VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Thursday, December 22, 2005
"KAKA NA MIMI NINUNULIE MOJA"
Kawaida huwa naandika waraka huu mapema baada ya mwaka mpya kuanza.Mwaka huu,kwa sababu ni "mwaka wa uchaguzi" basi nimeamua kuandika huu kwanza nikitumaini kuandika mwingine pindi mola atakapofanya kweli.Yaani baada ya ule usiku wenye mbalamwezi(sio sehemu zote za dunia zenye bahati hiyo) ambapo familia,majirani,vijukuu na vitukuu hukusanyika na kuungoja kwa hamu mwaka mpya. Hapa nilipo bado nasikia sauti ya bunduki ambayo babu yangu alikuwa akifyatua pale kanisani pindi saa sita kamili usiku inapogonga.Sijawahi kumuuliza babu kwamba nani alikuwa anamwalika kanisani kufanya "makeke" yale, wala nani alikuwa anampa kibali cha kufanya baadhi ya watu wazima wafanye "msaada kwenye tuta" bila kupenda. Ninachojua mimi ni kwamba alikuwa anaashiria mwaka mpya.Enzi zile kulikuwa hakuna "sumu" ya ari mpya,kasi mpya.Zile zilikuwa ni enzi za "zidumu fikra" za fulani huku wazee wetu wakitulia kama kondoo!!!Walioshtuka wakapinga yaliyowakuta sote tunayajua ingawa ni mara chache kuyasikia yakiandikwa. Rafiki yetu Mark Msaki kutoka kule kwenye shujaa wa karne huwa anaandika sana kuhusu "dhambi" ile.Amini usiamini mpaka hivi leo kuna watu huwa wanairuka ile mistari yake.Aibu kubwa.Mark endelea na mwendo huo huo.
Usiku ule huwa umetawaliwa na mambo mengi sana.Kuna wale wanaokuwa kwenye vilabu vya pombe,wakinywa na kushangilia kwamba mwaka mpya umewasili. Hawa huwa wanakuwa wale wasioogopa ule uvumi kwamba mwaka mpya ukikukuta kwenye pombe basi mwaka mzima unaofuatia wewe utakuwa "bwana chapombe",ukikutwa safarini basi wewe "msafiri" mwaka mzima nk.Ukikutwa kwenye ngono basi cha mtema kuni utakiona. Tena nimekumbuka,hivi kilichompata mtema kuni ni nini? Tafadhali anayejua nisaidie. Nakumbuka rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa hana "gavana" na masuala ya ngono alijitahidi sana ili awe "juu ya kiuno" mwaka mpya unapoingia ili mwaka mzima uwe upande wake alivyolaani tabiri hizo baada ya kukimbiwa na kila kimwana katika mwaka mzima uliofuatia! Mimi nadhani waliokuwa wanavumisha uvumi huo ni wale wapiga upatu kwamba mwaka mpya lazima kila mmoja awe nyumbani na familia yake.Hilo ni la muhimu sana ila kama huwezi usije paramia milango ya treni ilimradi tu uwe na familia.
Kwa upande mwingine huwa kunakuwa na wale wakeshaji wanamaombi,wale watakatifu walio hai.Makanisa hupata "makuhani" wa muda. Mapambio,maigizo,ngonjera huwa ndio mwendo wa usiku kucha.Kahawa na kashata huwa ndio msaidizi wa kumfukuza "shetani" asilete usingizi mtu akalala akakosa "neno".Ukiachilia mbali wengi wa makuhani wa usiku mmoja ambao naambiwa wengi wao huwa wameenda kanisani kwa hofu na mashaka juu ya mwaka ujao, wapo wale mabitozi ambao wao huenda pale kutafuta "ngono" Najua utajidai kutoa ulimi kwa mshangao.Huo ndio ukweli ngono huwa zinafanyika kwenye viwanja vya makanisa kwa kisingizio cha "utakaso".Wao watakuwa wanatoa "mahubiri" tofauti.Majeruhi wa "wahubiri" hawa huwa ni wale mabinti wa geti kali. Kanisa moja kule Tabata lilipata mshangao baada ya kukuta maganda kibao ya "ninajali" asubuhi yake. Makasisi walishangaa sana kugundua kwamba "shetani" alifika mpaka kwenye mlango wa nyuma wa kanisani. Kasheshe ilikuja pale kasisi alipoteleza baada ya kukanyaga moja ya "ninajali" hali iliyofanya na zake mbili zianguke kutoka mfukoni mwake. Unajua majina ya watoto ambao mimba zao zilitungwa katika usiku wa mkesha wa mwaka mpya? Yanayotokea usiku ule ni mengi ndugu yangu,siwezi kuyamaliza nikiyaandika hapa.

Ninapopenda mimi ni ile siku yenyewe ya mwaka mpya.Yaani tarehe moja,mwaka mwingine(2006)Kwa walio wengi mwaka mpya humaanisha mambo mapya na kwa wengi vilevile mwaka mpya huashiria matumaini mapya baada ya kuachana na mabalaa,majaribu,mitikasi bubu na kila aina ya laana za mwaka unaokuwa unapewa kisogo(upende usipende).Kwa bahati mbaya mazuri ya mwaka huwa hayakumbukwi sana katika siku hii.
Takribani kila mtu ambaye anakuwa amejaliwa kuuona mwaka mpya bila kuwa kitandani kwa ugonjwa wowote huwa ni mwenye furaha ambayo inatokana na "matumaini" niliyosema hapo juu. Harufu za pilau na maandazi ya tangawizi, kahawa,tambi, kashata na buruba huwa zinaumiza pua za watu kila kona.Ukipita mitaani utaona jinsi ambavyo watoto wanacheza na kujirusha.Huwa hawajali hata magari na wapita njia wa aina yoyote ile.Kwanini wajali bwana?Mwaka mpya umefika,nyumbani mama karekebisha maaakuli ya kueleweka,jioni ana uhakika wa kulala akiwa ameshiba? Usishangae akikuambia kwamba moyoni ana furaha kwa sababu ukiachilia mbali mwaka mpya,ahadi ya wazazi ya kumpeleka kuanza shule ndio inazidi kukaribia.Yeye hajali kama baba kichwa kinakuuma na ahadi yako mwenyewe.
Muziki mkubwa huwa bado unasikika kutoka kwenye ile "baa mpya". Magari(mengi yao madein japani) huwa yamesheheni pale asubuhi na mapema huku wenye nchi wakipata supu ya makongoro,mtori na chapati.Wengi utawaona macho yalivyowaiva,mwenye akili zako unajua kwamba hayo ni matokeo halisi ya mkesha wa mwaka mpya kwenye zile sehemu ambapo sadaka huwa ni "kaka na mimi ninunulie moja basi ya mwaka mpya".Kule ambapo kichwa hufa ganzi kila baada ya dakika kadhaa kutegemeana na kasi yako. Yaani kule ambapo urembo wa mtu huonekana dhahiri zaidi kadiri giza linavyozidi kutanda. Kama hupajui huko shauri yako.

Kwenye hii "baa mpya" ule uchangamfu wa jana usiku huwa umeanza kupotea. Sura ya majukumu huanza kujongea.Mama watoto ni mjamzito,hana kazi yoyote ya kusaidia kipato cha familia,watoto wawili ulionao tayari wanatakiwa kurudi shule mapema mwezi huu. Sare za shule,karo,vibegi nk hujanunua.Ule ushindi uliokuweka "kwa wense" jana usiku taratibu unaanza kugeuka kuwa maumivu. Tayari "mwaka mpya" umeingia.Ulilotimiza katika mwaka uliopita hulioni. Tafakari haina msaada kwa wakati huu.
Tutakiane kheri ndugu zangu.

 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 7:21 PM | Permalink |


Maoni: 3


  • Tarehe: 3:23:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    Kaka Jeff,

    nashukuru kwa heshima. mimi binafsi huwa ninaamini kuwa kufahamu tatizo ni zaidi ya nusu ya suluhisho! watanzania inabidi waamshwe! ona mabenki na NGO zinavyohangaika kutafuta watu wakope lakini watu eti wanaogopa! huu ni miongoni mwa uharibifu mkubwa wa akili za watu uliofanywa na mwalimu! sote lazima tuukiri ili tutafute suluhisho! ona sasa waafrika wenzetu wenye akili zaidi yetu sasa wanafurahia ukuaji uchumi wa Tanzania na wanaimba kale kawimbo kanakomchengua zaidi kaka ben - tuimbe sote "Tanzania tanzania - nakupenda kwa moyo wote!!!- nchi yangu Tanzania- nilalapo nakuota wewe! niamkapo ni kheri mama weeeee!!" wanasema hakuna kama tanzania kwa opportunity! tanzania ni bikra! sikatai wageni na sijawahi kupinga wageni kuwepo- ni muhimu kuchangamsha wenyeji si unajua penye miti hamna wajenzi, lakini hata hivyo mjenzi stadi akihamia atafundisha na wananchi!!, cha msingi ni kuwa maisha yamebadilika! miaka 10 toka sasa ambaye hajanyanyuka ni taabu kutokeza pua juu ya uso wa bahari! tuewasaidiaje wenzetu? - nina andika kimakala kifuupii cha "upande wa pili wa Nyerere - sehemu ya kwanza" vitakuwa vinakuja kadiri ninavyokumbuka matokeo. jamani ninaomba pia na wenzangu tukuze literature ya upande wa pili (usiotakiwa kudumu) wa kiongozi mkuu ili tufike safari yetu!!

    tukirudi kwa makala inaonyesha mabo tofauti, na jinsi ambavyo watu tofauti wamekabiliana na hali tofauti katika mazingira ya matukio - sherehe na imani - ibada, na ubinadamu - ngono!! pamoja na yoootee hayo umemrudia mlengwa wetu mkuu!! yule ambaye kwa mwaka huu hajafanya chochote zaidi ya kumweka muhishimiwa madarakani!!

     
  • Tarehe: 3:18:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Na mimi nataka, ndivyo Barmaid wa Bongo wanapokuja kukupa huduma pale kwa Macheni au Kili Wakati. Hiyo ndiyo token yao kinyume na hivyo mwambie kabisa ununue na usingizi.

    Kuna mambo yanachekesha lakini ikifika wakati wa kuwaza hali y maisha ya wananchi wetu inatia hasira. Nani awakomboe hawa, ndipo niliposema tazama nimekuja ee Bwana kuyafanya mapenzi yako

     
  • Tarehe: 11:25:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mloyi

    Mwaka mpya umewadia! Mwaka wa 2006 sijui utakuwaje? utaanza kwa matumaini, unajua tuna raisi mpya, huko mbele sitaki kuongelea nisije onekana mpinzani, hapana CUF.
    Mwaka tulioombiwa tupo unaisha lakini blogu tulizochagua wenyewe kuwapo haziishi zinazidi kuongezeka na kukomaa.
    Naona siku moja na sisi wanablogu wa Tanzania tutakuwa na siku yetu ya kuadhimisha na kuhamasisha matumizi ya blogu. Inabidi tutunge "uwongo" wa faida zake, hata kama zinatufilisi kulipia cafe na hazitupi akiri anabidi tupigia debe kuwa na nzuri.
    Mwaka mpya na mambo mapya. lakini kwenye blogu ni uimara mpya na habari motomoto.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker