VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Thursday, November 17, 2005
JAMANI KISWAHILI CHETU!
Waungwana wenzangu,wazalendo,wapenda amani na maendeleo,
Sio nia yangu kuamsha mijadala mikali.Lakini kwa sababu mimi na wewe tunaamini kwamba maendeleo yanatokana na mijadala endelevu huwa sina budi mara kwa mara kujaribu kutegua vitendawili vigumu vigumu vinavyotukabili.

Leo ningependa tupige gumzo kidogo kuhusu muelekeo wa lugha yetu ya kiswahili.Lugha tamu kwa ladha,miundo na inayopendeza masikioni. Lugha ambayo kwa walio watanzania(kama mimi) ni mfano wa umoja wetu,utaifa wetu na kimsingi ni bendera yetu ya kimataifa hivi sasa. Kwa sababu nadhani sote tukijiuliza kwa kina mengine yote tumeshayatupia mbali. Ile amani tuliyokuwa tunajidai nayo sidhani kama ipo tena, ule mlima wetu wa Kilimanjaro tumeshindwa kuutunza ili nao uendelee kututunza na ndio maana kwa ukataji wetu miti ovyo theluji inazidi kuyeyuka na huenda hivi ninavyoandika imekwisha(mtaniambia wale mliopita maeneo hayo siku za karibuni), riadha hatufanyi vizuri kama zamani, soka ndio tumeshasahauliwa kabisa, uchumi hauna haja ya kuuzungumzia wala kutoana macho juu yake. Umoja wetu kama watanzania ni legevu kuliko mlenda.Viwanda tumebinafsisha karibuni vyote kama sio vyote kabisa, madini yetu tumeuza yote. Tumethubutu kuyauza hata yale adimu kabisa dunia nzima ya Tanzanite. Sijui zaidi ya kiswahili,lugha yetu ya taifa tumebakiza nini?

Idadi kubwa sana ya watanzania tunaongea kiswahili.Nathubutu kusema kwamba tunaongea kwa sababu matumizi mengine ya lugha yetu hii ni ya kubahatisha kwa wengine. Kwani uongo? Hivi ni watanzania wangapi wanaweza kusimama mbele,wakajipiga kifua kwamba kiswahili wanakijua mwanzo wake mpaka Kigoma yake? Wangapi kati yetu wanajua miundo mbinu hasa ya kiswahili? Methali,vihisishi,viunganishi, viambishi nk ni maneno magumu sana kwa baadhi yetu. Simlaumu mtu hapa, naweka ukweli tu.Hata mimi mwenyewe kiswahili changu ndio kama hiki unachokisoma hapa.

Kuna maswali ambayo ninataka sote tujiulize. Wangapi kati yetu tunakipenda na kukithamini kiswahili chetu kama kitambulisho chetu thabiti? Wangapi leo wanatamani na mara zote hujifanya wamekisahau pindi wanapopanda ndege kuelekea ughaibuni? Hujawahi kukutana na mtu alikuwa Uingereza kwa miezi mitatu amesahau kiswahili? Hili ni suala la utumwa wa kiakili na mimi na wenzangu kadhaa tunazidi kulikemea lakini wakati huo huo lazima tukiri kwamba bado lingalipo. Wakati tukijiuliza jinsi gani tunakipenda na kukithamini kiswahili chetu sio jambo baya tukaangaliana machoni na kuulizana hivi siku hizi ukitaka kutukana unatumia lugha gani? Ukitaka kumtamkia mwenzako maneno matamu ya mapenzi unatumia lugha gani? Ukiwa ofisini unatumia lugha gani?Katika maneno hamsini unatumia mangapi ya lugha ngeni?

Tukishajiuliza maswali kama hayo tukae pembeni ya moto tukichoma mahindi na kujiuliza kwanini asiyeongea kiswahili huonekana wa maana kuliko sisi tunaoongea kiswahili? Kwanini kwenye foleni kusubiri huduma mbalimbali mwenzetu anahudumiwa kabla yetu?Kwanini mchumba anayeongea kiingereza anaonekana wa maana zaidi? Hivi kuna uhusiano kati ya lugha za kigeni na utajiri hapo kwetu?

Kuna huu mjadala unaoendelea kuhusu lugha gani itumike mashuleni? Mjadala huu sijui umefikia wapi mpaka hivi sasa. Binafsi nashindwa nisimame wapi wakati mwingine. Kiswahili nakipenda,nakithamini,nakitumia kila siku ingawa nipo mbali na wenzangu.Lakini je hii ina maana kwamba nisijifunze na kuzitumia lugha za wengine? Nadhani jibu la busara ni hapana. Sasa kama hapana ni nani anasema kwamba kiswahili ndio kiwe lugha ya kufundishia mpaka chuo kikuu wakati nchi ndio tushaiuza? Waajiri hawa wapya(wakoloni wa zamani) wanataka kweli mfanyakazi maimuna? Huu utandawazi ambao tumeshaingia mwake kichwa kichwa una huruma kweli na kiswahili chetu? Tuambianeni ukweli ndugu zangu,mtego huu hatuwezi kuukwepa. Kiswahili tukienzi lakini tukubali kwamba na lugha za kigeni pia tujifunze.Utumwa mbaya ni ule wa kuanza kukipiga vita na kutokithamini kiswahili chetu. Ukimfundisha mwanao kiingereza tu na ukaachilia mbali kiswahili utakuwa umefanikiwa kumuandaa upya kuwa mtumwa mzuri. Atakuwa hana kitambulisho chake,hana mwanzo wala muelekeo.

Sijui serikali yetu na washika dau wetu wanasemaje kuhusu masuala kama haya.Sijui kama wanaukubali ukweli huu au uongo ule.Sijui pia wana mpango gani kuendelea kushikilia na kutukuza hiki tulichobaki nacho.Najua kuna watanzania wengi hivi leo,hususani vijana ambao wanajifanya kwamba walizaliwa Tanzania kimakosa tu. Kizungu(tena wengi kinawapiga za chenga za mwilini) ndio kitambulisho chao.Acheni.Ukikutana na mzungu leo hapo mtaani kwenu unaanza vipi kusalimiana naye.Jiulize.Kama unaanza kwa maneno hata Hi,Hello,Whats up,How are you ujue tayari ushakuwa mtumwa.Unategemea yeye akiwa huku kwao atakuambia,Habari,Hujambo,nk? Sema usikike.
Nakaribisha maoni.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 6:36 PM | Permalink |


Maoni: 5


 • Tarehe: 8:20:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Indya Nkya

  Kuna hoja nyingine pia kwamba kiswahili nacho kimejaa utumwa mtupu. Sijuhi ni asilimia ngapi ya maneno ya kiswahili ni kiarabu. Wakongo wanasema watanzania ni watu wazuri sana lakini mambo mawili yanawapiga chenga. Moja ni kwamba hwajuhi kiswahili na pili ni kwamba hawajuhi kuvaa suruali. Wanasema wao wanaongea maneno machache ya kiswahili lakini mazito. Tanzania maneno mengi lakini mwepesimwepesi. Hakuna ubishi kwamba kila lugha imetohoa maneno toka lugha nyingine lakini ni kiasi gani tumetohoa? Nitaweka makala moja ya jamaa aliyejadili hoja hii kindani kwenye blogu yangu kupanua huu mjadala.

   
 • Tarehe: 7:14:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Ndesanjo Macha

  Kwanza mambo mawili yamenifanya nicheke: umoja wetu kulegea kama mlenda. Hii umesema Jeff.

  Halafu Nkya ametoa kisa cha Wakongo. Niliposoma nimecheka nikajisema, "Kuna ukweli." Wakongo wanaongea mabomba kweli tena yametoka kwenye lugha zetu na sio maneno ya kutohoa toka lugha nyingine.

  Jambo moja ninalojua ni kuwa Kiswahili pamoja na kuchukua maneno toka lugha ya kiarabu, kishirazi (irani), kihispani, kireno, kijeremani, n.k. kanuni zake ni sawa na zile zinazotumiwa katika lugha nyingine Afrika hasa za Kibantu. Lakini ningependa kujua zaidi kuhusu hili la asilimia.

   
 • Tarehe: 5:15:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Bwaya

  Kiswahili kimeingiliwa, ni wazi. Enhee! hebu tujiulize kidogo ni aina gani ya utumwa tunaounyesha sisi wenye blog zenye kiswanglish? Heading in english, yanayobaki kibantu! Hivi kweli sisi ni wazalendo au tunakopa uzalendo na kuuchanganya na utumwa kidogo ingawa sio sana? Sijui sana ila nadhani nina haja ya kutafuta kubadilika.

   
 • Tarehe: 8:41:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mloyi

  Tunaendelea kupinga na kulaumu, sauti za wanyonge zisizo na sauti. soma nakala yangu mpya.

   
 • Tarehe: 1:39:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  chris haupaswi kubadilika kwa sababu ya mtu au eti mtu kasema sasa huo ndo utumwa wenyewe.

  fata kitu roho yako inapenda na fanya unachofurahia.

  na siamini hili swala la kumuita mwingine mtumwa hilo lenyewe sio kiswahili fasaha litafutwe neno sahihi linaloendana na mambo kama haya mnaongelea na sis neno utumwa neno chafu sana kwa minajili na haswa kwa hapa tulipofikia mnataka kuipa picha gani dunia wanaposoma sisi wenyewe kwa wenyewe tunaitana watumwa. ni bora kutumia neno ulimbukeni lakini utumwa la hasha huku ni kuvuka mipaka.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker