Friday, February 17, 2006
HATUA GANI ZITAFUATA?
Ripoti ya mwanahesabu mkuu wa serikali imetoa cheche za aina yake kuhusiana na matumizi mabaya,ya kizembe,yenye harufu chafu ya rushwa na ubadhirifu.Mojawapo ya idara nyeti za serikali ambazo zimeumbuka kutokana na ripoti hiyo ni balozi za Tanzania nje ya nchi.Soma hapa. Wakati ripoti hiyo imetolewa nasikia bunge lililokuwa kikaoni Dodoma limeahirishwa. Nilidhani pangekuwepo hata kikao cha bunge cha dharura ili kuchambua ripoti hiyo na kutoa adhabu muafaka kwa wazembe na wala rushwa waliotajwa.Pili je ripoti kamili ipo wapi ili sote tuisome,kuichambua na kuanza kushika mabango yetu? Ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya wahusika ambao naamini ni wengi wakiwemo na mabalozi wenyewe? Kikwete amesema jana kwamba muda wa kulindana umeisha.Je ni kweli? Tafadhali kama kuna mwenye hii ripoti iweke hewani kwa faida ya wengi.
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 12:17 PM


|
Permalink |
-
Jeff kumbuka Waziri wa Wizara yenye Kashfa ya Rushwa sasa ni Rais sijui hapo patakuwaje. Nakumbuka wakati anawasilisha hotuba yake mwaka jana hakuulizwa swali hata moja hiyo inakupa picha ya kampeni zilivyotawala kuliko kuwajibika. Sasa yetu macho tungoje kuitafuta hiyo ripoti nasi tuisome.
-
Hii habari inastusha! Kumbe majuzi tu alikuwa yeye mwenyewe Jakaya kiongozi wa wizara hiyo? Alishindwa kuisafisha wizara yake wakati huo. makenne safi kwa kuliona hilo haraka haraka.
Pili Rais mpya katoa ahadi nyingi sana. Mwezi wa pili huu wa uongozi wake, bado hajawajibisha mtu. Bado anatisha toto.
Nitaamini dhati ya kauli zake nikiona ushahidi. Wasiseme tena ati siasa ngumu, maamuzi mengine magumu na kauli nyingine mbofu mbofu.
Tunga
-
kwa kweli tusubiri tuone. labda kwa mwendo wa mkuu BWM angekoroma angeuliwa asingezogea hata hapo...labda naye angeingiza timu na mzee wa Kiraracha!! tumpe muda inawezekana anataka watu wajisahau kidogo. na jana kapokea ya mauaji, sijui wataweka mambo hadharani au!!
Makene. mmwage Omari hadharani kibarazani iwe fundisho kwa wtu kukimbilia vyeo bila kujua nini tamu chungu zake...pia kujipendekeza!
kuna wakati niliwajhi kuuliza pale kwa blogu langu, je...Omari ni mjumbe wa NEC moja kwa moja kwa nafasi yake?? swali kwa wanablogu ni je aliombwa kukandamiza wazanzibari na upinzani au alijipendekeza?
-
Hizo taarifa za ripoti chafu za fedha zimekuwepo mara nyingi mno na wizara ya mambo ya nchi za nje imekuwa na kashfa hiyo kila wakati. Mwaka jana pia ndio iliongoza. Msisahahu pia kwamba aliyekuwa katibu mkuu wa wizara hiyo ndiye Katibu Mkuu kiongozi sasa -Luhanjo
-
Kikwete alikwapua hela za kampeni kutoka balozi hizo. Mmeshasahau rushwa aliyowapa vijana.
-
Yetu macho Msangi.
Kuhusu ripoti: unajua wakati wa serikali ambayo inatutumikia kuendesha mambo yetu kwa kificho unafikia kikomo. Ripoti kama hizi tunazisikia zikitajatajwa kwenye vyombo vya habari. Kwanini tusipewe tuzisome? Nadhani kuna haja ya kuanza kufunza wanablogu ambao wako jikoni wawe wanablogu kwa majina ya kalamu ili wawe wanatupa taarifa ambazo kimsingi ni zetu ila hawa wezi hawataki tuzijue.
Jeff kumbuka Waziri wa Wizara yenye Kashfa ya Rushwa sasa ni Rais sijui hapo patakuwaje. Nakumbuka wakati anawasilisha hotuba yake mwaka jana hakuulizwa swali hata moja hiyo inakupa picha ya kampeni zilivyotawala kuliko kuwajibika. Sasa yetu macho tungoje kuitafuta hiyo ripoti nasi tuisome.