VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Wednesday, January 25, 2006
HII SIO RUSHWA?
Kwa mshtuko na mshangao nimesoma habari hii hapa kwenye tovuti ya IPP.Yaliyonishtusha ni kwamba Kamanda Msikka alitoa hizo fedha kama mtego au ni kweli aliamini kwamba angepata cheo kikuu cha polisi? Makosa ya jinai huwa yanaangaliwa kwa upande wa kitendo chenyewe na upande wa fikra halali.Swali gumu linalojijenga kichwani kwangu ni je kama Kamanda Msikka alitoa fedha hizo akiamini kabisa kwamba ataukwaa u-IGP hajatenda kosa baya kabisa la jinai la rushwa? Kimsingi kama kamanda Msikka alifikia hata hatua ya mbali kabisa ya kuwa na majadiliano ya kuwezeshwa kuwa IGP kwa kutumia mlungula basi ni wazi kabisa ile sifa ya uadilifu imemtoka.Cha msingi ni yeye pia kuwajibishwa kikamilifu na sio kufungua mashtaka ya utapeli kwa mfanyabiashara peke yake.Nabakia na imani kwamba mwandishi wa habari ile hakuwa makini katika alichokuwa akikiandika.La sivyo,sheria ichukue mkondo wake mzima na sio nusu mkondo.Kama kuna mtu mwenye undani zaidi wa habari hii naomba anifahamishe.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 11:07 PM | Permalink |


Maoni: 10


  • Tarehe: 5:21:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    kaka Jeff, suala zima hata mie naliona limegubikwa na kiza kinene...kimsingi nilipoisoma habari hii kwa mara ya kwanza, ilimtia hatiani kamanda Msiska moja kwa moja...baadae sasa nikaona inageuzwa kuwa ulikuwa ni mtego...kwanini basi walisema ametapeliwa na sasa wanazungumza ilikuwa mtego? kwani hiyo hela ilikuwa ni ya polisi? maana kufanya kazi kufuata utaratibu ndio dawa pekee ya kumlinda raia mwema dhidi ya dosari katika utendaji wa kazi. kama hela hiyo ilikuwa ya polisi, basi hana hatyia kinyume cha hapo...polisi kuna haja ya kuisafisha..tena kutokea juu!! juu kabisa!

     
  • Tarehe: 11:09:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Jeff kwa nini tusianzishe mjadala huu kwenye blogu zote na kisha kwenye vibaraza vytu vya kila Jumapili huko nyumbani ili kila wanaposoma waone uchafu huu. Nadhani watatambua namna tunavyotazama mbinu hizi za kidhalimu. Niliwahi kuandika hili kidogo nadhani sasa napaswa kuongeza pia.

     
  • Tarehe: 11:21:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger John Mwaipopo

    Jamani hata mimi ubongo wangu uliparaganyika baada ya kusoma habari hii. Inavyoonyesha Kamanda Msikka anataka kuepushwa na zahama hii ilhali inaonyesha naye ni mshiriki tu. Iweje atoe pesa ili apendelewe u-IGP wa kasi mpya nk. Inavyoonyesa ni pesa za kawaida sio zile za moto, ama darhotwire watueleze vinginevyo.

    Kumbe naanza kuwa na mawazo kuwa kuna uozo ndani ya jeshi la polisi bongo. Kuna haja liangaliwe na lisafishwe upya kuanzia juu kabisa kwa Mahita mwenyewe.

     
  • Tarehe: 11:57:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Makene,
    Nadhani kuna umuhimu wa kuufanya huu uozo uwe mjadala wa nguvu kabisa.Vita dhidi ya rushwa inahusu watu wote,viongozi na wananchi.Nakuahidi kuweka bayana kwenye kibaraza changu wiki hii.

     
  • Tarehe: 12:38:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Ndesanjo Macha

    Hata mimi nilishtuka sana kusikia kuwa eti huyu mkuu wa polisi anatetewa na wakuu wake kuwa yeye hana kosa. Habari tunazopata ni kuwa alidanganywa. Hii inamaanisha kuwa aliamini kuwa kutoa kwake fedha kungempatia cheo cha juu. Baadaye ndio akagundua kuwa amedanganywa ila kabla ya kugundua nia yake ilikuwa ni kupewa cheo kwa kutumia kujuana na sio uwezo wake wa kazi na taratibu husika. Huu ni uozo na uchafu mkubwa kabisa. Mtu mwenye mamlaka kama yeye kutaka kuombewa eti apewe cheo cha juu na kutumia hela kufanikisha azma hiyo. Hivi ndio vipimo, ndugu zangu, vya aina ya serikali iliyochukua madaraka hivi majuzi. Tunatumia vipimo hivi kutazama kama kauli zao zinaendana na vitendo. Asante Jeff kwa kulileta hili kwenye blogu.

     
  • Tarehe: 11:22:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    jeff washa moto kibarazani homuu!!!

     
  • Tarehe: 1:02:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Jeff nina blogu tatu kwa mpigo zimefunguliwa zipo hapo kwangu pita ukawasabahi.

     
  • Tarehe: 12:49:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Ni rushwa. Rushwa. Rushwa.

     
  • Tarehe: 4:18:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Reggy's

    "Hiyo kitu ni rushwa' ndivyo nilivyoona kwa mara ya kwanza. Baadaye, kwa busara zangu na vyanzo vingine, ikaonyesha uwezekano wa kuwa Msika, ni mtu makini anayehisiwa kuwa anaweza kuwa IGP baada ya Mahita. Hivyo unachezwa mchezo mchafu ndani ya jeshi hilo, ili kumharibia kwa maslahi ya wengine. Mnaonaje. washa moto

     
  • Tarehe: 4:08:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Indya Nkya

    Reginald kweli umewasha moto. Inawezekana anachezewa? Tatizo ni lile lile; mambo kama haya atakayeumia ni jamaa hata kama huyo kamanda alikuwa na mpango wa kutoa rushwa. Lakini jamaa aliyepokea naye si anaweza kumtega kwa sababu kupokea na kutoa kote ni makosa, akasema kwamba alitaka kuhakikisha kama jamaa ni mtoa rushwa kwa sababu amekuwa akisikia hivyo? Halafu kesi ikaanza kwenye sifuri!!

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker