VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Monday, December 12, 2005
DUH! BARIDI IMEWASILI
Ni majira ya baridi kali.Yale majira yasiyopendwa na wengi.Wakuja kama mimi hatutaki hata kuyasikia.Wazawa kidogo wanaweza kuyavumilia.Wana kila aina ya shughuli hawa jamaa.Wengine eti wanaenda kuvua samaki kutoka kwenye mito na maziwa kulimojaa barafu.Wanakenua kama watoto wa chekechea.Wakimaliza hapo wanaenda kujirusha kwenye vichuguu vilivyojaa theluji. Lakini pamoja na yote hayo wengi wao huomba majira ya joto yarejee mapema.

Huu ndio wakati wao wa kupeana zawadi za kila aina.Sehemu za maduka zimejaa bidhaa hivi sasa.Televisheni hazitangazi kitu kingine zaidi ya nini umnunulie mwenzako kama zawadi ya mwisho wa mwaka na kwa wale wakristo sikukuu ya kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu.Uongo! Yesu hakuzaliwa mwishoni mwa mwaka.Alipozaliwa wachungaji walikuwa makondeni.Watu hawachungi wakati wa baridi kali namna hii.Nahisi ubepari na misingi yake ya kibiashara ndio vilipendekeza masuala haya.Imani haina uhusiano na ubepari nadhani.

Nimesimama kwenye kituo cha treni tayari kuelekea katikati ya jiji la Toronto ambapo mwendo ni ule wa hakuna kulala mpaka kieleweke.Pembeni yangu wamesimama wapenzi wawili wakifanya karibuni kila kitu kuhusu mapenzi.Walichobakiza nadhani ni kanyusi kumuingila sinyuka tu! Mwanamke analalama kwamba anasikia baridi, jamaa ndio joto la asili. Nataka niwashauri wakatafute "gesti" wamalize haja zao.Looh nakumbuka sipo mitaa ya kati ya jijini Dar,kule ningechukua bakora na kuwatandika.Maadili yetu hayaendi hivyo wajameni.Hapa siwezi kuthubutu. La sivyo nitakuwa gumzo na jela nitaenda.Nitaambiwa siheshimu haki za watu.Hivi hawa jamaa wanajua kuhusu "mfadhaiko"? Shauri yao.

Naelekea mtaa mmoja unaoitwa Yonge(inatamkwa yang) yaani kama vile Yanga bila hiyo a. Inasemekana huu ndio mtaa mrefu kupita yote duniani. Mimi sina uhakika na hilo bwana.Kwanza sijatembelea dunia nzima na pili hawa wenzetu bwana kila jambo lao ni la dunia nzima. Si ushawahi kusikia wale mabingwa wao wa ligi ya mpira wa kikapu wakiitwa mabingwa wa dunia bila hata kucheza na timu za nchi zingine zozote? Hujawahi kusikia zile tunu za muziki wakasema mwanamuziki fulani ndio bora dunia nzima?Kwa wengi wao dunia huanzia hapa na kuishia hapa. Sisi tunaotoka mbali ndio tunajua zaidi yao.Kule kwetu kwenye warembo wa kila aina.Kwenye huduma nzito kama za mama ntilie na mama sukari.Kule kwenye....simalizii.

Naenda kuhudhuria mkutano wa
masuala ya Afrika. Tumeendelea kugundua kwamba picha ya Afrika sio mbaya kama wenzetu wanavyotaka tuamini.Tumeamua kupambana nao kwa kutumia nyenzo za kisasa kama huu mtandao. Pembeni yangu wamekaa vijana wanapiga hadithi ya jinsi majira ya joto yalivyokuwa. Yaani wanakumbushia ule wakati wanajamii wa hapa wanapotembea huku asilimia tisini na tano ya miili yao ikiwa wazi/uchi. Hata sijui uchi unatafsiriwa vipi hapa.

Ndani ya chumba cha mkutano mimi ndio wa kwanza kuwasili.Nilihisi nimechelewa lakini kumbe ule utaratibu wa "Hakuna matata wala haraka Afrika " Huwa hauishii Afrika tu bali huwa tunakuja nao hata huku ughaibuni. Nachelea kumlaumu mtu kwa kuchelewa kufika.Huenda wenzangu waliamua kuendesha magari yao hivyo wako kwenye foleni mbaya za majira haya ya baridi. Huwa napenda sana heshima wanayokuwa nayo madereva wakati huu wa barafu barabarani.Kila mmoja anakuwa makini kuliko kawaida! Nadhani wakati huu polisi wa hapa hawaupendi kabisa. Polisi wa hapa bwana ni kama wakusanya kodi vile.Wanapenda sana kutoa tiketi kwa binadamu wenzao. Halafu kama ulidhani utaratibu wa kujificha vichakani ni wa trafiki wa bongo tu umenoa.Muulize
Ndesanjo kama unadhani natania. Yaani wanapojificha hata huwezi dhania. Utakachoona ni vimulimuli tu nyuma yako. Siku moja nilitaka nisimamishe gari nimuulize polisi mmoja "hivi ukigongwa na nyoka huko vichakani utasema nini"? Halafu unaambiwa eti wanalinda maisha ya mwananchi.Uongo.Nishapita taa nyekundu,nimeshapigwa dafrao la nguvu,wewe ndio unajitokeza huko vichakani kwako.Ungekuwa unaonekana barabarani vizuri ningepita kweli taa nyekundu? Ni mfano tu wandugu,msipite taa nyekundu aisee,hatari sana.Naona jamaa zangu wameanza kuwasili hapa mkutanoni. Baadaye
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 3:07 PM | Permalink |


Maoni: 4


 • Tarehe: 10:35:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Boniphace Makene

  Jeff maana uandishi huu hatari sana kisa unakipanga yaani nimesoma hapa nacheka sana. Hizo tiketi zingekuwa zinatolewa Bongo basi. Kule hatuna ila tunacho kitu kidogo. Kwa nini hawa wanaweza kutoa hizo tiketi na bila kupokea rushwa?

   
 • Tarehe: 11:14:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Ndesanjo Macha

  Moja ya sababu inayofanya wanatoa tiketi na rushwa sio rahisi kupokea ni kuwa kati ya vigezo vinavyotumika kwenye kuongeza mishahara na kupandisha vyeo ni utendaji wa kazi (ikimaanisha jinsi ulivyo mnoko kwa kukamata watu wengi). Ndio maana utakuta askari wabaya kabisa ni wale walioanza kazi majuzi ambao wanataka kupanda vyeo, hawa wanatafuta wavunja sheria kwa udi na uvumba.

  Halafu utagundua pia magari ya polisi yote yana video ya kurekodi kila unachofaya. Na pia utaratibu wa kutoa tiketi umeundwa kwa namna ya kuzuia tabia ya "kuzungumza kidogo." Askari wa usalama barabarani akikusimamisha kwa kuendesha gari bila taa, atakachofanya sio eti atakufuata kwenye gari lako kukuuliza, "Kwanini unaendesha gari bila taa?," kama wanavyofanya nyumbani. Atakusimamisha na kisha ataandika tiketi akiwa ndani ya gari lake na kisha anakuletea na kukukabidhi.

  Hii ni sawa. Kama mtu anaendesha gari bila taa kinyume na sheria kwanini uende ukamuulize, "kwanini unaendesha gari bila taa?" Amevunja sheria, mpe tiketi.

   
 • Tarehe: 1:27:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Kuna makala yangu nimeiweka hapa kwenye blogu yangu upande wa kulia inaitwa Jambazi na mtutu askari na kirungu.Nimejaribu kuelezea utendaji wa polisi wetu nikifananisha na wa hapa.Inaweza kuelezea zaidi nini kinafanyika na wale "ngunguri" wetu wafanye nini.

   
 • Tarehe: 12:39:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger mark msaki

  DEar Jeff, sasa nimekupata! nimependa jinsi ulivyotumia lugha kiufasaha! hadi nimekuonea raha nadhani sio wivu! mungu akubariki sana huko toronto na tuendelee kupeleka merikebu kinyume na mrama!

  akhsante!

  mark

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker