VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Sunday, February 19, 2006
SAFARI NDIO IMEANZA?

Lile tulilokuwa tunalisubiri kwa hamu limeanza kuchomoza.Ile imani niliyokuwa naiota na kuitamani imeanza kuwa ni ndoto ya kweli.Ule usemi kwamba muosha naye huoshwa si alinacha za kina babu na bibi tu.Majuzi tume aliyounda Raisi Kikwete kuchunguza mauaji waliyofanya polisi kwa kisingizio cha "ujambazi"iliwasilisha ripoti yake ya uchunguzi ambayo iliambatana na kutoa mapendekezo.Matokeo yake ni haya hapa.Tafadhali yasome kabla hujaendelea. Tume hiyo iliongozwa na Jaji Kipenka Mussa(pichani kulia) ilifanya kazi kwa siku 21 tu,tofauti na zile zilizokuwa zinafanya kazi mwaka mzima kisha senene wanaanza kuruka.

Binafsi nimefurahi sana kwa sababu wasiwasi wangu ulikuwa tume zilikuwa zinatumika kama makaburi ya haki.Ilikuwa ni mpako wa mafuta kwa mgongo wa chupa.JK anaanzisha historia mpya ya kutogeuza tume kuwa makaburi ya haki.Lakini kama ulivyo wewe,bado natamani kusikia nyangumi akiibuliwa kutoka majini.Naamini hawa 15 ni dagaa wadogo tu katika bahari nene na yenye kiza totoro.Atawafanya nini wale waliokuja mbele ya microphone na kutetea utumbo? Utendaji wao na kauli zao hazitoshi kuhakikisha wanaelekea Kisutu kujibu mashtaka pia? Lazima kuna jambo litafuata au ni lazima lifuate.Nimekubali kwamba raisi Kikwete ni msomaji mzuri wa blogu zetu.Nilidhani ukachero wa rafiki yangu ulikuwa butu,hapana.

Kwa mbali nasikia sauti ya treni kutoka bara.Nauona mwanga ingawa bado unakatikatika.Nadhani ni kwa sababu ya mabonde na milima yaliyopo katika nchi yetu.Kuna jamaa ananigusa begani na kuniuliza "Bwana Jeff,hivi ungekuwa wewe ndio raisi aliyepita Ben Mkapa,ungejisikiaje kuona kwamba uliunda tume lukuki ambazo mapendekezo yake uliyatupa kapuni? Eti ungekuwa wewe ungejisikiaje kuona mwenzio anaanzisha safari ambayo ilikuwa iwe inafikia mwisho hivi sasa?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 6:21 PM | Permalink |


Maoni: 5


 • Tarehe: 2:27:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

  Naona tuanze na Jakaya Watch. Hapa kafunga goli moja katika miezi miwili ya utawala wake. mie naweka alama ya pata.
  Nasubiri Mahakimu wa kesi. Sijui kama watatekeleza haki. Tusubiri.

   
 • Tarehe: 5:43:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mark msaki

  Jeff kuna kitu kimoja hapa nilitaka kuona na pengine ndio hivyo! - cha kwanza ninadhani kabisa kuwa kwa kuwa alijua kutakuwa na mandamano ya CUF kumtaka ampige chine kamanda Mahita, na Cuf walisema wataandamana iwapo tu atakuwa hajampiga chini hadi jana, aliwapa fursa CUF kuandamana ili iwe kielelezo cha utawala wake ambao unapenda kuwa rafiki na malezi bora ya demokrasia kwa maendeleo ya nchi!!! - aliishapata ripoti ila alisubiri CUF waandamane kwanza halafu atekeleze!

  unless otherwise kudeal na makoplo 15 ambao wamefundishwa na bosi wao na utawala uliopita kusema uwongo bado sio hatua ya kutosha! - si umeona walikuwa wanadai CUF wana vurugu- Je umeona kuwa ni viongozi wao ndio waliomba wafuasi wawe na amani katika maandamano? waliomba pia CCM wapenda demokrasia wahudhurie na kizuri zaidi waje na T shirt zao!! - aliyekuwa na vurugu ni huyu Mahita sio CUF! sasa hivi tukiendelea hivi hata mie nitaitoa kibindoni kadi yangu ya Chama changu na kuutangazia umma fahari ya chama changu na nchi yangu!!

  nashukuru kuwa umekubali kuwa Raisi ni msomaji mzuri wa blogu! mungu mbariki JK!

   
 • Tarehe: 5:48:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mark msaki

  Jeff kuna kitu kimoja hapa nilitaka kuona na pengine ndio hivyo! - cha kwanza ninadhani kabisa kuwa kwa kuwa alijua kutakuwa na mandamano ya CUF kumtaka ampige chine kamanda Mahita, na Cuf walisema wataandamana iwapo tu atakuwa hajampiga chini hadi jana, aliwapa fursa CUF kuandamana ili iwe kielelezo cha utawala wake ambao unapenda kuwa rafiki na malezi bora ya demokrasia kwa maendeleo ya nchi!!! - aliishapata ripoti ila alisubiri CUF waandamane kwanza halafu atekeleze!

  unless otherwise kudeal na makoplo 15 ambao wamefundishwa na bosi wao na utawala uliopita kusema uwongo bado sio hatua ya kutosha! - si umeona walikuwa wanadai CUF wana vurugu- Je umeona kuwa ni viongozi wao ndio waliomba wafuasi wawe na amani katika maandamano? waliomba pia CCM wapenda demokrasia wahudhurie na kizuri zaidi waje na T shirt zao!! - aliyekuwa na vurugu ni huyu Mahita sio CUF! sasa hivi tukiendelea hivi hata mie nitaitoa kibindoni kadi yangu ya Chama changu na kuutangazia umma fahari ya chama changu na nchi yangu!!

  kimsingi indgekuwa mimi Mahita, kiasi cha matokeo ya ripoti hiyo kutoka tu ilibidi nitangulie chini, labda ningepata hata benefiti za uzeeni kuliko kuny'ang'anyawa na raisi. lakini nina wasiwasi kama kichwa chake kinafanya kazi sawasawa!!

  nashukuru kuwa umekubali kuwa Raisi ni msomaji mzuri wa blogu! mungu mbariki JK!

   
 • Tarehe: 9:17:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Kuna wakati ulituambia kuwa kwenye jambo zuri lazima tuseme. Nakubali kuwa katika historia ya tume Tanzania jambo hili ni kama historia. Halipaswi kuwa jambo kubwa la kushangaza (ninamaanisha kufukuzwa kazi na kupelekwa mahakamani kwa wahusika kutokana na ripoti) kwani hivyo ndivyo inapaswa kuwa. Lakini kutokana na historia ya watwawala wetu kusoma ripoti za tume chumbani kwao na kuzitupa, matokeo ya ripoti hii yanatia moyo kiasi. Ninapenda kuamini kuwa vita ya Kikwete dhidi ya rushwa, uzembe, uozo, n.k. haitakuwa inakumba samaki wadogo tu. Mkapa alikuwa akitoa mifano ya vita yake dhidi ya rushwa kwa kutaja idadi za kesi za rushwa mahakamani. Kesi hizo zilikuwa za rushwa ya elfu 20, 50, laki moja...kesi za rushwa za mabilioni sijui zilikuwa zikisikilizwa wapi.

   
 • Tarehe: 3:17:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mark msaki

  Leo asubuhi nilikuwa ninamsoma Enerst Mpinganjira huyu bwana mpinganjira kweli....Mpinganjira anakubaliana moja kwa moja kuwa bwana Mahita alionyesha yale majibisu na kuongea kisiasa kuwakumbusha watawala kumlipa hisani habari hiyo iko hapa

  http://allafrica.com/stories/200602200184.html

  ......At the centre of the drama is fear that showing the police boss the door would open a can of worms with Mahita spilling hitherto untold secrets of CCM's election strategies and funding.....

  CCM in Dilemma As Public Wants Police Boss Sacked

  by Ernest Mpinganjira. Nairobi

  The East African Standard (Nairobi)

  February 19, 2006
  Posted to the web February 20, 2006

  Ernest Mpinganjira
  Nairobi

  Tanzania's ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) is in dilemma over whether to sack Inspector-General of Police Omar Mahita, or retain him and incur the wrath of crime-weary populace.

  In the past two weeks, there have been attempts to hold the Government to account through calls to dismiss non-performers in the police. Top on the list is Mahita, who is fighting to cling onto the top perch of demoralised law-enforcement agency that is said to be teaming with criminals to spread mayhem.

  At the centre of the drama is fear that showing the police boss the door would open a can of worms with Mahita spilling hitherto untold secrets of CCM's election strategies and funding.

  In the past two weeks since Mahita threatened to banish the opposition from national politics, CCM has been at pains to distance itself from the IGP's comments, which the opposition and the ruling party agreed insinuated poll fraud in the form of the machinations the ruling party employs to scuttle opposition.

  Embarrassed by the insinuation of the police force's complicity in election results fixing, senior CCM officials have attempted to force the police boss - at least in public - not to curry favour with President Jakaya Kikwete by issuing threats to opposition parties.

  With Mahita's back to the wall over his wealth, there is now fear within the CCM government that he could retaliate and expose the ruling party.

  Wary of being purged as new regime attempts to forge new alliances, Mahita threw all caution to the wind and told a recent meeting of top policemen in Dar es Salaam that opposition parties were behind runaway crime in the country.

  As proof of his allegations, he produced two knives he said were part of a consignment opposition party supporters use to perpetuate criminal activities.

  "I will make sure that CUF does not rule this country for a long as I'm still the police boss," Mahita vowed. The flipside of the utterance, analysts said, were meant to remind CCM of the favours he had done the party when it faced serious opposition in Zanzibar and major towns on the Mainland.

  Mahita's utterances triggered a public spat with senior members of the government over the police force's role in election fraud and cover-ups of high-profile economic crimes. In parliament as in public the ruling party immediately came under pressure to distance itself from Mahita's sentiments by sacking him.

  As public calls for Mahita's sacking intensified and the debate over his complicity in spiralling crime threatened to suck in CCM bigwigs, the Government leaked a report to the Press last week showing that the IGP is due for retirement in May, hence no need for his dismissal.

  CUF, which held a public demonstration yesterday in to compel Kikwete to sack the police boss, scoffed at the leak as one calculated to buy Mahita's silence.

  For nearly two months now, the police have been under pressure to fight crime in major towns, with senior police officers being singled out as members of criminal gangs that have been on the loose since the new government gave the shoot-to-kill orders in January.

  Crime wave ratcheted up after Kikwete and Mwapachu, who have vowed to weed out the bad elements from the force to clamp down on economic crimes, indicted the police for incompetence.

  Kikwete and Mwapachu have accused the police of culpability in bank heists and ordered a confidential dossier on senior police officers.

  The highlight of the dossier is Mahita's properties that are strewn across Tanzania's 21 provinces, is estimated to run into billions of shillings.

  Relevant Links

  East Africa
  Tanzania
  Legal and Judicial Affairs  Even more intriguing was that, as Mahita's verbal outburst took centre-stage most of last week, the public learnt that his office at the police headquarters in Dar es Salaam could not account for over Tsh3.64 billion ($3.1 million), according to a controller and auditor general's 2004/05 report presented to parliament on Tuesday.

  The report coincided with Mahita's fight-back against accusations that he has been shielding criminal gangs and economic saboteurs from prosecution.


  MASWALI HAPA NA NI MTIHANI WA KWANZA KWA RAISI KIKWETE NI:-

  1. Kwa mujibu wa hotuba ya raisi jana akifungua semina ya TAKURU alizumgumzia eneo la nne lililogubikwa na rushwa na la kufanyia kazi.....kuwa ni SIASA na akaomba TAKURU walishughulikie severely!! - SUALA HAPA NI JE ALICHOFANYA MAHITA SI SI RUSHWA? -rejea hotuba kwa michuzi!

  2. Je, raisi Kikwete anaungana na bwana Ben kuhusu matumizi mabaya ya polisi kuvunja haki za wananchi wake na hasa wale wa visiwani - kuwauwa, kutia vinyesi kwenye visima, kuwapiga bila kosa, kuwamwagia maji ya pilipili, kuwabaka,kuunga mkono janjaweed, kutumia askari wa mafunzoni kupiga kura, na zaidi KUZUIA SAFARI ZA BOTI KATI YA UNGUJA NA DAR MUDA MFUPI KABLA YA UCHAGUZI? - hizi ndizo tunazozijua naamini kuna nyingi hatujazijua na ndio jeuri ya Omari!!! hatujajua zaidi ya wale zaidi ya milioni ambao hawakupiga kura na karatasi za kupigia kura toka uchina...Museveni naye ametenga hela nyingi sasa hivi kuandikisha shahada za kupiga kura .....

  3. Je raisi Kikwete yuko tayari kuchafua CV yake, charisma na uwezo wake kama mwanasiasa kukiri kuwa

  a. Asilimia 80 % ya wapiga kura kumpa yeye kura ni matokeo ya juhudi ya bosi wa polisi?

  b. kuona kuwa maendeleo, upendo na imani ya wananchi kwake inafunikwa kama giza?

  c.kukubali kuwa ameishaleweshwa na rushwa toka kwa Omari kumuachia a do with pension yake ambayo bado kidogo astaafu? je atakuwa anatufunza nini vijana wake kuhusu demokrasia na utawala bora? je kanuni aliyosema ataipiga vita UMWENZETU SYNDROME itanshinda au ataidhibitisha?

  d. Je atatumia mbinu ya kiutu uzima kumwambia aachie ngazi kutumia mgongo wa vijana waliopigwa risasi Sinza? je inawezekana vijana wale na polisi walikuwa ni scape goats wa system kama pengine wengi wetu tutakuwa??

  e.Je Omari anaweza kuwa scapegoat wa chama kama JK akiamua kumrusha kichura? je atadissappear ghafla ili asipasue mabomu?

  suala zima la Mahita limechukua mtazamo wa kisiasa. huku bungeni kuna Mbunge mmoja wa Buchosa Samuel Chitalilo -CCM ameshindwa kuhimili kukaa kimya na kuropoka kuwa wabunge wa CUF Zanzibar watimuliwe na wasipewe marupurupu kwa ajili ya kumtomtambua raisi Karume! habari hii iko hapa

  http://www.darhotwire.com/dar/Habari/2006/02/17/15772.html

  nanukuu samahani Jeff kujaza blogu lako tukufu!

  Kimbembe kinawaandama Wabunge wa Chama cha Wananchi -CUF wanaohudhuria vikao vya Bunge Dodoma kutokana na pande lililowasilishwa kuwa wasilipwe mishahara yao.

  Hoja hiyo inayosubiri jibu kutoka serikalini iliwasilishwa na Mbunge wa Buchosa Samuel Chitalilo -CCM kutokana na msimamo wa Wabunge hao kutokuitambua Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Rais wake.

  Mbunge Chitalilo alitonya kuwa kitendo cha Wabunge hao kuapa kuwa waaminifu na kuitumikia serikali ikiwa serikali ya Zanzibar ni sehemu yake kinapingana na matendo yao.

  Cha kusikitisha zaidi ni jinsi serikali ya Muungano inavyoisaliti serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuwalipa Wabunge hao mishahara, alisema Chitalilo.

  Aliitaka serikali kusimamisha mishahara yao ikiwezekana watimuliwe Bungeni hadi watakapoitambua serikali inayoongozwa na Rais Abeid Karume.

  CUF ina jumla ya Wabunge 22 ambao kati yao 19 ni kutoka visiwani Zanzibar na kutokana na msimamo wa Chama hicho, hakiitambui serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


  .........lakini ukiangalia utagundua hii imekuja mara tu baada ya wabunge wa CUF kuibua kimbembe cha Mahita!....mimi hapo mwanzi nilihisi huyu mbunge ni wa kuteuliwa, niliporudia nikaona ni wa jimbo, ambako pia wananchi wake wanateseka kwa ujambazi......nikashindwa kuelewa kuwa kama kweli hilo jimbo lilikosa mbunge mbadala!!!maana pia sijui kama serekali ya mapinduzi Zanzibar haiwalipi wabunge hao!!

  baadaye nikahisi atakuwa kwenye mtandao wa bwana Omari...hii yoye ni katika kukifikiria vizuri chama chetu na kukkiepusha na uchafu......na pia alienda kinyume na nia ya JK kuua mpasuko wa visiwa na muungano kwa busara...

  ....jibu la mwisho nadhani linaungana na maoni ya bwana Mpinganjira kuwa ni kidonda kimeguswa!!!!

  KWA RAISI JK sasa ndio kumekucha! Raisi hapa ana uchaguzi wa kujiunga na maraisi wa kisasa wasioangalia makunyanzi e.g. Thabo Mbeki na Bingu wa Mutharika ambao hawa wote wamewakung'uta mamakamu wao wa uraisi sembuse mkuu wa polisi!!

  Raisi ana mtihani kutuonyesha kuwa je anachosema ndicha anachotenda?

  Maamuzi ya raisi yana uwezo wa kumwongezea umaarufu maradufu kufanya vyama vingine kusimamisha wagombea ubunge na madiwani tuu...au kuwatia shaka wananchi! ni kusuka au kunyoa!

  Bahasha ndio imefunguliwa na mtihani ndio huoooooooo !!! na uanze!

  naomba nisiulizwe imani yangu kichama! teyari raisi aliishanitetea hapo..."kuna hatari watu wanapoulizwa wakishindwa kuwajibika kusema anayewahoji ni mpinzani......kumbe sio ni kada wa CCM!

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker