
Katika muendelezo wa uchunguzi wangu kuhusiana na chuo cha polisi cha Ontario (pichani) na kivuli cha uhitimu wa mkuu wa jeshi la polisi Tanzania leo nimewasiliana na wahusika wa chuo hicho kwa njia ya simu.Kwa bahati mbaya sera zao za ubinafsi haziwaruhusu kutoa habari zozote za kitaaluma kumhusu mtu yeyote aliyewahi kuhitimu au kupitia kwenye madaraja na korido za chuo chao. bila ruhusa ya kimaandishi ya mhusika.Nikawa nimekwama.Ila nilichoweza kudadisi na kugundua ni kwamba chuo kinatoa certificates na diploma tu na kuna vyeti vya hata kozi za siku mbili ama tatu.Lakini uchunguzi bado unaendelea.Je kuna mtu anaweza kunisaidia na mwaka ambao mheshimiwa wetu alihudhuria chuo hiki?Kivumbi na jasho.
Jeff nazidi kushukuru jitihada hizi. Maana wasishangae watu tunatafuta taarifa za kuandika Orbituary si unajua waandishi tunazitunza kabisa kwenye Rpways kusubiri tu siku. Lakini tukikamilisha taarifa hizi lazima niruke naye huyu kwenye makala Bongo.