VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Saturday, February 18, 2006
NDANI YA NCHI MPYA?


Ni asubuhi na mapema jijini Dar-es-salaam.(pichani kushoto)Kijua cha mashariki kimeshachomoza.Nachungulia dirishani na kuona kwamba tayari kumekucha.Nimechelewa kudamka kama kawaida yangu baada ya sherehe za jana usiku kusheherekea kupitishwa kwa mradi wa kuanzisha matumizi ya umeme unaotokana na nuklia. Magari tayari yameshajaa barabarani,hizi barabara sita upande wa kwenda na sita upande wa kurudi karibuni zinazidiwa uwezo wa kuhimili wingi wa magari hapa jijini.Lakini sina wasiwasi sana,majuzi raisi ameahidi kupitisha mradi wa kujenga barabara zingine kwa juu,yaani ziwe zile za gorofa.Wanamazingira nao wameshaandika sera za usafi wa mazingira ambazo zitahakikisha moshi unaotoka kwenye magari unapunguzwa madhara yake kwa afya za wananchi kadiri itakavyowezekana.

Nachungulia nje ya na kumuona jirani yangu akimwagilia bustani yake.Yeye ameshastaafu na ni majuzi tu alikuja kunitembelea majira ya jioni.Tuliongelea mambo mengi sana ingawa mpaka leo nakumbuka mawili muhimu.Alisifia utendaji wa serikali katika kuhakikisha wastaafu hawapati tena matatizo ya malipo ya mafao yao.Anasema anafurahia maisha yake ya uzeeni.Pili akazungumzia jinsi ambavyo ujambazi umepotea kabisa.Akanikumbusha enzi zile za ambapo usingizi ulikuwa wa nadra kwa jinsi ambavyo ujambazi ulikuwa umetawala mitaani.Anasema imepita miaka kumi na tano sasa hajawahi tena kusoma au kusikia habari za ujambazi.

Sina budi kujiandaa na kuwahi kazini.Serikali ya leo haitaki masihara kwenye suala la uwajibikaji.Kila mtu anatimiza wajibu wake bila mizengwe.Hata hivyo baadaye itanibidi niende kumuona daktari wangu wa familia kwa ajili ya uchunguzi wa afya yangu wa kawaida kila baada ya miezi sita.Vyuo vyetu vinatoa madaktari mabingwa na wataalamu wengine wa fani mbalimbali.Nakumbuka zamani kuwa na daktari wa familia ilikuwa ni kama ndoto.Maisha kweli yamebadilika.Upepo wa bahari hindi unavuma,nakumbuka zamani pembezoni mwa bahari palikuwa hapatamaniki kwa harufu mbaya.Kweli hawa watu wa mazingira wanafanya kazi yao sasa.Natamani nikanywe kahawa yangu ya asubuhi pale ufukweni,nione mwendo wa mawimbi ili nianze siku kwa nguvu zaidi.

Njiani nakutana na mabasi ya umma,enzi zile tulikuwa tunayaita daladala(pichani juu kulia).Siku hizi ya utaratibu maalumu na yanakwenda kwa kufuata muda maalumu.Ukitaka kwenda Ubungo kutokea Sinza unaweza kufanya makadirio ya muda utakaotumia.Unakumbuka enzi zile makondakta walivyokuwa wakipasua mishipa ya makoo yao kwa kuita abiria? Siku hizi wengi wao wamepata kazi viwandani,wanalipwa ujira mzuri tu na mazingira yao ya kazi yamejaa ubinadamu.Nasikia juzi yule jamaa aliyeteguka kidole akiwa kazini kalipwa fidia ya shilingi laki nane bila usumbufu wowote.Enzi zile angempa hakimu shilingi ngapi kati ya hizo laki nane?

Sikuwahi kudhani kama tungefika hapa.Usafi uliopo jijini Dar-es-salaam hivi sasa sijawahi kuuona dunia nzima.Nyasi na maua zimepangwa zikapangika.Jana nilipoenda muhimbili kumtembelea mjomba wangu aliyelazwa nilitamani nilale palepale. Nakumbuka enzi zile za uharo wa rushwa,enzi zile ambapo hata mfagizi aliniomba rushwa ili aniruhusu kupita mahali alipokuwa ametoka kusafisha.

Radioni nasikia jinsi ambavyo uhuru wa kujieleza na kujisemea unavyofanya kazi.Mtangazaji anaeleza jinsi jamaa mmoja alivyomwambia raisi ukweli juu ya tabia zake za kizinzi.Enzi zile angeozea jela huyu bwana.Hata kama sheria haipo ingetungwa dhidi yake,kumdhalilisha raisi au amiri jeshi mkuu.Jambo moja la wazi ninapoelekea kazini ni kwamba ile tofauti ya maisha kati ya mitaa fulani imepungua sana.Nashindwa kugundua kwamba nimetoka Kibanzi,nimepita Kongowe,nimepita Kimara,nimepita Ubungo,nimepita Manzese,nimepita Magomeni na sasa naingia Kisutu.Duh,tumetoka mbali,hatujafika mwisho lakini angalau tumefika mahala.Simu yangu ya mkononi inaita,tutaongea baadaye......
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 5:52 PM | Permalink |


Maoni: 8


  • Tarehe: 5:18:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger MICHUZI BLOG

    sikujua kuwa u mtenzi mzuri. hongera, nimefurahi kukusoma, ushairi wako wafaa tungiwa kitabu.

     
  • Tarehe: 5:19:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger MICHUZI BLOG

    sikujua kuwa u mtenzi mzuri. hongera, nimefurahi kukusoma, ushairi wako wafaa tungiwa kitabu.

     
  • Tarehe: 6:37:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    yeah! that is the dream land! kazi imeishaanza hakuna kurudi nyuma! tuna uhakika JK hatatuachia boga lituongoze! vivo hivyo..tuna hazina nzuri tu ya watu wanaofahamu mambo na wanablogu wakichombeza chombeza....kuna kila dalili ya merikebu kufika inapokwenda....

    kuna hili tatizo la nishati. siku hizi wenzetu wengi wanatumia nuclear plants, hata hapa afrika kusini...na nimesikia pale milima ya uluguru tuna uranium ya kutosha...sikumbuki yale mafuta waliyosema yapo yaliishia wapi....JK juzi akihutubia ile cocktail ya wafanyabiashara aliwaomba wasaidiane kubrainstorm kuwa ni kwanini Tanzania pamoja na utajiri wote huo hautumiki ?? pengine sasa tunaingia kwenye era ya kisasa ambayo inahitaji watu wa kisasa kujibu matatizo ya sasa...ilikuwa hotuba nzuri sana iko kwenye mtanzao wa serekali...naomba na sie tumsaidie kumjibu.....

    nadhani swali hili hata iran ndio wanapambana nalo dhidi ya mmarekani???

    cheers

     
  • Tarehe: 3:32:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Simu inayoita inapiga kelele sana. Abiria mmoja anakuuliza kama umesoma Magazeti Tando ya siku hiyo. Mkononi ameshika gazeti lililotanuka kutoka Gazeti Tando na sasa linachapishwa kabisa na kusomwa bure mtaani. Gazeti hili limetambua kuwa gharama za uchapachi zaweza kulipwa na matangazo ya makampuni ambayo yameongezeka sana. Gazeti hili nasikia lina historia. Lilianza mtandaoni kama mzaha hivi na sasa linasomeka na linapendwa, abiria huyo anakuonyesha jina lake, unatzama na kucheka sana, linaitwa Kasri la Mwanazuo. Kicheko chako kinapaa hadi unasahau kuwa umefika Posta na ulipaswa kushuka, unacheka na kucheka huku ukikumbuka kuwa harakati hizi zilianza kama ndoto.

     
  • Tarehe: 4:53:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger John Mwaipopo

    utenzi mwanana isipokuwa umesahau kukadiria miaka ya maendeleo.Miaka 15! Ingependeza ungechomekea miaka kama 100, 150 na kuendelea. Hata 'majuu' waliendelea kwa miaka mamia. Kwa mfano barabara ya gorofa ya Ferry New York peke yake ilichukua zaidi ya miaka 20.

    Pia ingeswihi sana kama hadithi za magumu yaliyopo Bongo zingekuwa kama umezisoma vitabuni vile.

    Kwa mara ya kwanza leo nimeona Michuzi kacomment kwa wengine. Maana amekuwa hatambelei 'blogu' za wasomaji wake. Inaonyesha kwa jinsi gani utunzi wako u-mahiri.

     
  • Tarehe: 6:02:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Makene,ahsante sana kwa mwendelezo huo.Tutafika
    Mwaipopo,nadhani ushauri wako ni safi sana.Itabidi niweke toleo endelezo la haka-kahadithi.Ahsanteni wachangiaji wote.

     
  • Tarehe: 5:33:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    Makene, nilikuwa sijawahi kusema. labda nilikuwa sijui wewe ni mwandishi. naamnini magazeti tando yatayozaliwa huku mtandaaoni yatakuwa na uwezo mkubwa wa kutekeleza wajibu wake na kwa haki katika jamii ya watanzania! mungu bariki safari yetu na ya watoto wetu napia wajukuu na watukuu wetu!

     
  • Tarehe: 9:08:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Moja ya mambo yanayotufanya tuwe binadamu ni uwezo wa kuwa na ndoto. Kuwa na ndoto, na pia kuzifanyia kazi.
    Najua mtasema ninapigia debe wordpress, lakini unajua Jeff huwa unatoa simulizi fulani poa sana. Zinafurahisha. Hazichoshi kusoma. Na wakati huo huo zinaelezea mambo fulani mazito sana. Staili hii ni nzuri sana kuzungumzia mambo mazito bila kuchosha. Sasa kungekuwa na uwezo wa kuweka simulizi zako au hadithi kwenye kiungo pekee ambacho msomaji akija anaweza kuzisoma wakati wowote ingekuwa poa sana. Kuna nyingine ile uliwahi kuandika nimesahu uliipa jina gani, nikitaka kuisaka leo nitapata tabu sana. Lakini kama programu ya blogger ingeweza kukupa uwezo wa kupanga mambo kimaudhui, ambacho ningefanya ni kubonyeza kwenye maudhui ya hadithi au simulizi.

    Ndoto hizi muhimu sana kuwa nazo maana bila hivyo hatutaweza kujenga kesho tunayoitaka, hatutaweza kujua tunataka kesho ya namna gani.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker