VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Saturday, January 21, 2006
ONYESHO LA UMOJA!
Juzi jioni nilikwenda kutizama onyesho la kundi moja linaloitwa UMOJA(The spirit of togetherness).Hili kundi linatokea Afrika ya Kusini na hivi sasa linatamba kwa maonyesho kabambe duniani kote.Onyesho hili nililiangalizia hapa.
Tafadhali,popote pale ulipo ukisikia hawa jamaa wamekuja jijini au mjini kwako fanya hima uende ukawaone.Historia ya kundi hili ni jambo la kuvutia sana.Hivi Tanzania hivi sasa tuna makundi mangapi kama hili la UMOJA?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 12:49 PM | Permalink |


Maoni: 4


  • Tarehe: 3:29:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Christian Bwaya

    Msangi,
    Nilisoma kazi yako katika Tanzania Daima. Nilivutiwa na mada uliyokuwa nayo mezani, kwamba watanzania wanapaswa kuanza kujiona ni matajiri.
    Hili naliunga mkono kwa dhati kabisa kwa sababu, nchi kama Tanzania haifanyiwi haki kuitwa eti ni "ulimwengu wa tatu", wakati kila aina ya raslimali tunazo.
    Tatizo la nchi yetu (mimi naweza kusema kuwa) ni la kiungozi. watawala wetu hawawajibiki ipasavyo. Hapa nina maana ya kuanzia kwenye ngazi ya chini kabisa, yaani mtaa. ni kwa sababu hii unakuta wananchi wanashindwa kuzitumia mali-asili zao kama inavyotakiwa.
    Vilevile, unakuta ni kwa sababu hii tunakuwa na baa la rushwa kubwa kubwa zinazokinzana kabisa na juhudi za kujiletea maendeleo.
    Ni kama ulivyosema kuwa tukifika mahala kila Mtanzania akaachana na propaganda kuwa yeye ni maskini, akaamka akijua kuwa yu tajiri, basi hapo tutakuwa katika nafasi nzuri ya kujiletea uhuru wa fikra ambao hatimaye utatuelekeza katika mafanikio endelevu.
    Tunahitaji mageuzi ya fikra (kama asemavyo mara zote Ndesanjo Macha). Tunahitaji mapinduzi ya kufikiri kwetu. Tunahitaji kugeuza mwelekeo wa muono wetu. Maendeleo yatakuwa ni haki yetu.
    watu kama wewe, Msangi, mlibahatika kuwa katika tamaduni za nchi za watu, mwatakiwa kutiwa moyo zaidi katika kutimiza wajibu wenu ambao kimsingi ni kuhamasisha wananchi kubadilika. Mimi niwe mmoja wa hao. Hongera sana!

     
  • Tarehe: 8:07:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    bwana bwaya amesema ukweli kabisa kuhusiana na mada ya umasikini wa watanzania. kwa kweli kwa miaka mingi tanzania ilikata kuwa nchi huru na kuwa na vichhwa ambavyo vinaweka mbele kulaumu wengine bila kushughulikia tatizo upande wetu...ebu ona kwa mfano, tunawajua maafisa ardhi wanaouza viwanja mara mbili mbili...na umekuwa ni mtindo wa utendaji serekali na wote tukaukubali..walioelewa kuwa wakati ukuta wakaishia na kushughulikia maslahi ya familia zao tu....ona kwa mfano ndani ya siku hizi kadhaa mambo anayofanya JK....kwani ni kipi kipya?? ilifika wakati unataka kuchangia ambulance wanakataa sababu ya kwamba wewe si CCM. angalia hata leo hii ukienda pale kiraracha KNCU kuna mapipa kibao ya lami mrema alitaka aweke wakamzuia ni vijimambo kama hivyo vinatakiwa viondolewe na sie tushiriki kujenga...kwani kwa mfano kikwete alivyoonesha nia ya kuwa na hospitali kila kata, hahitaji peke yake kuingiza mikono mfukoni...mbona mimi hapa nilipo sitaona uchungu na nina uwezo wa kutoa laki 5 kwa mara moja kuchangia hospitali katani mwangu bila kufukiria mara 2? je ni wangapi tuna vidola vichache huku nje ambavyo haviwezi kufanya lolote (keep change) lakini ni mtaji mkubwa home? suala hapa ni kupendana tu!!!

     
  • Tarehe: 4:58:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    bwaya alinipokea juu juu nikasahau kilichonileta hapa. bwana Jeff, ili sanaa yetu isife inabidi kila mtu kutimiza wajibu wake. ukimtembel;ea mkwinda utaona nimekuwa nikimshawishi kufanya mpango wa kuingiza bustani za malenga zote tangu uhuru na mzalendo inaanzishwa kwenye mtandao...lakini ni kazi kubwa na wizara husika (utamaduni) ndio kazi zake, kuhakikisha kama sio kuingiza kumbukumbu hizo basi ni kuwezesha. kundi la umoja ninalifahamu. hapa afrika kusini idara ya utamaduni iko makini sana kuhakikisha kuwa utanmaduni haupotei, unakuzwa na inapobidi pia utaona kuna vionjo vinaingizwa hapa kwa kuazimwa kutoka sehemu nyingine za afrika ili kuutajirisha urithi wa mtu mweusi. watu binafsi pia hushiriki..kwani serekali ikitaka nani atapinga? na ni shughuli ya kuwafanya watu waishi vyema tu! - nchini kwetu imebaki ngoma ya kuagizwa kutika jeshini kumtumbuiza mgeni atokaye ulaya....tunahitaji mabadiliko nadhani nikisema "transfornation" inagusa zaidi......inabidi tufikie mahala hata kucheza ngoma iwe ni shughuli halali ya kumpatia mtu riziki zake!

     
  • Tarehe: 12:33:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Ndesanjo Macha

    Picha za hawa jamaa kwenye tovuti yao inaonyesha kuwa onyesho lao lilikuwa balaa tupu. Sikuwa nawafahamu. Nimewaingiza kwenye daftari langu.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker