Tarehe: 2:54:00 PM, Mtoa Maoni:- boniphace
Tarehe: 2:05:00 AM, Mtoa Maoni:- mwandani
Jeff, Nafurahi kuwa nawe umeliona hilo. Mwanzoni mwa mwaka huu, mwezi wa tatu au wa nne, kulianza swala hili la kutaka kupata tafasiri ya neno blogu. Pakatengenezwa hata chumba cha kuchangia mawazo.
Lakini kutokana ama pengine na wingi wa shughuli au ukweli kuwa pengine huo haukuwa wakati muafaka wa kutafuta neno jipya, mradi huo wa tafasiri ukaishia hewani.
Wengine walidai kuwa kuwa tafasiri sio muhimu kwani hata neno komyuta lina neno lake 'tarakilishi' lakini wengi wameamua kutumia neno kompyuta... basi wengi wape, ya nini kubadili mambo wakati maneno yaliyopo yanafaa?
Tafadhali tazama nukuu za hapo chini kikiwemo kiuongo hicho, pengine mtapendelea kuendeleza mradi huo kupitia chumba hicho au vinginevyo. Shughuli iendelee. Nashukuru tena kwa kuamsha hisia.
BLOGU, BILOGI, BLOGI !!!?!!????
Haya, kuna ushauri nimepewa na mwenzetu. Tujaribu kuita blogu kwa kiswahili. Hivyo nikidhani kutia herufi U mwisho wa neno ndio tutakuwa tushatafsiri... na neno blog ndio lishabadilika kuwa la kiswahili.
Masihara mbali hebu tuambiane... tupeane ushauri. Mie namuafiki huyu huyu mwenzetu. Nukuu yake isome hapa chini:
Nafurahi kuona kwamba Watanzania tumetumia nafasi ya maendeleo ya teknolojia hii ya mtandao, lakini..., nadhani ni vema kama tutajaribu zaidi (kwani tunajaribu...) kutafuta tafsiri zinazofaa toka ki-ingereza kwenda kiswahili. Kwa mfano "BLOG" tunasema BLOGI au BLOGU, nadhani tungeweza kuita kwa jina ambalo linafanana na mazingira yetu, kwa mfano BARAZA au UBAO au UBAONI. Katika kutafisri tujaribu kuepuka tafsiri kasuku. Ni vema kutafsiri kufuatana na mazingira yetu.Kumbuka UJAMAA, angali ufafanuzi wa neno hili katika kamusi za ki-ingereza.
CHANGIA TAFASIRI
Shukrani ziwafikie waungwana kwa kutoa mchango wenu kutafasiri neno BLOGU kuwa la Kiswahili sawia. Ila nimeng'amua jambo moja kuwa kile kiungo nilichoweka hapo kwenye ujumbe wa awali chini, hakiwezi kutufikisha kwenye chumba cha mjadala. Labda hiyo ndiyo sababu mojawapo inayofanya wengi tutume barua pepe au maoni hapa ndani ya blogu.
Tafadhali baada ya kufuata KIUNGO HIKI ambacho bila ya shaka kitakufikisha, nakili jina la anwani ya ukurasa wa chumba cha mjadala:(http://www.quicktopic.com/31/H/KDFGe3iwuy5Aq) linalotokea kwenye sehemu ya anwani za tovuti juu ya dirisha unalosoma, ili uweze kupata kuingia chumba cha mjadala unapotaka.
Tena nasema, Akhsanteni.
Tarehe: 5:40:00 PM, Mtoa Maoni:-
Nikiwa sipingi hoja yako waziri mkuu (sijui heo hiki ulikwisha kipokea au la) nami naona nichagie kidogo kwa kuungana na mwandani kwa kiasi fulani. Lugha si ugomvi. Sidhani kwa kuwa unakimudu kizungu vema basi fikira zako ni za kitumwa bado kwa wakina Blair na mama Thatcher. Hoja hii imenileta nyumbani kwangu. Zikiwemo kazi zingine za lugha kama vile utamaduni n.k., kazi ya msingi ya lugha ni kuwasiliana na kuelewana.
Kabla sijaenda mbali sina budi kumpongeza aliyejithidi kutumia neno 'blogu' kutoka 'blog' hata sasa twaelewana.
Sasa kama tayari tunaelewana kwa neno blogu basi nafikiri yatosha. Tukumbuke kila lugha ni mdaiwa wa lugha nyingine. Kwa nmaneno mengine kila lugha hukopa kutoka lugha nyingine pale panapo uwazi ama utupu wa msamiati. Ni wazi Kiswahili kilikuwa 'tupu' kwa neno blogu kwani hatukua na teknolojia hii. Kama ni utumwa (huu ni utumwa wa lugha, sio wa uchumi ambao umekupembeja kuwaza hili)basi kizungu ndio lugha tumwa namba moja kwani ni mdaiwa mkuu kutoka takribani lugha zote za hapa ulimwenguni. Mpaka sasa kingereza bado hakijatulipa maneno kama 'safari'(sijui zitakua paundi au dola?).
Lugha haikui kwa jazba za eti hawa walitutawala zamani. Hapana. Tukifanya hivi tutafika pahala ambapo yawezekana hatutaelewana kwani tutajisikia kurekebesha maneno mengi katika kiswahili ambayo yalishibisha lugha hii. Mengi tutakumbuka yalitoka katika Kiarabu, Kireno, Kizungu, Kifaransa n.k. Hebu fikiria haraka haraka maneno machache tu haya halafu yatafutie maneno ya "kiswahili": rais, jamhuri, katiba, ardhi, (Kiarabu)spika, posta, (kizungu).Tukiazimia kuyabadili leo maneno haya na mengine tutabaki mabubu kwani hatutakua ma maneno kwani mvutano na ugomvi mwingine mpya utakuja. Kila mhusika atataka aweke neno la kikabila chake. Mazungumzo kwa kinyakyusa ni "inongwa". Kumbe tutakuja kukuta tunachokifikiria ni Kiswahili kumbe sio. Itakuwaje pale wasukuma watakaposema basi nasi mturudishie neno letu 'ikulu'(yaani msilitumie).
'Hata hivyo mheshimiwa spika naunga hoja'
Tarehe: 11:06:00 PM, Mtoa Maoni:- Ndesanjo Macha
Mwaipopo kaja kwa ukali (sio ukali mbaya bali mzuri sana). Nilitaka kuchangia lakini kanifanya nisite kidogo. Nifikiri. Na labda nijiulize swali ambalo pengine sikuwa nimejiuliza vyema huko nyuma: kwanini hasa tunataka neno jipya? Mwaipopo changamoto kama hizi muhimu sana. Kukua kwa jamii huwa kunatokea kwa kuwepo na changamoto kama hizi...hata zikileta migongano na misuguano ndio jamii inavyokwenda mbele.
Tarehe: 10:59:00 PM, Mtoa Maoni:- Jeff Msangi
Mwaipopo ametoa hoja za maana sana na zilizo na msingi mwema,nyumba inaweza ikajengwa.Labda niseme kwamba kero yangu ni jinsi tulivyolipata hili neno kirahisi,nataka tukune vichwa ili tutohoe letu.Nitafurahi sana kuona kama vile "ikulu" ilivyotoka kwa wasukuma basi blogu(la kiswahili)litoke popote kule kwetu.Iwe ni usukumani,ukereweni,umwerani,utungujani n.k yote sawa.
Tarehe: 6:18:00 PM, Mtoa Maoni:- boniphace
Nilikaa kimya kufikiri sana, niliangalia sana dhima za blog. Nikafananisha dhima hizo na manenmo mengine ya Kiswahili. Kazi kubwa hapam ni habari na upashanaji habari kinachoongezeka ni uhuru katika uchujaji wa habari hizi. Nikaona nipendekeze nami blog kuitwa "Gazeti" dhana gazeti haitoshi maana tunayo maana yake lakini hili gazeti pana, lasambaa na kitendo hiki naweza kifananisha na kutanda.
Hivyo mapendekezo yangu blog iitwe "Gazeti tando" mwandishi wa Blog kwa siku zijazo ambapo Kasri litakuwa limetanuka ataitwa Mwandishi wa Gazeti Tando na mimi nitaitwa Mmiliki wa Gazeti Tando. Vile vile mtoa maoni katika Gazeti Tando nk.
Utakumbuka utando wa buibui, utazame na angalia Magazeti Tando yanavyotanda kwa kasi paso mipaka. Jina hili litakuwa linatokana na muundo wa majina unganishi.
Aksanteni waheshimiwa waungwana naomba kuwapa hoja!
Jeff mara nyingi mgunduzi uhitaji kutulia ili apate fikra za kigunduzi. Hapa naweza kutoa mazingira machache, mosi kulala ukiwaza jambo, pili kufunua historia na vyanzo vya taarifa na tatu kulinganisha jambo na mambo yanayofanana na hilo unalotaka kuligundua.
Nadhani hoja yangu ya tatu inaweza kuwa ya kisayansi zaidi kuliko nyingine mbili. Tunapaswa kufikiri dhima au hata ufafanuzi wa hili neno na hapo twaweza kufika. Kero yangu ya kubadili neno hili ipo asilimia mia na niachie nami hapa ili niweze nami kufanya upembuzi yakinifu ili niweze ng'amua la kufanya baadaye. Nadhani kuanzia kesho itakuwa mjadala wa kubadilishana aina na mapendekezo ya maneno.