
Katika viongozi ambao wananivutia duniani sidhani kama kuna ambaye ananivutia kuliko Fidel Castro.Huyu ndio yule jamaa ambaye hujaza watu na wakamsikiliza kuanza mashariki mpaka magharibi.Anachokiongelea Fidel Castro hapa ni kama majumuisho ya masuala mengi sana ambayo wanablogu wa kiswahili tunayazungumzia hapa kila siku.Naamini tunaeleweka vilivyo kwa sababu habari za uhakika za kijasusi nilizonazo ni kwamba "tunaogopwa".Tunasema ukweli bila woga,tunatimiza haki zetu za msingi na zilizoandikwa kwenye katiba za nchi zetu.Kama ziliandikwa bila nia ya kutekelezwa basi bahati mbaya.Tafuta muda muafaka,kama unakunywa maji ya baraka basi yatayarishe,msome Fidel Castro hapa kwa makini,kwa vituo.
mzee anaongea kwa kirefu. nimesoma nusu tu. nitaendelea baadaye. jambo zuri alilosema mpaka nilipofikia ni juu ya umuhimu wa kuuliza maswali kuhusu hali yetu. Na lazima tuendelee kuuliza na kujadili kila upande.
Mwandani.