Monday, January 02, 2006

KUMBE HATA MAREKANI WANAOGOPA BLOGU!

Kheri ya mwaka mpya!Ni lazima tutakiane kheri jamani.Mwaka mpya ndio umeanza rasmi na tayari umeshaanza kuyoyoma,leo tayari ni tarehe mbili mwezi wa kwanza 2006!Nina imani kwamba mwaka huu changamoto ya uwanja huu wa blogu itakuwa pevu zaidi katika kuelekea kwenye mabadiliko tunayoyataka kwenye jamii zetu.
Uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza bado ni jambo ambalo dunia nzima inalilia.Bado wanahabari tunazongwazongwa.Blogu ndio tishio zaidi kwa hivi sasa.Hata Marekani imeanza kupata hofu ya aina yake kuhusiana na blogu.Visingizio kibao vimeanza kutolewa,soma hapa ujionee.
Labda cha msingi ni kutambua kwamba blogu zina nguvu na nguvu ni kitu ambacho tunakihitaji sana ili kuweka sawa merikebu zetu.Kheri ya mwaka mpya tena!

2 comments:

  1. Jeff nimeona hiyo moto kama kazi, nimefika Ottawa sasa nadhani mwaka umeanza na kazi ya kuzitanua za Bongo inapaswa kuwa kali bila kuchoka,

    ReplyDelete
  2. jeff,

    heri ya mwaka mpya kwako pia. nguvu ya blogu teyari kubwa tu na kama nilivyosema mahali kwamba ninahisi hata muhishimiwa raisi wetu ni mwanablogu japo tu hajafungua yake. si umesikia anatuanzishia kale kawizara tulikuwa tunakalilia ka kushughulikia uraia?

    ni blogu tu kwa ari mpya nguvu mpya na kasi mpya! - ndio njia pekee ya kumsaidia kupeleka merikebu vyema ukiacha yale magazeti ya wahariri nyumbani yanayosifia tu bila kueleza kasoro zilipo!

    cheers

    ReplyDelete