). Katika cd ya Waridi ya Culture Musical Club kuna nyimbo na 3 Njoo iliyoimbwa na Mzee Makame Faki nimeisikiliza mara kadhaa tangu nitoke dukani na leo sasa hivi ninayo hapa ofisini nitaichomeka niisikilize mara nyingine na nyingine na nyingine tena na tena na tena.

    Jamani nyie! hawa watoto wa kizazi kipya hawajui wanazinyima nini roho zao kwa kusikiliza makelele yale wanayoyasikiliza. Kizazi kipya muziki gani ambao haupigiki mluzi? Muziki unajengwa na nguzo tatu mdundo (rhythm), melody (sauti), na vikolombwezo (harmony)kwa wataalam wengine wanaongeza maneno (lyrics). Kizazi kipya ni muziki unaojengwa na mdundo na maneno. Midundo ya miziki ya kizazi kipya wala haina ustadi, midundo yake yote ni ya kawaida iliyotengenezwa kwenye vinanda. Baadhi ya nyimbo za kizazi kipya zina maneno mazuri lakini nyingi ya hizo ni upuuzi mtupu. Hata kama wana ujumbe mzuri wanapungukiwa lugha ya picha ya kumkuna msikilizaji. Ukisikiliza sauti ya miziki hiyo ambayo huwa inatengezwa na vinanda hupati shauku wala ashki ya kuiimba wala kuucheza.

    Soko la muziki linajengwa kwa uzuri wa muziki. Muziki kama sanaa nyingine huwa inalenga kugonga milango ya fahamu (to appear and appeal pleasant to the senses, in music especially the ear). Miye siongei Lingala lakini ni mshabiki mkubwa wa Hayati Franco Luambo Luanzo Makiadi na Hayati Pepe Kalle, siongei Kijaluo lakini namsikiliza D O Misiani na Shirati Jazz, hata wakati nilipokuwa sijui Kiingereza nilipenda miziki ya Osibisa, kina Slim Ally and Hood Boys, Stevie Wonder, Jackson 5, na wengineo. Kwa sababu miziki hii iligonga milango ya fahamu zangu. Nakumbuka kulikuwa kuna kipindi RTD kilikuwa kinaitwa Ombi Lako baadhi ya waombaji katika kipindi hicho walikuwa wanafafanua vizuri sana kwanini wanaoomba miziki waliyokuwa wanaoomba. Kama mtakumbuka wengine walikuwa wanasema " Ndugu mtangazaji naomba kibao cha Mayasa cha Dar International, Wana Super Bomboka kilichotungwa na Jabali la Muziki Marijani Rajabu Mwana wa Manyema- kwa sababu kibao hicho kinanipa raha sana kwa ujumbe wake mzito na vyombo vilivyopangwa vizuri. Nikiusikia wimbo huu hata nikiwa nakula huwa naacha kula. Tafadhali naomba sana usinitie kapuni.." Ukimsikiliza mwombaji huyu utaelewa kwamba muziki wa WanaSuper Bomboka umemgonga fahamu zake. Tofauti na sasa ni kwamba miziki haigongi fahamu isipokuwa inasilibwa kwenye fahamu kwa kuisikia kila mahali kuanzia kwenye radio, madisko, maonesho, televisheni, magazetini na kwenye matangazo mbali mbali. Kwa hiyo wengi wa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya hawakunwi na muziki bali ni maamuma wa vyombo vya kuongoza akili (thought controlling facilities). Bwana Mwandani analiita suala hili maopiamu: yale madawa ya kuzorotesha uwezo wa akili kufanya kazi yenyewe.
    Haya mauzauza(kwa maneno ya swahiba wangu Mchungaji Christopher Mtikila) ya kiazi kipya yamezagaa dunia nzima lakini wenzetu wamejua kuchambua kati ya pumba na mpunga.
    Kuna nchi kama Kameruni wao walikuwa na mpango mahususi wa kitaifa wa kuinua miziki yao kwa hiyo miziki ya kiajabu ajabu ikawekewa vikwazo. Ukisoma historia ya kukua kwa muziki wa Reggae utakuta kwamba wale mashababi wa nywele ngumu na macho mekundu walikuwa wanatumia hadi mitutu kuondoa maopiamu kwenye redio za Jamaika. Kaburu na ubaya, unyama, na upuuzi wake wote hakuruhusu maopiamu yaingie kutibua muziki wa Afrika ya Kusini. Pamoja na kuwapa nafasi wanamuziki wa kizazi kipya Mwingereza kila siku anabadilisha jina la paketi "The Beatles Love Songs" "The Best of The Beatles" "The Beatles Anthlogy" The Beatles this The Beatles that" Rolling Stones This Rolling Stones That. Hawa kizazi kipya hakuna hata mmoja atakayeitwa kuonana na Malkia Mtukufu Elizabeth asiye na jina ukoo wala mume.
    Marekani na nchi zote za ulaya zina miziki yake ya kitaifa. Ukienda kwenye madisko ua karaoke unaweza kucheza na kuimba usiku mzima nyimbo za nchi hiyo bila kukuta hata nyimbo moja ya kigeni.

    Masalaam, watakabahu, ni miye maridhiya,

    F MtiMkubwa Tungaraza

     
  • Tarehe: 8:41:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mloyi

    Muziki, muziki wa kizazi kipya na siyo kilichopita. Muziki usiona maana kwa wasioupenda lakini ni fahari kwa wanaoupenda, sijui wanaupendea nini? Ufahari? umaarufu? utajiri? lakini hauwapatii vitu hivyo.
    Muziki usioendeleza sanaa, hauna ujuzi wowote na utofauti na jamii nyingine, Muda mwingi mimi ni msikilizaji wa reggae, nikisikia tu na jua hii siyo ya jamaica, siyo ya afrika kusini, lakini muziki huu huwezi kujua labda kwa kusikiliza lugha iliyotumiwa.
    Uvivu wa kizazi kipya nao umeingia ndani yake, huhitaji kupanga vyombo mashine itakufanyia, lakini bado kuna tuzo hutolewa sijui hizo tuzo hupewa mwimbaji au mashine iliyoupanga? Naona ni njia nzuri ya kuzika upigaji wetu wa ngoma, kumbuka ngoma zilivyoweza kukusanya mashujaa wakati wa uvamizi wa kwanza wa afrika kuja kupambana na wavamizi,Sasa leo hazipewi nafasi yake ili tuzisahau uvamizi mwa kizazi kipya ukija tutaweza kuukabili?
    Jeff anasema tununue kazi halisi sio za wizi, (utani) anakuwa kama ndesanjo anayekaribisha ngozi nyeupe ikulu, mimi ninasema tutafute kazi zetu za asili ambazo ni kitambulisho chetu, ndio tuzinunue.

     
  • Tarehe: 12:53:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    lakini sioni sababu hasa ya sisi kupigizana kelele juu ya muziki huu,Wengi wenu mmeongea lakini mtazamo wenu pia bado ni ule ule wa kiotumwa kwamba muziki huu mpaka uuzike ulaya ndiyo nanyi mkubali kwamba umekubalika.
    Na bwana mmoja anadiliki hata kuponda baadhi ya maendeleo yaliyofikiwa na kudai kuwa eti wasaanii hawa uchukua vidio zao kwenye viji hotel.mimi ninafikili hapa tunachanganya kuhusu swala la utamaduni na umaskini,kama mnataka hawa vijana wafanye kazi ya kuutangaza umaskini wa tanzania ulaya mseme lakini sioni mantiki yoyote ya ninyi kuwa ponda hawa vijana wanao jishughurisha na kazi ya muziki huu.Sikatai kwamba wapo wale hambao wanatia dosali muziki huu,lakini mnapaswa kukumbuka kwamba wapo wanaotunga nyimbo zenye mafunzo kwa jamii na wengine wao kazi zao zimetumika katika vipindi mbalimbali vya kuelimisha jamii,Vile vile msisahau kwamba Tanzania ajira hakuna kwa hivyo hawa vijana wanafanya muziki kama kazi na wanakubalika nchini na wengi wa vijana hawa wameachana na tabia mbaya walizo kuwa nazo,kama kukwapua,kubaka,kuzamia na mengine mengi.
    Kwa hivyo kimsingi mimi ninafikili mngelionekana wenye busara kama mngelenga kuwapa ushirikiano na si kuwaponda,kwani swala la hip hop hata marekani kwenyewe lina migogoro kedekede.Mimi ninafikri maisha tunayo ishi ni kielelezo tosha cha utamaduni wetu si jui nyie uko maana hata ninyi mlipaswa kuvaa rubega na sio suti kama mnavyo onekana kwenye tovuti zenu kwani suti hili ni vazi lasmi la mwingereza na ulaya kwa ujumla.Kwa hivyo kimsingi hawa vijana mimi sidhani kama wanastili kulaumiwa kiasi hicho.

     
  • Tarehe: 7:40:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    ewe ndugu unaesema kuhusu kupigizana kelele achia hapo hapo hatusemi kwamba ni lazima muziki uuzwe nje kinacholalamikiwa ni utamaduni kupotea. lakini haya madongo mangine uliyotoa ni kweli kabisa si kwasababu wao wako nje ya nchi sijui nani aliwapa nauli kwa hiyo wanasemea kwa mbali siwaje Tanzania tulione wotw jua alafu ukichunguza wengine hata utakuta wameoa hao hao wazungu tena waache kabisa ngebe zao.

    wenyewe ndo watumwa wakubwa na wala hawajui ni nini kinacho endelea Tanzania kwa undani.

    kuna kina kazi t, renee, na wengineo wengi wanaimba vizuri tuu lakini hawawaoni wanachojua ni kupiga vijembe.

    Unajua hawa jamaa wanachanaganyikiwa maisha huko walipo ni magumu sana kwa hiyo wanapatia faraja kuponda wenzao wanaotanua nyumbani.

     
  • Tarehe: 5:48:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    ndo maana nasema wengi tunaongea tukiwa tumefunga akili

     
  • Tarehe: 8:46:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    WE FATUMA KARAMA WACHA UONGO NA KUCHAFUA MAJINA YA WATU. KWANZA MIMI SIO MPENZI WA HIP HOP WALA SIJAWAHI KUWA MPENZI WA HIP HOP... PILI CONVERSATION ULIYOSEMA HAIJAWAHI KUTOKEA. AND 3RD WE NEVER REALLY USED TO TALK THAT MUCH UNTIL WHEN YOU CAME AND LIVE IN MY HOUSE (SO UNGENITOA DIRISHANI KWENYE NYUMBA YANGU?!?! INGEKUWA HATARI KWA KWELI
    SO USIPENDE KUANDIKA UONGO KWENYE WEBSITES... WILL COST YOU

    C SAPRAPASEN

     
  • Tarehe: 9:20:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    WE FATMA KARAMA WACHA UONGO WAKO SAWA NA TABIA YAKO YA KUCHAFUA MAJINA YA WATU..

    MIMI NI CHRIS SAPRA..

    KITU CHA KWANZA MIMI SIO MPENZI WA HIP HOP WALA HAIJAWAI KUTOKEA KUPENDELEA HIP HOP, PILI THIS CONVERSATION NEVER HAPPEN NOT I CAN RECALL. 3RD WE NEVER USED TO TALK THAT MUCH MPAKA ULIVYOKUJA KUISHI KWANGU, YET WE NEVER REALLY TALK MUCH.

    NA KWELI UNGENITOA DIRISHANI KWENYE NYUMBA YANGU?!?! SI INGEKUWA HATARI KWELI...

    THE MOST IMPORTANT THING YOU SHOULD KNOW; ALL THOSE STUFF YOU HAVE WRITE (VIJANA WENGI HAWAJIPENDI, HAWAJITHAMINI WALA HAWAJICHUNGUZI WAKIJUA WAO WAKINA NANI).. UKWELI THOSE WORDS DOES APPLY TO YOU AS WELL..
    WEWE SIO INNOCENT AND YOU KNOW IT VERY WELL OR I CAN SAY WE BOTH KNOW IT. SASA DADA WACHA KUPENDE KU-POINT FINGERS TO OTHER PEOPLE ANZA KUJIANGALIA WEWE NA KAMA UPO REALLY DIFFERENT FROM ALL THOSE YOU HAVE WRITTEN, WELL HONGERA SANA BUT I DOUBT THAT..


    C SAPRAPASEN

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker