VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Saturday, January 07, 2006
BARAZA LA MAWAZIRI;JE TUTAFIKA?
Ni wazi kwamba uteuzi wa baraza la mawaziri la Raisi Kikwete umepokelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa watanzania. Wapo ambao wameona amefanya uteuzi mzuri kwa maana ya kuteua baadhi ya sura mpya huku wengine wakiona kwamba amerudisha baadhi ya sura zile zile pasipo na rekodi yoyote ya kiutendaji.Wapo ambao wameshikwa na butwaa kuona kwamba "shikamoo" bado zimetamba.Wapo ambao wameona uteuzi wake wa kinamama kushika madaraka ya uwaziri katika wizara nyeti kabisa ni jambo la kujivunia na la msingi.Mimi pia naunga mkono uteuzi wa kinamama,lakini kwangu mimi sio suala la jinsia tu bali suala la uwezo wa kiutendaji.Yapo pia maoni juu ya mzigo ambao Kikwete tayari ameitwisha Tanzania.
Huku wanablogu wengi wakiwa bado vichwa chini wakitafakari,kupitia ule uwanja wangu wa Tanzania Daima kila jumapili,wiki hii (yaani jumapili ya kesho) nimeandika namna hii.Nimeona niweke kabisa waraka huu ili nisije nikasahau.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 2:24 PM | Permalink |


Maoni: 4


 • Tarehe: 3:30:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Ndesanjo Macha

  Nimeingia hapa nikakumbuka kuwa nilikuwa nitazame ukubwa wa sirikali ya Joji Kichaka nikasahau!

   
 • Tarehe: 2:05:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Bwaya

  Hivi ukubwa wa Serikali ndio uchapakazi? Hii serikali imekuwa kubwa mno. Wasi wasi wangu ni gharama za kulihudumia> Nchi imewekwa rehani, nadhani.

   
 • Tarehe: 7:23:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mark msaki

  nakubaliana na wewe kaka msangi kwa kuchokoza akili za wenzetu kule home katika hili. nia siku zote ni ujumbe ufike hivyo ni heko. sijui kama gazeti, mtanzania daima inauza kopi ngapi kwa siku/wiki? je kati ya hizop ngapi dar na ngapi nje ya dar?

  nakubaliana na uteuzi wa kina mama. ni waelewa na wasiopenda kukaa na mabomu. pia wana utu. kitonda cha hisia kuwa mgombea uraisi wa ajaye kuwa mama ni chema kwani hawa wenzetu hawana mgango wa kurig ili waongoze.

  baraza la sasa japo lina gharama lakini ninaona kama muheshimiwa ametaka wabunge nao wamlipe fadhila kwani pia aliwapigia kampeni ya bidii katika ile slogan ya mafiga matatu. sasa anataka kila mtu amsaidie kwenye section husika ya ilani yake. nadhani kama uzalendo utashika nafasi yake inaweza ikawork out. vitu vingine mfano mapuri kupiga wananchi kupitia magereza polisi wangeamuaje? - labda ndo maana kawatenga. unajua kutokuwa na vitambulisho vya uraia vimewanyima watz nafasi na resources zao nyingi? labda tumpe nafasi kama nia yake ni nzuri, mazuri yaweza kupita gharama.

   
 • Tarehe: 2:57:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Boniphace Makene

  Jeff hicho kiunganishi cha Tanzania Daima kiko kwenye Construction hadi lini? Wengine tulishatanga za ukombozi wa kupata walau taarifa mpya tumechoka kusoma Uhuru na magezeti ya Mengi. Mtaarifu Mbowe mheshimiwa, mwambie asikie kilio chetu na kutuwekea kiunganishi hicho haraka kama alivyofanya kwa kuweka kiunganishi kwa bendera ya Uingereza kwenye ile tovuti ya chadema. (kauli hiyo ya mwisho ni ucheshi tu)

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker