VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Tuesday, November 01, 2005
MJADALA HAUJAISHA
Jamani huu mjadala ndio kwanza unapamba moto, F MtiMkubwa Tungaraza ameweka maoni ambayo sina budi kuyapa kipaumbele ili wote myasome. Unaweza kutembelea blogu ya Tungaraza hapa(sina uhakika kama J Nambiza Tungaraza ndiye huyo huyo MtiMkubwa Tungaraza, mnaojua mtanisaidia) hapa.Maoni yenyewe haya hapa

"Awali ya yote: Bi Fatma,Nimesoma maoni yako na kalipio lako kali kwa huyo kijana Saprapasen nimebakia nacheka kutwa nzima. Asante sana dada.Jana nilipita dukani nikakusanya CD tatu za Taarab: Culture Musical Club (Waridi), Ikhwani Safaa Musical Club-1905-2005 A Hundred Years of Taarab in Zanzibar (Zanzibara 1) na 1965-1975 Golden Years of Mombasa Taarab (Zanzibara 2). Katika cd ya Waridi ya Culture Musical Club kuna nyimbo na 3 Njoo iliyoimbwa na Mzee Makame Faki nimeisikiliza mara kadhaa tangu nitoke dukani na leo sasa hivi ninayo hapa ofisini nitaichomeka niisikilize mara nyingine na nyingine na nyingine tena na tena na tena. Jamani nyie! hawa watoto wa kizazi kipya hawajui wanazinyima nini roho zao kwa kusikiliza makelele yale wanayoyasikiliza. Kizazi kipya muziki gani ambao haupigiki mluzi? Muziki unajengwa na nguzo tatu mdundo (rhythm), melody (sauti), na vikolombwezo (harmony)kwa wataalam wengine wanaongeza maneno (lyrics). Kizazi kipya ni muziki unaojengwa na mdundo na maneno. Midundo ya miziki ya kizazi kipya wala haina ustadi, midundo yake yote ni ya kawaida iliyotengenezwa kwenye vinanda. Baadhi ya nyimbo za kizazi kipya zina maneno mazuri lakini nyingi ya hizo ni upuuzi mtupu. Hata kama wana ujumbe mzuri wanapungukiwa lugha ya picha ya kumkuna msikilizaji. Ukisikiliza sauti ya miziki hiyo ambayo huwa inatengezwa na vinanda hupati shauku wala ashki ya kuiimba wala kuucheza.Soko la muziki linajengwa kwa uzuri wa muziki. Muziki kama sanaa nyingine huwa inalenga kugonga milango ya fahamu (to appear and appeal pleasant to the senses, in music especially the ear). Miye siongei Lingala lakini ni mshabiki mkubwa wa Hayati Franco Luambo Luanzo Makiadi na Hayati Pepe Kalle, siongei Kijaluo lakini namsikiliza D O Misiani na Shirati Jazz, hata wakati nilipokuwa sijui Kiingereza nilipenda miziki ya Osibisa, kina Slim Ally and Hood Boys, Stevie Wonder, Jackson 5, na wengineo. Kwa sababu miziki hii iligonga milango ya fahamu zangu. Nakumbuka kulikuwa kuna kipindi RTD kilikuwa kinaitwa Ombi Lako baadhi ya waombaji katika kipindi hicho walikuwa wanafafanua vizuri sana kwanini wanaoomba miziki waliyokuwa wanaoomba. Kama mtakumbuka wengine walikuwa wanasema " Ndugu mtangazaji naomba kibao cha Mayasa cha Dar International, Wana Super Bomboka kilichotungwa na Jabali la Muziki Marijani Rajabu Mwana wa Manyema- kwa sababu kibao hicho kinanipa raha sana kwa ujumbe wake mzito na vyombo vilivyopangwa vizuri. Nikiusikia wimbo huu hata nikiwa nakula huwa naacha kula. Tafadhali naomba sana usinitie kapuni.." Ukimsikiliza mwombaji huyu utaelewa kwamba muziki wa WanaSuper Bomboka umemgonga fahamu zake. Tofauti na sasa ni kwamba miziki haigongi fahamu isipokuwa inasilibwa kwenye fahamu kwa kuisikia kila mahali kuanzia kwenye radio, madisko, maonesho, televisheni, magazetini na kwenye matangazo mbali mbali. Kwa hiyo wengi wa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya hawakunwi na muziki bali ni maamuma wa vyombo vya kuongoza akili (thought controlling facilities). Bwana Mwandani analiita suala hili maopiamu: yale madawa ya kuzorotesha uwezo wa akili kufanya kazi yenyewe. Haya mauzauza(kwa maneno ya swahiba wangu Mchungaji Christopher Mtikila) ya kiazi kipya yamezagaa dunia nzima lakini wenzetu wamejua kuchambua kati ya pumba na mpunga.Kuna nchi kama Kameruni wao walikuwa na mpango mahususi wa kitaifa wa kuinua miziki yao kwa hiyo miziki ya kiajabu ajabu ikawekewa vikwazo. Ukisoma historia ya kukua kwa muziki wa Reggae utakuta kwamba wale mashababi wa nywele ngumu na macho mekundu walikuwa wanatumia hadi mitutu kuondoa maopiamu kwenye redio za Jamaika. Kaburu na ubaya, unyama, na upuuzi wake wote hakuruhusu maopiamu yaingie kutibua muziki wa Afrika ya Kusini. Pamoja na kuwapa nafasi wanamuziki wa kizazi kipya Mwingereza kila siku anabadilisha jina la paketi "The Beatles Love Songs" "The Best of The Beatles" "The Beatles Anthlogy" The Beatles this The Beatles that" Rolling Stones This Rolling Stones That. Hawa kizazi kipya hakuna hata mmoja atakayeitwa kuonana na Malkia Mtukufu Elizabeth asiye na jina ukoo wala mume. Marekani na nchi zote za ulaya zina miziki yake ya kitaifa. Ukienda kwenye madisko ua karaoke unaweza kucheza na kuimba usiku mzima nyimbo za nchi hiyo bila kukuta hata nyimbo moja ya kigeni. Masalaam, watakabahu, ni miye maridhiya" F MtiMkubwa Tungaraza
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 4:15 PM | Permalink |


Maoni: 11


  • Tarehe: 7:50:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    unajua wengi tunaimba hizi nyimbo tumeibukia tuu wengine hatujasoma, wengine watoto wa mitaani wengine tulikuwa machangu tuuu kwa hiyo tukiona tumetokea kwenye TV mara moja mbili tunaona tumefika yaani bonge la dili hakuna wa kutufundisha wala kutufungua macho hao mapromota wenyewe ndo mnajua tena pamoja na hayo wengi wetu tumetoka vijijini kwa hivyo tukija mijini tunalimbuka tunafikiri umarekani dili.

     
  • Tarehe: 5:40:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

    Mti mkubwa ni kaka yangu. Mie Nambiza ndio mwandani, siyo mti mkubwa.

     
  • Tarehe: 5:46:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

    Walahi, umenipa elimu. Mada mzuri sana.

     
  • Tarehe: 3:06:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Ahsante Mwandani kwa kunielewesha na samahani kama kuna usumbufu wowote uliojitokeza.Tuendelee kufafanua masuala haya wandugu.

     
  • Tarehe: 6:53:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Ndesanjo Macha

    Jeff, mada tamu mno mno. Mti Mkubwa kataja wanamuziki na miziki ambayo kweli daima itapendwa. Tujiulize, kwanini baadhi ya wanamuziki na miziki yao huwa haina habari ya kupitwa na wakati? Pia kanichekesha anaposema kuwa muziki mzuri lazima upigike mluzi. Hii kweli kabisa. Tunaelimika na kuburudika. Tuendelee kujadili.

     
  • Tarehe: 12:54:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger patashika

    Nyimbo zao zinadumu kwa sababu si madomo kaya, wamekaa chini na kufanya kazi wanayalenga matatizo ya jamii na kufurahia pia mazuri yanayotekelezwa na wanajamii.
    Siti binti saad mwimbaji wa kwanza wa taarabu nchini Tanzania alisema'' taarab ni mbaya ikiwa itaimbwa na mtu domo kaya'' si taarabu pekee ni kila aina ya muziki na kazi pia kama itafanywa kipuuzi nayo pia itakua mbaya.

     
  • Tarehe: 12:28:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    we Mwandani mtimkubwa kakayako unafikiri hatujui eeeeeeeeeeeeeee

     
  • Tarehe: 6:55:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Kwanza napenda kumshukuru MIJA SAYI kwa kuweza kunikaribisha katika huu Mjadala unaozungumzia Muziki wa Kizazi Kipya. Mimi nikiwa kama mmoja wa watu wanaojaribu kuutangaza huu Muziki duniani kote kupitia BONGO RADIO, nimeona nami nitoe yangu machache kuhusiana na aina hii ya Muziki.

    Muziki wa Kizazi Kipya kama wengi tujuavyo ndio umeshika hatamu katika kukua kwa haraka pale Nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Kama tujuavyo huu muziki wapenzi wake wakubwa ni vijana ingawa siku hizi hata wazee utawakuta nao ni wapenzi wa aina hii ya muziki. Mizizi ya aina hii ya muziki kwa kiasi kikubwa imetokea katika Hip Hop ambayo ni aina ya muziki iliyoanzishwa na Wamarekani Weusi wakati wa kupigania haki na pia aina nyingine za muziki pale Nyumbani Tanzania.

    Ni kweli kuna baadhi ya Wasanii ambao nyimbo zao huwa hazina dira wala mafundisho lakini wengi wao hutoa ujumbe mzito na ulio makini. Naona Mwandishi wa Makala hii ameshindwa kuonyesha mafundisho yatolewayo na aina hii ya muziki na kuishia kukumbatia makosa tu ambayo nayo yapo katika hizo aina nyingine za Muziki ambazo amezitaja kuwa ndizo zinazowakilisha muziki wa kweli. Kasi ya Muziki wa kizazi kipya ni kubwa sana na hivi punde tu itaweza kuiteka mioyo ya wengi hata ndugu Mwandishi.

     
  • Tarehe: 7:26:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Geeque,
    Sidhani kama mimi au wachangiaji wengine tunakataa kwamba hakuna mafunzo,kemeo au maono ya msingi katika muziki huu.Tunachojaribu kutanabaisha hapa ni njia gani itumike ili kufikia mafanikio ya kweli ya kimuziki kama kitambulisho cha jamii yetu kimataifa.Hapo ndio suala la umuhimu wa kukumbatia utamaduni,mila na desturi letu linapoingia kati.Kama kuupenda muziki huu wote tunaupenda ingawa tamaa tunakatishwa.Natumaini tumerudi barabarani.

     
  • Tarehe: 11:14:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    geeque mimi sioni kama umeongea lolote la kuipa hoja yako uzito na pia hujaelewa nini haswa watu wanachogombea watu wanachogombe ni utamaduni kupotea, kama ulivyotaja hapo juu kama muziki wa aina hii ulitumiwa na wamarekani kulilia na kuombea haki zao, nasema kuombea kwa sababu sio kwao hawawezi kugombea iliwalazimi waombe. sisi watanzania si wamarekani na hatutakua wamarekani hata siku moja hakuna jambo la muhimu na la msingi hapa duniani kama mtu kujua kichimbuko lake na likukubali. Huoni hata hao wamarekani weusi wenyewe sasa imefikia mahali wanakimbia nchi, mfano mzuri Michael Jackson huoni sasa kaamua kukimbilia Bahrain. Hii inatufundisha nini? jiulize? kwenu ni kwenu na ukiwa kwenu utathaminiwa kwa hiyo ni lazima upaheshimu na kupatukuza kwa kuendeleza mila na desturi zenu hichi ndo kitambulisho chenu duniani kote. kwa hiyo bwana tabia ya kuiga iga inasaidia nini ndo mana wale wamerakani unaona wanatoka na miziki ya kufoka foka hebu jiulize ni kwanini wanafokafoka, wanataka kufikisha ujumbe kwa msisitizo lakini bado hawakubaliki kwa hiyo bwana msiwaone hawa watu mkafikiri wana raha, hawana. kinachowasaidia angalau ni vile mzungu ameanzisha sheria mwenyewe kwa hiyo zinambana ndo maana hawezi kufanya ubaguzi bayana pamoja na hayo anatumia mbinu za kila aina kumfedhehesha mweusi na kumkumbusha hapa si kwenu bwanaaa. kwa hiyo kama nilivyosema kama una kwenu heshimu. hatukatai wote tunacheza hii miziki na kisikiliza sababu hatuna budi unaenda muziki unaisikia, radioni inapigwa kwa hiyo mtu huna budi lakini moyoni unajua kuna makosa na hatusemi kwamba hawa watu hawafanyi kazi wanafanya kazi lakini sio kazi inayoendana na Taifa letu. hicho ndo
    kilio chetu.

     
  • Tarehe: 1:46:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Better tomorrow

    Nimekubaliana na mengi yaliyosemwa likiwepo swala la lugha na maaarifa yatumikayo kutengeneza muziki.Umefika wakati sasa wa wanamuziki wa tanzania kwenda darasani na kujifunza muziki.LUGHA YA PICHA.ama hakika hii ni muhimu..mziki hauyawa muziki usipoweza kupiga mluzi kweli..
    Je wanamuziki wapo tayari kwenda darasani kujifunza ala za muziki?Je watengenezaji muziki nao wapo tayari kuweka upeo wa muziki kwa wateja wao(wasanii)?Ama hakika vijana wazamani waliimba akina marijani Rajabu unakumbuka nyimbo zake kama ZUWENA,HARUSI?

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker