VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Sunday, February 05, 2006
TUME ZA UCHUNGUZI:MCHEZO WA KUJIFICHA?
Nakumbuka zamani,nyakati zile ninazoweza kuziita za utoto wangu tulikuwa na mchezo wa kujificha.Mnaanza kwa "tiyari,bado" wanaoenda machakani wanaitikia bado,bado,bado na kisha unasikia tiyariiii..halafu kimyaaa.Mwenzenu anaanza kuwatafuteni.Kama nyie ni mabingwa wa kujificha basi anatafuta mpaka anachoka kisha anasema "jitokezeeeeeni".Yaani ameshindwa kuwaona.Nimesahau adhabu ya kushindwa kuwapata,hivi ilikuwa mnarudia tena kujificha au inakuwaje?

Wakati nikitafakari na kuukumbuka mchezo ule ambao wengine walikuwa wakiutumia kuanzisha uchunguzi wao wa jinsia tofauti,nimeufananisha na mchezo wa kisiasa unaoitwa "uundaji wa tume za uchunguzi" kuhusu jambo moja au lingine.Nauita "mchezo" kwa sababu moja kubwa.Hivi zile tume huwa zinafanikisha malengo gani?Wanakusanyika,wanaenda vichakani,wanakaa kimya,tunawatafuta(tunataka majibu)hatuyapati,kisha baada ya kuchoka tunawaambia wajitokeze.Ndio tumeshasahau mantiki nzima ya tume.Kabla hatujakaa vizuri tunaundiwa tume nyingine.(Raundi nyingine ya kujificha)Mwendo mdundo.

Katika utawala wa miaka kumi wa bwana Mkapa tume kibao ziliundwa.Wewe unayesoma habari hii,ulipata kuona ripoti ngapi ya tume hizo??Hukumbuki hata ile ya jaji fulani ilivyopingwa na muunda tume mwenyewe kwa sababu tu iliendana kombo na matarajiwa au "maelekezo" ya mwenye nyumba??Zilifanikisha nini?

Hivi sasa nchini Tanzania suala la ujambazi linatisha.Makubwa yashatokea na tume imeundwa.Tume imeundwa kutafuta majibu ya unyama au "uhalali" wa kiutendaji na kuitikia agizo la waziri.Mashahidi chungu mbovu washajitokeza.Tume ilipewa siku ishirini na moja kumaliza uchunguzi wao.Kimsingi,tume inapoundwa lazima iwe na malengo au walengwa.Waliojificha vichakani.Nchini mwetu hali ni tofauti.Anayechunguzwa huwa hasimamishwi kazi yake.Anaendelea kushikilia bakora yake kiganjani.Utamchunguza vipi mtu ambaye ana madaraka makubwa pengine kukushinda hata wewe mwenyewe?

Hii ni tume ya kwanza ya Kikwete.Je tutaona "uwazi" ambao mwenzake aliyepita alibakia kuweka maneno pasipo na vitendo huku askari wake wa miamvuli wakiogopa kuchupa kutoka hewani?Wakabakia hewani kwa miaka kumi.Sijui tofauti kati ya askari na mwanafunzi wa uaskari ni ipi.Kujitokeza kwa mashahidi zaidi ya themanini ni ishara tosha kwamba wananchi sasa wamechoka na pengine wanaanza kurudisha imani zao kwa mkuu wa nchi na utawala wa sheria.Hapa Canada mashahidi kama hao huwa wanaitwa "whistle blower" sheria zinawalinda vizuri.Pengine na Tanzania imefikia hatua hizo.Nasubiri kuona matokeo.

Pili ni suala la njaa.Watu wanakufa kwa njaa jamani.Tume imeshaundwa?Ile idara ya maafa inafikiri maafa ni MV Bukoba peke yake?Hili naomba nilihifadhi kwa leo,nitaliundia tume huru ikiwezekana,tena mapema iwezekanavyo.

 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 1:15 PM | Permalink |


Maoni: 4


 • Tarehe: 2:38:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Halafu inaweza kuundwa tume kuchunguza tume iliyoundwa kuchunguza jambo nyeti.

  Waziri wa Usalama wa Raia labda kasahau yaliyowakuta kina Rais Mstaafu Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Rashid Kawawa, Waziri Peter Siyovelwa, Ndugu Augustine Mrema, Ndugu Lee George Mdachi, Ndugu Ernest Said, na wengine waliokumbwa na kesi ya mauaji ya kina Twiga Nindwa na Mazengenuka Mwanankoboko yaliyotokea Shinyanga. Angekumbuka hili nadhani asingitoa hiyo amri au rai aliyoitoa.

  Masalaam,
  F MtiMkubwa Tungaraza.

   
 • Tarehe: 6:40:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger John Mwaipopo

  Unajua nini. Mtu haonekani wa maana kwao. Ungalisema maneno haya Tanzania ungalionekana juha. Sasa umenena humu tandoni hata wakiona wataifanya hawaoni ilimradi kwao maisha mwendo mdundo.

  Yule jamaa aliunda tume ile kwenye mabano kwa kuwasifia wanatume kuwa ni wabobezi katika fani yao. Walipotoa matokeo ambayo yaliendana na tafiti na utaalamu wao akasema sio wasomi na ni wajinga. Sasa swali nani mjinga aliyeunda au waliondwa katika tume.

  Msululu wa tume ulimkera kila mwenye fikra thabiti, kwani hakuna lililofanyika baada ya uchunguzi. Mfano tume ya mlungula.

  Sijui huhu jamaa aliyeingia Magogoni hivi punde atakuja na staili gani. Zima moto ya kuunda tume ili watu wakae kimya na kusahau au kuzifanyia kazi chunguzi na tafiti za tume hizo. Sasa tupo kwenye 'tyari bado?' ya ujambazi.

  Tumpe nafasi tuone

   
 • Tarehe: 5:55:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mark msaki

  tayari bdo!! juzi mheshimiwa JK akiongea na waze DSM alisema tume ina kazi ya kujenga mahusiano mazuri kati ya polisi na raia...nadhani aliishaona presha inayowaka baina ya pande mbili...wananchi na polisi.....sasa sijui kama ataitoa hewani hata kama inaonyesha kuwa yai bovu liko nyumbani mwake?? au ataifumbia macho??

  JK ameishasifika kuwa amekuwa mwenye kukiri udhaifu wa serekali yake na kupania kuupiga vita...tunachoomba mungu ni kuwa tume hii basi na iwekwe wazi, kwani itapreside matokeo ya tume zote zijazo...kwa mahusiano mema si tena ya polisi na umma bali ya serekali na wananchi.....

   
 • Tarehe: 11:16:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Boniphace Makene

  Jeff hapa katika suala la Tume hukukosea kabisa. Huu ni mchezo wa kujificha ama kuficha mambo. Kuna tume zinazoundwa wakati ripoti ilishachapishwa. Kazi ya tume hiyo inakuwa kukusanya geresha na kusubiri tarehe waliyopangiwa kutangaza ripoti kwa waanbdishi ambao nao huwa ahawana maswali badala ya kunakili kila kilichoandikwa na tume.
  Tunasubiri katika tume hii lakini tujikumbushe mzee wa Tax Return (Mkapa) amefanya nini na sasa mbona hatumsemi kama alivyoanzisha Ulimwengu?

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker