VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Thursday, January 12, 2006
NAJIVUNIA UAFRIKA WANGU,WEWE JE?
Kama wewe ni mtafiti wa mambo kuna uwezekano mkubwa sana kwamba umeshawahi kuketi kitako na kujiuliza maswali kadha wa kadha kumhusu mtu mweusi,mwafrika.Binafsi fikra za namna hii hunijia kila mara.Fikra hizi huwa ngumu nikichanganya masuala ya dini,ukoloni,mwanzo wa ulimwengu,biashara ya utumwa,ubaguzi wa rangi,jamii nk.Nimewahi hata kujiuliza hivi dunia ingekuwaje au ingewezekana bila kuwepo kwa watu weusi?Huwa siishii hapo,huwa pia najiuliza imekuwaje dunia nzima imetapakaa watu weusi? Ningali nabukua,na nazidi kubukua historia ya mtu mweusi.Naepuka historia iliyoandikwa na mtu mweupe,akiwa kilimani Yale University au Oxford na kwingineko akidai anaijua Afrika.Katika pembua zangu nimekutana na huyu bwana.Amenisisimua na kuendelea kunipa ghani za kufurahia na kutukuza uafrika wangu.Nahisi wanangu watu wenye bahati kwa sababu kimsingi nitawafunza (tena wangali wabichi) juu ya ukweli mpya,yale niyajuayo na kuyaamini ipasavyo sio tu kwa sababu nataka kuyaamini bali kwa sababu yana ushahidi uliokamilika.Soma zaidi hapa.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 1:43 PM | Permalink |


Maoni: 2


  • Tarehe: 3:32:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mloyi

    Dunia bila Afrika sijui ingekuwaje?, Wengine wanasema malalamiko yasingekuwepo, sijui kama vichwa vyao vinafanya kazi.
    Dunia bila Afrika Hata wao wasingeijua marekani, pengine wangekuwa wanalala nje mpaka leo, njaa ingekuwa ni ndugu yao wa karibu na Mungu asingekuwa mmoja kwao, kila kitu kingekuwa mungu.
    Dunia bila Afrika, Bahari ingemeza dunia yote iliyobaki, pengine wangerejea kuwa manyani walikotokea au hata mungu angeacha kuwaumba na wao.
    Dunia bila afrika Ingekuwepo nayo pia.

     
  • Tarehe: 1:36:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Ndesanjo Macha

    Runoko Rashid amaefanya utafiti sana juu ya waafrika waliosahauliwa katika nchi kama India, China, au bara la Amerika ya Kusini. Pia kuna bwana anaitwa Ivan van Sertima ambaye ameandika "they came before columbus", "Black presence in early Europe," n.k. Halafu kuna mzee wao Dakta Yosef Ben Yoachanan ambaye kaseti za hotuba zake ziliniwehusha kabisa nilipozisikiliza mara ya kwanza. Mloyi anazipatapata hotuba zake. Dakta Ben kazeeka na mgonjwa kidogo. Nilimwona akiongea mwezi wa kumi mwaka huu, hakuwa na nguvu kama zamani. Yeye ametafiti na kuandika juu ya uafrika katika dini za kiislamu, kikristo, na kiyahudi. Anasema, kwa ushahidi, kuwa bila Uafrika dini hizi leo hii zisingekuwepo.

    Kuhusu Runoko Rashid, nadhani Mwandani anamfuatilia kwa karibu. Kama sijakosea. Eti, Nambiza...

    Kwa kifupi, watu hawa ni kati ya walimu wangu. Nimekuwa nikisema mara kwa mara kuwa wakati mwingine inakupaswa eti utoke nje ya Afrika ndio ujifunze juu ya Afrika. Au ukutane na watu ambao walizaliwa nje ya Afrika ndio wakufunze juu ya Afrika. Unajua historia tunayofundishwa shule asilimia kubwa ni uongo na silaha ya kupumbaza utambuzi wa uafrika wetu.

    Unapokutana na kazi za watu hawa unajifunza jambo moja muhimu sana: hoji maisha yako na mambo yote ambayo umekuwa ukichukulia kuwa ni ukweli.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker