Tarehe: 4:27:00 PM, Mtoa Maoni:- boniphace
Tarehe: 10:38:00 PM, Mtoa Maoni:- Jeff Msangi
Tarehe: 6:16:00 AM, Mtoa Maoni:- mloyi
Nadhani bado hujakiaga kiswahili, hivyo hapa utakikubali....
Sio wote tunazungumza kiswahili, hivyo uamuzi wako unaelekea kuwa na lengo la kupanua upeo, wadau kuongezeka, mawazo mapya kuingia na kuwapa nafasi pia.
Endelea hivyohivyo lakini usisahau kwamba hapa bado tunakuhitaji.
...umekumbuka kuiomba msaamaha mizimu kwa kutotumia lugha iliyokaribu nao?...
Tarehe: 8:26:00 AM, Mtoa Maoni:- Ndesanjo Macha
Jeff, uamuzi wako sio mbaya. Unajua tunapoamua kublogu kwa Kiswahili hatumaanishi kuwa tuna ubaya na kiingereza, kifaransa, kichina, n.k. Tunachosema ni kuwa kuna mambo ambayo tunaongea sisi kwa sisi kwahiyo hatuhitaji kutumia lugha ya watu wengine. Pia tunasema kuwa kuna watu wetu wengi ambao hawaelewi lugha ya kiingereza kwahiyo itakuwa ni kosa kubwa kama tunataka kuelimishana juu ya utamaduni wetu, demokrasia, historia yetu, n.k. kwa kutumia lugha ambayo watu ambao tunataka kuelimishana nao hawaielewi. Kwahiyo tunapoongea sisi kwa sisi hatuhitaji hata kidogo kuazima lugha wakati tunayo lugha ambayo wote tunaielewa.
Jambo jingine tunalofanya ni hili ambalo ni sawa na lile ambalo Ngugi aliliandikia kitabu. Kitabu kiliitwa "Decolonising the Mind." Hata ndugu Chinweizu wa Nigeria (Mloyi unampata sana huyu bwana) aliandika kitabu kiitwacho, "Decolonising African Literature." Sasa sisi tunachofanya kwa lugha hiyo ya kimombo ni "Decolonising Blogosphere" au "Decolonising Cyberspace." Tunaondoa ukoloni kwenye ulimwengu wa blogu. Tunaondoa ukoloni kwenye mtandao wa kompyuta. Ukoloni huo ni hali ile inayotulazimisha kutumia lugha waliyotupa wakoloni hata pale tunapoongea sisi kwa sisi.
Na pia bila mjadala wowote, hii ni lugha yetu! Au sio?
Tuje sasa kwenye kiingereza. Kwanza niseme kidogo juu ya lugha. Lugha ina kazi moja kuu: chombo cha mawasiliano. Lakini ina kazi nyingine kuu: lugha ni benki ya maarifa, utamaduni, desturi, na historia. Kutokana na sababu hii unaona kuwa unapotaka kummaliza mtu unamyang'ganya lugha yake. Mtu akipoteza lugha anakuwa amejipoteza. Amepoteza utamaduni na historia yake. Lugha inapopotea duniani ni sawa na kuchoma moto maktaba yenye orofa maelfu na maelfu. Hapo ndio unaona umuhimu wa kutumia zana za teknolojia mpya kutunza historia yetu na kurekodi mambo kwa lugha yetu.
Mimi sina ubaya na kiingereza kama chombo cha mawasiliano. Huwa ninapenda kusema hii hoja mara kwa mara maana watu wengi wanaponisoma wanadhani kuwa nina "siasa kali" dhidi ya kiingereza na ninahukumu Waafrika wanaokitumia. Kumbe sivyo. Siwezi kuwa na ubaya na lugha ambayo inaniwezesha kuwasiliana na watu wengine wema duniani. Inaniwezesha kuwasiliana na kaka na dada zangu Marekani waliochukuliwa utumwani. Imeniwezesha kufaidia mafunzo ya muziki wa Bob Marley. Imeniwezesha kumsoma Wole Soyinka, Dambudzo Marechera, na wengine. Ninatumia lugha hii katika kazi zangu kwenye mradi wa Sauti za Dunia.
Tatizo langu linakuja pale tunapozungumzia lugha kama benki ya maarifa. Hapo kiingereza kinakuwa hakina nafasi kwangu kwani nina lugha nyingine za kiafrika ambazo zinatunza utamaduni na historia yangu. Hapo ndio ninaingia na kampeni yangu ya kublogu kwa lugha za Kiafrika.
Ninapokuja katika suala la kuwasiliana na dunia, nitasema kuwa kiingereza kina nafasi yake na heshima yake. Tena kina nafasi kubwa sana maana tunaishi katika dunia ambayo inatuchambua Waafrika katika mantiki ya njaa, vita, ukimwi, ufukara, n.k. Kwahiyo tunaweza kutumia lugha wanayoielewa hao wanaotuchambua namna hiyo kuwaonyesha afrika ni nini kwetu? Kwamba Afrika kwetu ni zaidi ya vita vya Sudan, mauaji ya Rwanda, utawala songombingo wa Somalia, n.k.
Hongera, Jeff.
Tarehe: 10:20:00 AM, Mtoa Maoni:- Jeff Msangi
congrants Jeff, Blogu yako mpya inazalwa siku ya kuzaliwa kwangu n hivyo nakupongeza maana kweli kwa unayeishi nje ya Tanzania kuna hadhira inayotaka kupata cheche zako na kama ukiandika Kiswahili pekee hawawezi kukuelewa. Niko mbioni kuingia ukurasa huko lakini kwanza ngoja nilikomaze hili Kasri langu.