VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Thursday, January 05, 2006
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM HII HAPA!
Tupende,tusipende CCM ndio chama tawala hivi sasa nchini Tanzania.Kwa maneno mengine ndicho chama chenye madaraka ya kuipeleka nchi yetu pwani au katikati ya bahari ambapo wasiojua kuogelea ni dhahiri watakufa maji.Baada ya jana kuweka "hotuba mahiri" aliyoitoa Raisi Kikwete wakati akilihutubia Bunge la Tanzania kwa mara ya kwanza akiwa kama raisi,nimeona ni vyema niweke pia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi au kwa maneno mengine muongozo wa 2005-2010.
Mtakumbuka kwamba kilio changu kimekuwa ni UWAJIBIKAJI wa viongozi wetu. Kama viongozi waliopo madarakani hivi sasa wamechaguliwa kidemokrasia au kwa kutumia rushwa(takrima) sio suala la msingi sana hivi sasa.Yaliyopita si ndwele,tugange yajayo.Sasa ili wananchi waweze kuwa na nguvu ya kuhoji ni lazima wajue kwanza ahadi zilizotolewa.Ni dhahiri kwamba mwananchi akilijua hilo(asilimia kubwa sana ya wananchi hawana habari na ilani hii) basi ataweza kushiriki ipasavyo katika kusukuma mbele gurudumu la nchi kijamii,kiuchumi na pia kisiasa.Wanablogu tunalo jukumu kubwa sana la kuelimisha umma ambao nadhani kimakusudi huwa unawekewa pazia ili usijue nini kinatokea upande wa pili.Badala yake nchi inakuwa inaendeshwa kwa "viini macho".Jambo fulani linatokea,hakuna anayewajibishwa na nguvu ya wananchi kuhoji haipo kwa sababu hawana "nguvu ya habari" Matokeo yake ni kurukana," hapana bwana,ilani yetu ya uchaguzi haisemi hivyo,inasema hivi na hivi".Bila ushahidi kesi inakuwa ngumu sana hata ukilia machozi ya damu. Basi tuisome kwa makini hii ilani,tuwakumbushe na wenzetu waisome,tuwasomee babu na bibi zetu.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 1:24 PM | Permalink |


Maoni: 3


  • Tarehe: 1:39:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    yeap kaka msangi na bila kusahau kupiga fimbo makaburi ya wazee!

    huyo ni kikwete, namnukuu alipokuwa anataja mawaziri

    "Nilipokuwa Nachingwea kulikuwa na mtu mmoja ambaye kila asubuhi alikwenda na fimbo kwenye kaburi la baba yake na kuanza kulipiga huku akimlaumu kwa nini hakumsomesha, na ndiyo maana anapata taabu zote alizonazo," alisema.

    Rais Kikwete alisema ni muhimu kutoiharibu nchi ili wajukuu watakaokuja baadaye wasipate nafasi ya kupiga makaburi 'yetu' kutokana na shida watazozipata zitazokuwa zimesababishwa na 'sisi tuliowatangulia'.

    cheers

     
  • Tarehe: 1:43:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    WADHIFA wa uwaziri au unaibu waziri hauhitaji kwenda kusomea katika shule yoyote, na kama ingekuwa hivyo kila mtu angekwenda kusomea uwaziri. Kauli hiyo ilitolewa na Rais Jakaya Kikwete, alipokuwa akitangaza Baraza lake la Mawaziri Ikulu jana, mbele ya waandishi wa habari.

    Rais Kikwete alitoa mfano wake mwenyewe, kwamba alipoitwa na Rais wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi na kupewa ubunge wa kuteuliwa na baadaye kupewa unaibu waziri wa Maji na Nishati. Alisema baada ya kupewa wadhifa huo alimueleza Rais Mwinyi kuwa asingeweza kazi hiyo, lakini Rais Mwinyi alimwabia utaweza kwa kuwa najua uwezo wako wa kufanya kazi.

    Ni vyema pia hata wao walioteuliwa wajue kuwa si kweli kuwa bila wao nchi haina uwezo wa kuendeshwa na pia wakiri kuwa kwa kuwa hawakuusomea uongozi shule basi wasiugeuze uwaziri ajira ya kudomu!

    cheers

     
  • Tarehe: 1:44:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    habari hizi naziibua www.uchaguzitanzania.com ukifika pale juu kabisa click habari za kitaifa.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker