YESTERDAY HAS GONE FOREVER!TOMMOROW WILL NEVER ARRIVE,BUT TODAY IS YESTERDAY'S TOMMOROW WITHIN YOUR REACH.WHAT ARE YOU DOING WITH IT?
Wednesday, January 25, 2006
HII SIO RUSHWA?
Kwa mshtuko na mshangao nimesoma habari hii hapa kwenye tovuti ya IPP.Yaliyonishtusha ni kwamba Kamanda Msikka alitoa hizo fedha kama mtego au ni kweli aliamini kwamba angepata cheo kikuu cha polisi? Makosa ya jinai huwa yanaangaliwa kwa upande wa kitendo chenyewe na upande wa fikra halali.Swali gumu linalojijenga kichwani kwangu ni je kama Kamanda Msikka alitoa fedha hizo akiamini kabisa kwamba ataukwaa u-IGP hajatenda kosa baya kabisa la jinai la rushwa? Kimsingi kama kamanda Msikka alifikia hata hatua ya mbali kabisa ya kuwa na majadiliano ya kuwezeshwa kuwa IGP kwa kutumia mlungula basi ni wazi kabisa ile sifa ya uadilifu imemtoka.Cha msingi ni yeye pia kuwajibishwa kikamilifu na sio kufungua mashtaka ya utapeli kwa mfanyabiashara peke yake.Nabakia na imani kwamba mwandishi wa habari ile hakuwa makini katika alichokuwa akikiandika.La sivyo,sheria ichukue mkondo wake mzima na sio nusu mkondo.Kama kuna mtu mwenye undani zaidi wa habari hii naomba anifahamishe.
kaka Jeff, suala zima hata mie naliona limegubikwa na kiza kinene...kimsingi nilipoisoma habari hii kwa mara ya kwanza, ilimtia hatiani kamanda Msiska moja kwa moja...baadae sasa nikaona inageuzwa kuwa ulikuwa ni mtego...kwanini basi walisema ametapeliwa na sasa wanazungumza ilikuwa mtego? kwani hiyo hela ilikuwa ni ya polisi? maana kufanya kazi kufuata utaratibu ndio dawa pekee ya kumlinda raia mwema dhidi ya dosari katika utendaji wa kazi. kama hela hiyo ilikuwa ya polisi, basi hana hatyia kinyume cha hapo...polisi kuna haja ya kuisafisha..tena kutokea juu!! juu kabisa!
ReplyDeleteJeff kwa nini tusianzishe mjadala huu kwenye blogu zote na kisha kwenye vibaraza vytu vya kila Jumapili huko nyumbani ili kila wanaposoma waone uchafu huu. Nadhani watatambua namna tunavyotazama mbinu hizi za kidhalimu. Niliwahi kuandika hili kidogo nadhani sasa napaswa kuongeza pia.
ReplyDeleteJamani hata mimi ubongo wangu uliparaganyika baada ya kusoma habari hii. Inavyoonyesha Kamanda Msikka anataka kuepushwa na zahama hii ilhali inaonyesha naye ni mshiriki tu. Iweje atoe pesa ili apendelewe u-IGP wa kasi mpya nk. Inavyoonyesa ni pesa za kawaida sio zile za moto, ama darhotwire watueleze vinginevyo.
ReplyDeleteKumbe naanza kuwa na mawazo kuwa kuna uozo ndani ya jeshi la polisi bongo. Kuna haja liangaliwe na lisafishwe upya kuanzia juu kabisa kwa Mahita mwenyewe.
Makene,
ReplyDeleteNadhani kuna umuhimu wa kuufanya huu uozo uwe mjadala wa nguvu kabisa.Vita dhidi ya rushwa inahusu watu wote,viongozi na wananchi.Nakuahidi kuweka bayana kwenye kibaraza changu wiki hii.
Hata mimi nilishtuka sana kusikia kuwa eti huyu mkuu wa polisi anatetewa na wakuu wake kuwa yeye hana kosa. Habari tunazopata ni kuwa alidanganywa. Hii inamaanisha kuwa aliamini kuwa kutoa kwake fedha kungempatia cheo cha juu. Baadaye ndio akagundua kuwa amedanganywa ila kabla ya kugundua nia yake ilikuwa ni kupewa cheo kwa kutumia kujuana na sio uwezo wake wa kazi na taratibu husika. Huu ni uozo na uchafu mkubwa kabisa. Mtu mwenye mamlaka kama yeye kutaka kuombewa eti apewe cheo cha juu na kutumia hela kufanikisha azma hiyo. Hivi ndio vipimo, ndugu zangu, vya aina ya serikali iliyochukua madaraka hivi majuzi. Tunatumia vipimo hivi kutazama kama kauli zao zinaendana na vitendo. Asante Jeff kwa kulileta hili kwenye blogu.
ReplyDeletejeff washa moto kibarazani homuu!!!
ReplyDeleteJeff nina blogu tatu kwa mpigo zimefunguliwa zipo hapo kwangu pita ukawasabahi.
ReplyDeleteNi rushwa. Rushwa. Rushwa.
ReplyDelete"Hiyo kitu ni rushwa' ndivyo nilivyoona kwa mara ya kwanza. Baadaye, kwa busara zangu na vyanzo vingine, ikaonyesha uwezekano wa kuwa Msika, ni mtu makini anayehisiwa kuwa anaweza kuwa IGP baada ya Mahita. Hivyo unachezwa mchezo mchafu ndani ya jeshi hilo, ili kumharibia kwa maslahi ya wengine. Mnaonaje. washa moto
ReplyDeleteReginald kweli umewasha moto. Inawezekana anachezewa? Tatizo ni lile lile; mambo kama haya atakayeumia ni jamaa hata kama huyo kamanda alikuwa na mpango wa kutoa rushwa. Lakini jamaa aliyepokea naye si anaweza kumtega kwa sababu kupokea na kutoa kote ni makosa, akasema kwamba alitaka kuhakikisha kama jamaa ni mtoa rushwa kwa sababu amekuwa akisikia hivyo? Halafu kesi ikaanza kwenye sifuri!!
ReplyDelete