Tarehe: 7:09:00 AM, Mtoa Maoni:- FOSEWERD Initiatives
Tarehe: 1:26:00 PM, Mtoa Maoni:- Ndesanjo Macha
Dhana kuwa Afrika ni masikini inafanya kazi moja kubwa sana: kuendeleza sekta ya misaada ya fedha/utaalamu na kuyapa mashirika ya "misaada" kazi na kuwalipa wenye mashirika hayo mishahara na marupurupu. Sababu kubwa ya kuita blogu yangu Jikomboe ni kutokana na imani ya dhati niliyonayo kuwa sisi Waafrika wenyewe tuna suluhisho na dawa ya matatizo yetu. Lakini suluhisho hilo litapatikana pale tutakapoamua kusema kuwa "tunaweza." Tukiamini kuwa sisi masikini tukakubali kuongozwa na serikali zinazozunguka na mabakuli Ulaya na Marekani kuomba na wasomi wetu nao na mabakuli wakiomba fedha kwa ajili ya mashirika yao yasiyo ya kiserikali, tutayasikia maendeleo kwenye bomba. Sisi na vizazi elfu kadhaa vijavyo.
sawa hasa kaka jeff. ninachokufurahia wewe ni balozi mzuri wa mawazo yaliyochekechwa na bunga bongo kwa wadau. umefanya vyema kabisa. sasa ukiwa unajadili nao hili ambalo walikuwa hawalijui, pia uwakumbushe kile kilio cha kila mara cha mkapa kuwa kwa sasa hatupendi sana kupokea misaada lakini tunalilia fursa sawa ya biashara - au level ground. nilisoma juzi european market imefinya mgao wa kuchukua bidhaa toka afrika na hapo hapo inaongeza misaada! - kwa ujumla ni mfumo, nina uhakika unajua mengi sana katika uwanja huu! kila kheri!