VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Tuesday, February 21, 2006
NANI MTANZANIA?
"Mi akulia pae pae Kaiakoo,jumba ya baba angu pale mtaa wa chikichi,mie furahi sana leo kutana na tanzania enzangu" Hiyo ni sauti na maneno kutoka kwa jamaa fulani ambaye tumekutana dakika chache zilizopita.Aliona beji yangu imeandikwa Jeff Msangi,akakumbuka kina Msangi anaowajua,akahisi na akawa sahihi kwamba pamoja na hilo jina la kizungu la mwanzo,waasisi wa uwepo wangu hapa duniani wamelala mapumzikoni nchini Tanzania.Ananiambia ana miaka 40,anasema ameishi Tanzania maisha yake yote mpaka hivi majuzi alipokuja Canada.Ana miezi michache tu tangu aingie nchi hii.Ninaanza kumuuliza masuala ya nyumbani,namuuliza katika uchaguzi uliopita alimchagua nani?Nani alikuwa mgombea wa ubunge jimboni mwake,nani aliwania udiwani wa kata yake?Naona jamaa anaishiwa nguvu,anataka kuondoka pale tulipoketi.Sina budi kuendelea kumuuliza maswali yangu.Wananchi wanasemaje kuhusu utendaji wa raisi Kikwete?Hivi waziri wa mambo ya ndani ni nani hivi sasa? Sina budi kuachana na maswali haya ya siasa.Sio kila mtu anapendelea kujadili au kujua habari za kisiasa.Si unajua tena siasa zilivyo jaa uongo wakati mwingine?

Hivi inakuwaje uzaliwe na kukulia Tanzania lakini kiswahili chako kinakuwa matata matupu? Hivi jeshi la polisi lina askari wangapi wenye asili ya asia? Hivi kuna wangapi miongoni mwa koo zenu na jamii zenu kule Segerea? Hivi ni kwanini pale katikati ya jiji la Dar-es-salaam nyie huonekana mitaani nyakati za jioni zaidi? Hivi kuna wahindi wangapi wanachezea timu yoyote katika ligi za mpira wa miguu Tanzania?

Inakuwaje hapa Canada umoja wa watanzania hauna wahindi wakati ambapo takwimu za serikali ya Canada zinaonyesha kwamba kuna watanzania lukuki kwa sababu tu walitumia pasipoti za kijani kuingia Canada? Huwa mnajificha wapi washikaji?

Ee bwana ee nikatoka kwenda chooni,kurudi jamaa hayupo! Kaenda wapi,sijui.Kitendo cha huyu jamaa kunikimbia wakati tunajadili masuala ya "nyumbani" nimeshindwa kukielewa hata hivi sasa ninapoandika.Hata sijui ninaandika nini.Swali langu linabakia kuwa moja,hivi ukiwa hujui kuhusu siasa,uchumi,historia,mila na tamaduni,jamii nk ya nchi unayooita nchi yako,unastahili kweli kuwa mwananchi?Utanzania ni nini?Je Tanzania ina matabaka mangapi ya wananchi? Hapa Canada ukiomba uraia wa nchi hii lazima ufanye na ushinde mtihani ambao una hakikisha kwamba unajua masuala niliyoyataja hapo juu.Hudhani Tanzania nayo ianzishe utaratibu huo? Najua huu unaweza kuwa mjadala mrefu,baadaye nitarudi na kuedit.Tujadili jamani.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 11:44 AM | Permalink |


Maoni: 12


  • Tarehe: 12:55:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Jeff mtafute huyo hata kama yuko chooni mfate
    mtafute mueleze uzandiki mwisho wake mueleze
    Mueleze aelewe kutojua si ujinga aelewe
    Aelewe Tanzania sii yake ajivue atambue.

    Atambue nchi yake ya awali atangaze
    Atangaze akotoka tupajue tuelewe
    Tuelewe tumjuze nchi yetu asiponze Asiponze abaini wenye yao tungalipo
    Tungalipo twatambua wenye nguvu twajulia
    Twajulia tukali ughaibuni aelewe
    Aelewe kuitwa mtanzania si kumiliki pasipoti.

     
  • Tarehe: 1:46:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Labda kajificha chooni.
    Swali jingine: wangapi wenye asili ya kiasia wako jela? Au wao huwa hawavunji sheria?

     
  • Tarehe: 8:51:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger John Mwaipopo

    tehe! tehe! hii nitachangia kwesho

     
  • Tarehe: 10:13:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Hodi!

    Miye sina blog lakini nina tabia ya kuandika na kutuma maoni yangu juu ya mambo anuai kwenye anuani kadhaa za watu ninaowafahamu. Niliwahi kutuma maoni yangu kufuatia kauli aliyotoa Balozi Ramia kwamba "Urafiki wa Tanzania na India ni wa kidugu" wakati alipokuwa anamuaga aliyekuwa kwa balozi wa India nchini Tanzania.

    Katika maoni hayo niliuliza maswali kama uliyoliza Ndugu Msangi: Kama tuna udugu na Wahindi mbona hatuoleani nao? Hatusali kwenye majamati yao? Mzungu na Mwarabu tunasali nao. Tunaoleana nao. Machotara wa Kizungu na Kiarabu wapo kila mahali Tanzania lakini wa Kihindi hamna na kama wapo wachache sana tena mno kabisa. Mungu wa Waarabu na Wazungu ndiyo wetu japokuwa upapa hatuupati lakini uburuda, utawa, upadre, uaskofu na ukadinali tunaupata. Hali kadhalika ual haji, uimamu na ushehe miskitini tunaupata. Lakini kwenye majamati ya Wahindi ukimuona Mtanzania kaingia jua boi kaenda kufagia au kolokoloni kaenda kulinda. Ikifika saa ya sala wanabakia wenyewe kina Manoj, Prakash, Sandip na Rajesh.

    Nikaendelea kusema kwamba hakuna mcheza mpira wa miguu hata mmoja wa klabu yoyote inayojulikana kitaifa nchini Tanzania yenye mchezaji muhindi. Lakini vilabu vikubwa viwili Simba na Yanga na vizee kuliko vyote nchini Tanzania vipo au vimepata kuwa chini ya uongozi wa wahindi kama kina Marehemu Mohamed Virani, Marehemu Muheshimiwa Abdulabass Gulamali, Mohamed Dewji, na Azim Dewji. Pia Tukuyu Stars ilikuwa mali ya Muhindi Patel Kaka. Tena kibaya zaidi kuhusu kuongoza timu za kandanda ni kwa minajiri ya kupata jina ambalo baadaye hulitumia kukwea ngazi za kisiasa hususani kupata nafasi za ubunge ambazo huwasaidia sana katika kulobi masuala yao ya kibiashara na kijamii kuliko kisiasa. Ninakubali kwa dhati kwamba kuna wabunge wengine Watanzania weusi ambao katika kipidi chote cha miaka mitano huwa hawajawahi kutoa maoni au kuuliza maswali lakini nina hakika kitakwimu (kama zipo) wabunge wa asili ya Kihindi ni wengi zaidi ambao hawatoi maoni wala kuuliza maswali kwa kipindi chote wanachotumikia bunge. Wanapata kura zao toka kwenye majimbo na wilaya za mikoani walipojaa Watanzania maamuma. Nimewaita Watanzania maamuma kwa sababu siwezi kuwaita wajinga au waliochelewa. Asilani huwezi kusikia Muhindi anagombea ubunge wilaya ya Ilala au Temeke! Akigombea Dar es Salaam atagombea jimbo la Kawe ambalo lina vitongoji kama Boko, Goba, Wazo, na Tegeta ya zamani ambavyo ni mashamba na vyenye wakazi Watanzania Maamuma ambao hawana tofauti na Watanzania wengine wa vijijini. Naomba tuuangalie ukweli huu kwa kuangalia wabunge wa Kihindi wengi wao japokuwa ni wakazi wa Dar es Salaam huwa wanawakilisha majimbo gani.

    Baada ya kuangalia ukweli huo sasa twende katika shughuli za ajira za kiserikali. Tuna madaktari na wauguzi wangapi wa kihindi kwenye zahanati na hospitali za serikali? Wauguzi na madaktari wangapi wenye asili ya Kihindi wapo kwenye zahanati na hospitali za binafsi? Pia walimu waliopo kwenye shule za vidudu, msingi, sekondari, vyuo vya ualimu, ufundi, kilimo, vyuo vikuu na taasisi zingine za elimu za serikali. Halafu tuangalie na walimu wenye asili ya kiasia walioajiriwa katika taasisi za elimu za binafsi.

    Sasa tuangalie Wahindi walioajiriwa kwenye makampuni ya serikali na wale walioajiriwa kwenye makampuni ya binafsi na ya wawekezaji. Halafu tuangalie nafasi walizomo wahindi kwenye makampuni ya wawekezaji na zile walizopo wazawa kwenye miradi na makampuni ya wawekezaji. Mwaka 1999 nilipokuwa Tanzania nilifanya utafiti wa haraka haraka kuangalia nafasi za za Watanzania katika miradi na makampuni ya wawekezaji baada ya kutembelea benki moja ya wawekezaji na kukuta kwamba Watanzania walikuwa katika ngazi za chini ndani ya benki hiyo. Nilishangaa na kusikitika sana tena mno kukuta kwamba katika ngazi nyingi za juu za makampuni au miradi ya wawekezaji Wahindi huwa ndiyo wanaofuata kwa ngazi za vyeo baada ya wawekezaji weupe. Lakini nikakuta kwamba katika miradi na makampuni ya wawekezaji wa Kiafrika ya Kusini Muhindi hakuwa na nafasi za juu kama alizokuwa nazo katika miradi ya wawekezaji wa nchi za Ulaya, Marekani, Canada, Australia, au New Zealand!

    Jinginewe, ulilozingumzia ndugu Msangi suala la lafudhi. Kuna siku niliwahi kumwambia swahiba wangu mmoja wakati tukitazama habari kutoka BBC iliyokuwa ikisomwa na mtanzangazaji wa Kihindi. Nikamwambia unaiskia sauti Muhindi huyu ni kama ya Muingereza. Swahiba wangu akaniamba "..ni kweli, tena anaongea Kiingereza kama Muingereza." Nikamuuliza "..Sasa kwa nini wakiwa Tanzania hata kama ni wa kizazi cha nne bado anakuwa na lafudhi ya kihindi?.." Swahiba wangu akanijibu "..unajua kule Bongo huwa hawajichanganyi lakini huku yuropu wanajichanganya.." Nikamwambia "..sawa.. " kwa sababu sikutaka tuanzew mabishano kwa sababu huyo swahiba wangu ni mabishano.com ukianzisha naye ubishi ujue hautaisha.

    Sasa kwa kumalizia naomba ukitua uwanja wa ndege Dar es Salaam uangalie kama kuna ofisa Uhamiaji wa Kihindi? Halafu ukienda Posta Mpya upande wa Mizigo uangalie kama kuna Muhindi, halafu nenda bandari upande wa makonteina uangalie kama kuna Muhindi, Bohari Kuukama kuna Muhindi halafu ukiwakuta jiulize kwa nini wapo huko na siyo Kampuni Ya Mabasi ya Taifa KAMATA?

    F MtiMkubwa Tungaraza

     
  • Tarehe: 3:02:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    kha hii makala Tamu! nadhani sasa kwa kiasi fulani tunapaswa kuupandisha uzawa chati! nilibwabwaja juzi pale kwa Tunga..kuhusu hulka tabia au uwezo wa hawa wenzetu kwenye kuona opportunities - mianya! ukipewa uafisa wa TRA au dhamana ya serekali (mpaka enzi za utawala wa Mkapa BWM sina uhakika sana sasa) hawa watakuwa marafiki zako! ukipigwa chini the next day hawapo na wewe! wako na mdhamana mpya - nilishangaa sana walishirikiana na mzee ruksa kuendesha shamba kule dakawa-alilobinafsishiwa (nimelisahau jina walilolipa), alipoondoka kwenye kiti tu, nao hawakukaa sana wakawithdroo!! hawa huwa hawajengi nyumba mitaani bali kukaa kwenye maghorofa anayopigia kelele Magufuli mijini, huhakikisha kuwa asseti zao ni zile zinazohamishika upesi kwamba hata wakiambia wadepartiate hawatahitaji masaa hata 6 kujikusanya! kwa maana hii hutaona maendeleo yaliyowekwa kwenye akaunti ya beni ya kigeni ambayo ana uwezo wa kwenda kuitumia Kanada na kumnunulia soda kaka Msangi! - kibaya sasa wakija kutaka mahoteli na biashara zetu tunawapa wao na Mheshimiwa sana Masilingi anamnyima Mengi ambaye angalau angetunza round about ya Kariakoo na kuongeza majengo na ajira na bila kusahau kupeleka atoto kutibiwa! utaona lions wananunua feva kupeleka wagonjwa kutibiwa india badala ya kupambana kuimarisha kituo cha osheni rodi!

    kuna tendency ambayo nimeiona kwa wahindi wa Tanzania na sasa kwa wazungu wabaguzi hapa Afrika kusini! wahindi wa tanzania wakizeeka wanaamuunganishia mpangaji mungine vigofu vyao halafu wanahamishia mtaji wao Canada kwenda kula pensheni na kujenga uchumiwa kanada. kaka Jeff naye kwa kuliona hilo akaamua kwenda kubanana nao huko huko! wazungu wabaguzi wa hapa kusini ambao kila kitu wanaona kibaya kinachofanywa na kina mbeki wakilinganisha na vya Botha na De clerck! utasikia hamna kitu enzi hizo posta ilikuwa very efficient! barabara zilikuwa very clean! bili zilikuwa safi sana!! kumbe enzi hizo hawa wazungu ni kuwa walikuwa hawalipi bili halahli za umeme na maji, na ok. kwa ujumlla ni kuwa walikuwa wanabebwa na weusi, kodi yote ndio wakawa wanatumia wao na kujifagilia! huku hii kitu inaitwa rural development kwa kweli bongo tumejitahidi!! sasa hawa weupe pia wanafanya kila kitu kukamua nchi na hatawakiwa kwenye miradi huiba kweliiiii...na kuhamishia hela yao Canada...wakiwaachia weusi nchi yao!!

    kwa maneno haya naomba kutoa hoja! MJENGA NCHI NI MWANANCHI NA MBOMOA NCHI NI MWANANCHI! TUMUUNGE MKONO IDDI SIMBA NA MTIKILA KWENYE HII MAMBO YA UZAWA KWANI SIE TUKIZEEKA TUNATAKA KUBANANA PALE PALE BONGO KANADA HAENDI MTU!

     
  • Tarehe: 4:56:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

    kuna waziri wa muda mrefu wa Tanzania mwenye asili ya kihindi, mzalendo tangu uhuru, nasikia alipokufa alizikwa kanada, wala si morogoro kwenye jimbo lake tangu uhuru. Kwao wapi?
    Hili ni swala nyeti,na linapaswa kuzungumzwa bila jazba wala ubaguzi.
    Wakati wa kurekebisha mambo ni huu, tushike hatamu wenyewe. Wapumbavu wanaokwenda dina pati za kina rajpa na kuandika mikataba lazima wasemwe, na ikibidi akina Kikwete waunde tume kama iliyomuumbua mahita, ushindi mdogo mdogo mpaka kieleweke.

     
  • Tarehe: 12:14:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger MICHUZI BLOG

    mie naomba kuulizia kuna umuhimu wa kuwa na uraia miwili (sijui ni kisahili sahihi cha dual citizenship?) tanzania? je ni kweli mlio huko wengi mmejilipua (kuwa raia wa huko peke ama wa huko na huku?) naomba kutolewa tongotongo...

     
  • Tarehe: 12:31:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Nimemaliza kusoma Mti Mkubwa (Mkavu...jina kaongeza Michuzi hilo). Nafurahi sana mijadala inapojitokeza bloguni namna hii. Mti Mkubwa ni mwanahistoria. Namshukuru sana kwa maoni yake anayotoa katika blogu mbalimbali.

    Michuzi: nimepewa taarifa na Kasri kuhusu maoni yako kule kwenye mjadala wa neno blogu. Nitasoma baadaye na kuweka neno langu.

     
  • Tarehe: 7:57:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger John Mwaipopo

    Kizazi cha blogu sasa kimeamka. Walau kwa kusema yatosha kupunguza makali na masaibu tuliyonayo moyoni.

    Hawa jamaa huifanya Tanzania gateway yao, hasa ya kwenda Canada. Ni ni wengi chini Canada kuliko kwingineko. Tanzania hata sasa haijaamuu suala la uraia muwili (dual citizenship) lakini TZ hiyo-hiyo imelala usingizi kwa kutowachunguza hawa jamaa. Wana uraia wa nchi Mbili.

    Kule mbeya kuna tajiri anaitw Kanji Larji. Familia yake yoote iko Canada. Kule ni kwa kutafuta pesa tu na si vinginevyo e.g hata kujifunza lugha ya kuzugia. Ywezekana hapa Kodi hawalipi vema.

    Mnajua kuwa hata ujira kwa wafanyakazi wao ni duni kuliko kwingineko? Hawa ndio tuliokuwa tukiwajadili kuwa ndio "Tanzania Business Community"

    Pengine fikra zangu za kutest zahali katika siasa ni kwa minajili ya kutoa uozo huu, walau kwa mchango iwapo sitaganikiwa kuwemo 'ndani'.

    Vijana tumeamka na kitakapopita kizazi hiki kilicholala usingizi wa pono cha moto lakini cha haki watakiona. Hivi sera ya Mchungaji Mtikila Juu ya hawa aliowaita Magabacholi ilikuwa sio sahii?

     
  • Tarehe: 10:15:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Michuzi,
    Kuna umuhimu fulani wa kuwa na uraia wa nchi mbili au zaidi kutegemea na mazingira na kama kuna sababu za kimsingi sana katika kufanya hivyo.Raia wengi wa Canada ni raia wa Marekani pia kama ilivyo kwa wamarekani kuwa wacanada pia.Lakini ukiangalia hizi nchi mbili mambo yao mengi haswa ya kiuchumi yanashabihiana.Tatizo linakuja pale wanaopigia debe Tanzania tuwe na uraia wa nchi mbili wanapokuwa wachache ambao wanachotaka ni kupanua mirija yao ya kudhulumu na kuiba mali ya umma,tunawajua!

    Mwaipopo:Sera ya Mtikila haikuwa na mbaya,kulikuwa na tatizo la kueleweka.Lakini nakuhakikishia sera ile ipo njiani,itarudi tu

     
  • Tarehe: 6:57:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    si mnakumbuka Mrema aliwajibishwa kwa "kutoka nje ya line - kutoact in a collective responsibility" - kwa mujibu wa waziri mkuu wa wakati huo Cleopa Msuya baada ya kuhoji hujuma ya Chavda alihujumu mahela mengi ya taifa akidai anaboost kilimo kumbe anakula kwa namna nyengine! uzito wa serekali kujituma pia ni tatizo! nilipata habari katika hii serekali iliyopita kule wizara ya kilimo kuna hela zilikuwa zinaozea za kusaidia wajasiriamali wa kilimo katika era hii ya utandawazi - kisa wanaogopa kukopesha wazawa! kwa kweli nakiri kuwa ujasiriamali wa wazee, wa sisi wa kati na wale watoto waliokuwa wanachezea kumpyuta pale kwa michuzi ni tofauti!! tuwaamini na vijana sasa kama sie wakubwa wakubwa tunaogopa!!

     
  • Tarehe: 8:24:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Muhidin,

    Kujilipuwa na kuwa na urai wa nchi mbli ni masuala mawili tofauti kabisa.

    Kujilipuwa ni mtindo ynaotumiwa na baadhi ya watu wa taifa fulani kuomba ukimbizi kwa kutumia utaifa mwingine. Kwa mfano, maijeria anweza kujilipua kama Msierra Leone ili aweze kupata vibali vya kuishi kwenye nchi ambayo amejilipulia. Natumaini umenielewa.

    Suala la uraia wa nchi mbili siyo geni hususani kwa mataifa yaliyoendelea au yaliyotawala nchi zingine. Kwa mfano, mzawa au raia wa Australia, New Zealand, Canada, Marekani wanaweza kuwa raia wa nchi hizo pia nchi yao ya asili kama Uingereza na Ireland. Hii pia inatumika hata katika nchi kama Zimbabwe, Afrika ya Kusini,na Namibia. Kutokana na mchezo huu wa ambao nikirejea sayansi ya shule msingi ninaweza kuuita "litmasi pepa" ambapo unaweza kuwa rangi fulani katika mazingira fulani na nyingine katika mazingira mengine inafaidisha sana. Tukichukulia mfano, wakulima(farmers) na walowezi(settlers) wazungu wa Zimbabwe. Wameweza kuhodhi ardhi na mashamba kwa kutumia urai wa nchi mbili. Wamehodhi ardhi na mashamba kwa kutumia uraia wao wa Zimbabwe na wameweza kutetewa wasinyang'anywe mashamba na ardhi hiyo ya Zimbabwe kwa kujisalimisha kwenye urai wao wa Uingereza. Natumaini umenielewa.

    Kuhusu Watanzania kuomba kuruhusiwa kuwa raia wa nchi mbili ni suala ambalo mimi binafsi nimelisikia likiwakilishwa katika vikao vingi na viongozi wetu wa kisiasa ambao huwa tunapata nafasi ya kukutana nao wanapokuja ziarani huku ughaibuni. (Nafasi za kukutana na kuongea na viongozi wetu ana kwa ana nadhani sisi tulio ughaibuni ni moja ya mambo (priveledges) ambazo wenzetu waliopo nyumbani hawazipati kabisaaa!). Nakumbuka tulipoonana na aliyekuwa Waziri Mdogo wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Abderkadeer Sharrif, suala hili lilijadiliwa na Balozi Sharrif alisema kwamba kwa upande wake haoni sababu zozote za kimsingi za kumzuia Mtanzania kuwa na urai wa nchi mbili. Hali kadhalika tulipokutana na Rais wa Zanzibar Ndugu Amani Karume katika mkutano naye suala hili lilijadliwa tena. Rais karume alipochangia hoja alisema kwamba urai ni suala la mtu kujiamulia kwa hiyo hakuona ubaya wowote wa Mtanzania kuwa rai wa nchi nyingine na akaongeza kusema kwamba suala hili bado linatathiminiwa na vyombo husika. Kadhalika tulipokutana na Rais Mkapa alisema bado hatujawa tayari kuwa na urai wa nchi mbili lakini hakutupa sababu zozote za kimsingi za kutokuwa tayari kuwa na urai wa nchi mbili.

    Swahiba wangu Dennis Londo aliwahi kunionyesha tovuti ya Watanzania warufani wa suala la uraia wa nchi mbili akaniambia kwamba yeye binafsi haoni ubaya juu ya hilo lakini akanitahadharisha kwamba wengi warufani hao ni wale wenye asili ya Kihindi na wengi wao anuani zao zinatokea Kanada.

    Jinginewe ni kwamba tukilikurupukia suala la urai wa nchi mbili linaweza kuleta athari mbaya zaidi ya zile zilizoletwa na suala la soko huria. Ukizingatia kwamba wageni ambao wataweza kuhitimu vigezo vya uraia wa nchi mbili watakuwa na mitaji mingi na mikubwa ya kihali nammali kuliko Watanzania na hivyo kuwa na ukoloni wa wenyewe kwa wenyewe kama ilivyo nchini Liberia.

    Wanablog naomba mlipandishe suala hili kwa minajiri ya kulijadili kwa kina zaidi.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker