VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Saturday, October 08, 2005
UMAARUFU NA UKIMWI
Dunia yetu imejaaa watu wanaoitwa "nyota".Hawa ni watu mashuhuri,masupa staa,watu wenye kufahamika na watu wa kila rika.Kila nchi ina watu wa aina hii.Baadhi ya watu hawa hufahamila dunia nzima.Kila mtu anayajua majina yao.Hawa ni masupa staa wa dunia nzima.Hata kama hujawahi kupata bahati ya kumuona,utakuwa ushawahi kulisikia jina
lake.Wanamichezo,wanasiasa,watoa roho za watu,wasanii wa fani mbalimbali nk ni sehemu ambazo watu maarufu hutokea.
Mtu akishakuwa maarufu huwa anakuwa kioo cha jamii kwa njia moja au nyingine.Kama amekuwa maarufu kwa mazuri basi kila mtu hutamani kuwa kama yeye,hususani miongoni mwa vijana na watoto.Ukimuuliza mtoto mdogo au kijana kwamba anataka kuwa nani au kufanya kazi gani akiwa mtu mzima atakuambia sio tu jina la fani anayoitamani bali pia atakutajia jina la mtu wake(role model). Kama ulikuwa maarufu kwa mambo mabaya basi kila mzazi anajitahidi mwanae asije kuwa kama mtu huyo.Nani anataka au anamuita mtoto wake Hitler,Bokassa,Idi Amin nk?
Dunia yetu hivi sasa ina tatizo moja kubwa sana.Ugonjwa wa ukimwi.Mojawapo ya lawama ambazo nilipewa katika mikutano yangu mingi ya kuhusu ukimwi na bara la Afrika ni kwamba viongozi wake hawapo mstari wa mbele katika kuzungumzia suala la ugonjwa huu.Nilishangaa sana kusikia tuhuma hizo kwa sababu ninavyoona mimi viongozi wa kiafrika wanauongelea ugonjwa huu zaidi ya viongozi wa huku magharibi.Ni sehemu muhimu sana ya kampeni za kisiasa kuonyesha kwamba unalielewa na kuliongelea suala hili.Takribani maraisi wote wa bara la Afrika huzungumzia suala hili.Kwa bahati mbaya mojawapo ya mifano niliyopewa ni ule ambao sikuutegemea kabisa.Nikaambiwa hukuona jinsi ambavyo Nelson Mandela alichelewa kuweka bayana kwamba mtoto wake wa kiume Makgatho amefariki kwa ugonjwa wa ukimwi?Nilikuja juu sana na kumuomba huyo jamaa atafute mfano mwingine kwa sababu kama Nelson Mandela hayupo mstari wa mbele katika vita dhidi ya ukimwi basi hakuna kiongozi yoyote ambaye yupo,sio Afrika tu bali duniani pote.Nikamwambia mifano ya matamasha ambayo Mandela anaandaa kila mwaka kwa kushirikiana na nyota kutoka huku nk.Nikakasirika na kumuona jamaa mnafiki tu na asiyejua anaongelea nini.
Baadaye na mpaka hivi leo ningali nikijiuliza maswali lukuki.Najaribu kuwaangalia watu mbalimbali mashuhuri waliopo Tanzania.Wale ambao watoto na watu wengine wengi wanatamani kuwa kama wao siku moja.Naangalia pia viongozi mbalimbali na familia zao.Kisha naanza kupata maruweruwe.Hivi hakuna hata kiongozi mmoja ambaye ashawahi kufariki na ugonjwa huu?Hivi hakuna hata supastaa mmoja ambaye amerudi mbele ya haki kwa tiketi ya ugonjwa huu?Ina maana mojawapo ya njia za kuepuka kukamatwa na ugonjwa huu ni kuwa maarufu au kiongozi wa kitaifa? Maana wao hawafi kwa ukimwi ati!!!
Kama sio kiongozi au almaarufu mwenyewe kufariki kwa ugonjwa huu vipi kuhusu hata mwanafamilia yake mmoja?Najua tunaishi kwenye dunia inayozungumzia sana masuala ya haki za binadamu,wanaoishi na hata waliofariki.Lakini kama umaarufu wako au u-kiongozi wako unaweza kusaidia kuepusha watu kushiriki kwenye hizi ngono holela ambao mwisho wake ni kifo unaonaje kama ukifariki au ukipatwa na ugonjwa huu hatari usiweke mambo bayana?Kama unajali kweli kwanini basi usiwe na mirathi inayoishi(living will) kwamba ukifariki kwa ugonjwa wa ukimwi iwekwe bayana?
Wengi hatuamini kwamba aliyekuwa mcheza kikapu maarufu Magic Johnson ni muathrika.Tunaamini kwamba ile ilikuwa ni propaganda tu.Vyoyote vile,je tunahisi watu wangapi waliepuka ngono zembe na holela baada ya tangazo lile la kutisha kwamba Magic ameathirika? Kwanini viongozi wetu wasiige mfano wa Chief Buthelezi wa kule bondeni ambaye ameweka wazi kuhusu jinsi ugonjwa huu unavyochakaza kaa yake?
Hivi sasa karibuni kila familia imepoteza mtu kwa ugonjwa huu.Je kuna haja ya kuendelea kuficha??Nakaribisha maoni .
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 8:09 PM | Permalink |


Maoni: 1


  • Tarehe: 8:00:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Indya Nkya

    Tatizo la unyanyapaa hili Msangi. Lina chanzo chake mbali kweli. UKIMWI umekuja kujlikana kama ugonjwa wa kundi fulani. Magharibi unajua ni ugonjwa wa wasenge na wanaoshirikiana sindano ndio waathirika wakubwa. Dunia ya tatu kuwa na UKIMWI unaonekana kama mwendekezaji ngono hata kama uliupata vinginevyo au ulifanya ngono mara moja na kuupata. tatizo ni kubwa zaidi. Tunafundisha UKIMWI badala ya Elimu ya UKIMWI.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker