VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Monday, January 09, 2006
Kizuri kula na nduguyo!
Huo msemo kwenye kichwa cha habari nimeusikia toka enzi zile nikiwa pale kijijini kwetu Ndaga.Enzi zile nikiteleza na kuchubuka magoti kwenye changarawe nikiwa njiani kuelekea shuleni.Enzi zile za kujifunza kuandika na kuhesabu.Enzi zile za kuandika chini,nje ya darasa,kwenye mavumbi.Enzi zile za mikufu ya vijiti vya kuhesabia au vifuniko vya soda vyenye tobo katikati vikiunganishwa vyema kwenye uzi.Enzi zile za kuvaa bugaloo siku ya jumapili na kwenda kanisani tuking'aa nyuso kwa mafuta ya mgando!
Enewei hizo ni enzi zile,zimepita lakini hupenda sana kuzikumbuka.Nilichotaka kusema hapa ni kwamba nina uhakika wengi wetu ni wapenzi wa muziki.Na kwa wale wenzangu na mie waliopo "ughaibuni" kuna zile nyakati ambazo unakosa kabisa kupata ladha za muziki kutoka nyumbani Tanzania au barani Afrika.Mimi kwa bahati nzuri kila siku iendayo kwa mungu huwa naburudika na muziki kutoka nyumbani,barani Afrika na dunia nzima.Hili ni jambo zuri au ndio hicho kizuri ninachokisema hapo juu.Sasa kama na wewe unataka kuburudika basi bonyeza hapa. Ukishafanya hivyo kwenye hizo "genre" tafuta African,hapo utakumbana na redio kibao,zinatwanga muziki kutwa nzima.Na kama unapenda "bongo fleva" basi jamaa wa motovibes wapo kwa ajili yako.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 6:37 PM | Permalink |


Maoni: 6


 • Tarehe: 8:41:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mark msaki

  jeff, aksante sana. sasa hivi nakula rhumba "juju" music toka kule yoruba land. muziki wao ni tajiri sana.

  cheers

   
 • Tarehe: 9:34:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Pata burudani Mark,maisha haya lazima yaendane na burudani la sivyo wote tutaishia Mirembe!

   
 • Tarehe: 8:50:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Ndesanjo Macha

  Uliponimaliza ni hapo ulipotaja mafuta ya mgando. Unakumbuka ashanti? Au ulikuwa hujazaliwa enzi zake?
  HAya ngoja niende huko kwenye muziki. Asante.

   
 • Tarehe: 6:58:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Ndesanjo,enzi za ashanti nilikuwa tayari ninadunda mitaani nikipigana ngumi za "kuputa".

   
 • Tarehe: 6:30:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Bwaya

  Nikufagilie kidogo bwana kwa makala ya Jumapili kwenye Tanzania Daima. Sikuwa mnunuzi wa magazeti hayo ila sasa naona utanifanya nikufuatilie kwa huko. Kazi nzuri sana Jeff, lakini kumbuka bado utamaduni wa kusoma hapa nyumbani uko chini sana. Hilo halikatishi tamaa, ni changamoto kwa waandishi na wanataaluma kama wewe, ambao wana moyo wa uzalendo kwa watu wao.

  Niko kunako muziki haswaa, napata ile kitu roho "inapenda". Siku njema "mzee".

   
 • Tarehe: 5:17:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Mary Francis

  Jeff umenikumbusha mbali sana ulipozungumzia mafuta ya mgando na challenge ya ashati imenifuraisha sana anyway maisha yanaenda yakibadilika ndio maana kizazi cha sasa wanatumia lotion sio mafuta mgando tena. Well done site ya music ni nzuri inasaidia walio mbali na nyumbani kupata muziki wa nyumbani

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker