VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Tuesday, January 03, 2006
TUNAPOFUKUZANA WENYEWE KWA WENYEWE!

Mojawapo ya madhara mabaya kabisa ya ukoloni yalikuwa na bado yanabakia kuwa jinsi walivyoligawa bara la Afrika(angalia ramani niliyoweka hapa na mipaka yake) kufuatia ule mkutano wao wa kule Berlin. Cha ajabu ni kwamba wakoloni wale hawajawahi hata kuomba msamaha! Na sisi hatujawahi kuwashinikiza waombe msamaha kisha tufute vichwani mwetu upuuzi ule ambao mpaka leo umetufanya eti tuamini kwamba mtanzania na mkenya au mganda ni watu tofauti.Hii inamaanisha kwamba sote hivi sasa,kwa njia moja ama nyingine,tunashiriki dhambi ile. Hivi kuna tofauti gani kati ya mkamba na mpare? Kati ya mhaya na mhima(kabila la Museveni),kati ya mjaluo wa Kenya na yule wa Tanzania?Mifano ni mingi sana.

Viongozi wa bara la Afrika,hata baada ya kupata "uhuru wa bendera" (uhuru kamili bado,tusidanganyane) wameshindwa kabisa kuamua kufuta utumwa ule wa kiakili.Kina Nyerere ,Kaunda,Nkrumah na wengineo walijaribu,baadhi ya wazee wetu waliwaona vioja,wakapinga kwa nguvu zote,kisa? baadhi yao walikuwa washapewa ulimbukeni wa kuvaa kaptura za khaki na kuwa wanyampara.Hata hivi sasa wanapoongelea muungano(kama ule wa Afrika Mashariki) bado wanataka kutoana macho kupigania "utofauti" wao.

Madhara ya mambo kama haya ndio yanafanya waafrika,wenyewe kwa wenyewe,tuanze kufukuzana. Huko Misri wakimbizi kutoka Sudan(kumbuka nasema wakimbizi) wanarudishwa makwao baada ya songombingo lao ambalo naamini kimsingi lilikuwa katika kutetea haki zao na kujaribu kuishi tena.Kweli ni halali kwa waafrika kufukuzana wenyewe kwa wenyewe,kwa mtutu wa bunduki?Soma zaidi hapa.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 1:50 PM | Permalink |


Maoni: 6


  • Tarehe: 7:54:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Baragumu na Jeff macho yanatoka hapa nini mipaka hii Afrika. Tukija huku tabu na huko sisi kwa sisi tabu. Nakumbuka Wakenya wa pale Mwananchi, inauma inataka moyo kutazama suala hili upya. Haya ndiyo tunayofanya hapo Zanzibar tunaita matatizo yao na kamwe hatujitoi kuzungumza ukweli. Naishia hapa huku nikitafakari kuhusu mada hii.

     
  • Tarehe: 4:08:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    matatizo ya afrika yanaletwa na ubinafsi wa waliokamata jakipoti! alichosema makene ni sahihi kabisa. kwani seif angekuwa raisi sisi tungekufa? kwani fulani angekuwa mbunge nchi isingetawalika? matatizo ya afrika yanahitaji utatuzi wa ndani halafu tuje ya nje. lakini pia tokea nje pia inaweza kuwa nzuri. mfano, EAC wamekubaliana kuwa hapo 2010 wanazungusah uraisi wa nchi zote tatu za EA halafu kufikia 2013 anachaguliwa raisi wa federation! ishu ni kuwa je JK, Musyoka na museveni wakati huo wako tayari? federation ni njia nzuri sana ya kumaliza ukandamizaji mfano uliopo uganda na tanzania kwa sasa!

     
  • Tarehe: 4:09:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    jamani pia tusherehekee kuachiliwa kwa dr. besigye na mahakama ya uganda jana! mu7 ziiiiiiiiiiiii!!!!

     
  • Tarehe: 6:36:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Christian Bwaya

    Suala la ubaguzi linakwamisha maendeleo yetu. Tunabaguana kiwendawazimu.
    Umenikumbusha jinsi ambavyo Salim alivyobigwa buti kwa sababu eti yeye hajakolea sana rangi nyeusi!
    Watu wenye uwezo wananyimwa fursa sawa kisa eti wanatoka kabila fulani! Nasikia (sina hakika) eti haitakaa itokee mchaga au Msukuma awe Rais? Tatizo ni nini hapa? Hivi wote si ni watanzania? Kwa nini tuwe na watu ambao wanawekewa mikwara mingi kwa sababu ambazo hazina kiuno?
    Leo katangazwa Kingunge, mkongwe wa wakongwe kuwa mmoja wa askari miamvuli wa Kikwete. Watu wanalalamika? Kwa nini, hivi huu si ubaguzi jamani?
    Heri ya mwaka mpya!

     
  • Tarehe: 10:49:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Bwaya,
    Uteuzi wa Kingunge hata mimi naulalamikia,hivi kweli Kikwete amekosa kabisa nguvu mpya,ari mpya katika uteuzi wake?

     
  • Tarehe: 5:25:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Jeff nadhani rejea mjadala wetu kuhusu uchumi. Nini maana ya kuwa na genge la serikali wakati vikodi vya raia vikiwa chini. Kweli Kikwete hakuhitimu uchumi, hajui hali tunayokabiliwa nayo hasa rushwa. Hajui kuongeza umati huo ni kutanua wigo na si kupunguza. Haya sasa tazama vyeo vya kujitengenezea ili tu rafiki yangu fulani apate nafasi. Kizuri wanafahamika wote. Nikifika Texas kazi ya kwanza ni kuandika wizara zinazofanana na ambazo zingeweza kuwa moja. Tanzania haihitaji more than ten ministries na hakuna haja ya kuwa na manaibu waziri utitiri. Kwa sasa siwezi kushibisha hoja zangu lakini niandikapo I will come out with an economic plan especcialy for a country like Tanzania ambayo uchumi wake umekuwa ukishuka na sio kama IMF na WB wanavyodanganya huku kukiwa na growing/expanding of economic gap btn rich n poor ambalo halijawahi kutazamwa katika historia yetu. Mungu ibariki Afrika, Wabariki maskini wote. Ameni

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker