Ubinadamu na ustaarabu huwa haukamiliki kama suala la kusifia inapobidi linakuwa ni vita nyingine kama zile zilizozagaa katika maziwa makuu ya Afrika.Nimewahi kusema kwamba naichukia sanaa ya siasa kwa sababu huwa inakuwa kama uhuni wa kujifanya huoni na hausikii.Ukimuuliza kiongozi wa upinzani kama kwa mfano Prof.Lipumba,Maalim Seif,Mtikila,Mbowe,Cheyo na wengineo swali la kwamba yapi mazuri alifanya raisi Mkapa wakati wa uongozi wake,itakuchukua takribani masaa kupata jibu.Kwanini?Ni kwa sababu kusifia huwa ni kama mwiko kwa wanasiasa hususani kwenye hizi zama za "upinzani na chama tawala".Mfano huu si kwa Tanzania pekee.Ni dunia nzima,zikiwemo nchi kama hii ninayoishi ya Canada.Hapo ndipo utakapojiuliza,Kulikoni?
Sasa sisi sio wanasiasa.Ninaposema sisi nina maanisha wanablogu,wasomaji wa blogu na wachangiaji wote.Sasa kwa sababu sisi sio wanasiasa naomba leo nitoe sifa kwa IPP MEDIA kwa kujitahidi sana kuwa tovuti muhimu ya habari na ambayo inaonyesha wazi kwamba inafanyiwa kazi.Kila siku hawa jamaa hujitahidi kuwa na habari mpya na angalau picha moja mpya katika ukurasa wao wa mbele.Binafsi nimekuwa sina chanzo kingine kizuri cha habari za nyumbani Tanzania za wakati uliopo zaidi ya kupitia IPP kwanza.Vyombo vingine kama vile Business Times,Daily News,Uhuru na Mzalendo,The Express,Arusha Times nk vimekuwa vinyonga sana kwenye utoaji wa habari.Mara nyingi nimetembelea tovuti zao na kukuta yaliyoandikwa wiki mbili zilizopita bado yamesimama imara.Sifa kwa IPP.Mnajitahidi kwa kweli!
IPP oyeeee!!!! haina mjadala...na kuna na maoni kupitia IPP na DHW zinafaa sana