VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Wednesday, January 11, 2006
Mwapachu anamaanisha adhabu ya kifo?

Mawaziri wa Kikwete wameshaanza kazi (angalau kwa maneno hivi sasa) yaani kama ni harusi basi bado tupo kwenye "harusi ya makofi"(sijui kama tunaelewana hapa).Nasema wameanza kazi kwa maneno kwani nina uhakika wengi wao hivi sasa wapo kwenye kile kipindi cha kusoma na kukagua makabrasha za wizara zao.Kwa wizara mpya kama ya Usalama wa Raia sina uhakika wamefikia wapi mpaka hivi sasa.Pia sina uhakika kama wananchi wameshaweza kutambua wapi pa kupeleka baadhi ya matatizo yao ya "kiusalama".Je ni wizara ya mambo ya ndani au wizara ya usalama wa raia.Nadhani serikali ina jukumu la kuanza kwa kutoa elimu ya muundo wa serikali ili mwananchi asije akapeleka suala lake wizara fulani kisha akazungushwa kwa miezi kadhaa kabla hajaja karani wa wizara na kumuambia "unajua nini?,masuala haya yanashughulikiwa wizara fulani na sio hii.Sina uhakika hata kama wafanyakazi wa serikalini wenyewe wanajua jinsi ya kutofautisha masuala haya.
Sasa katiba habari moja hivi leo Waziri wa usalama wa raia bwana Bakari Mwapachu(pichani juu) amezungumzia suala la kutokuwa na "msalie mtume" kwa majambazi.Sina uhakika,waziri ana maana gani na kauli kama hii.Kama anamaanisha adhabu ya kifo basi nadhani kuna haja ya kufufua mjadala kuhusu adhabu ya kifo.Pengine huu ni mjadala tayari hata hapa miongoni mwa wanablogu wenzangu.Hivi adhabu ya kifo ni suluhisho la uharamia na ujambazi? Hivi nani anastahili adhabu ya kifo zaidi kati ya jambazi au waziri anayekula rushwa kisha kupelekea kutojengwa kwa hospitali au shule?Watu wangapi anakuwa ameua huyu?
Mengi ya majimbo ya Marekani yanatekeleza adhabu ya kifo.Jibu mnalo wengi juu ya swali,ujambazi umepungua?Canada haina adhabu ya kifo.Je uhalifu kati ya Canada na Marekani ukoje?
Siungi mkono uhalifu wa aina yoyote.Hebu tuliongeleeni hili wanablogu wenzangu.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 8:07 PM | Permalink |


Maoni: 3


  • Tarehe: 5:12:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

    suala la uhalifu na adhabu... Umangani kila wiki wanakusanywa wahalifu na kukatwa viganja, wengine mijeledi, mbona wahalifu bado wapo tu? Na wengine hukatwa vichwa.
    Mimi binafsi sidhani kama adhabu ya kifo ni sahihi. Nadhani serikali iwadhibiti majambazi na kupunguza bunduki mikononi mwa majambazi kwanza.Iwasake kama walivyosakwa akina Nyau wakati uleee pale Dar... mambo yatulie kidogo.

     
  • Tarehe: 6:32:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    ndugu jeff, sidhani kama bwana waziri alimaanisha hivyo. nadhani alikuwa na maana kuwa jambazi anayeshambulia kwa nguvu zote apambane na nguvu zote kutoka polisi? yaani kwenye eneo la tukio?

     
  • Tarehe: 6:42:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Christian Bwaya

    Na mimi niliposikia habari hiyo nilijaribu kufikiri maana ya maneno hayo.
    Ni dhahiri anahalalisha adhabu ya kifo kwa majambazi. Jambo hili haliwezi kuwa sahihi.
    Kwake (nafikiri) anadhani hatua hiyo itapunguza matukio ya ujambazi kitu ambacho si kweli.
    Huwezi kutetea uhai kwa kutoa uhai wa mtu mwingine. Isitoshe hata ikijulikana kwamba watauawa, majambazi hawaogopi, asidhani anawatishia! Sana sana anadhani atawatia hamasa kutafuta mbinu bora zaidi za kupambana na polisi! Huko si kutatua tatizo, ni kuzima moto kwa petroli.(Sijui anategemea nini huyu bwana!)
    Nadhani anaturudisha nyuma sana wakati dunia yote inatafuta kufuta adhabu ya kifo!
    Atafute mbinu nyingine.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker