VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Tuesday, February 07, 2006
TUSIFIE INAPOBIDI,TUSIWE KAMA WANASIASA!
Ubinadamu na ustaarabu huwa haukamiliki kama suala la kusifia inapobidi linakuwa ni vita nyingine kama zile zilizozagaa katika maziwa makuu ya Afrika.Nimewahi kusema kwamba naichukia sanaa ya siasa kwa sababu huwa inakuwa kama uhuni wa kujifanya huoni na hausikii.Ukimuuliza kiongozi wa upinzani kama kwa mfano Prof.Lipumba,Maalim Seif,Mtikila,Mbowe,Cheyo na wengineo swali la kwamba yapi mazuri alifanya raisi Mkapa wakati wa uongozi wake,itakuchukua takribani masaa kupata jibu.Kwanini?Ni kwa sababu kusifia huwa ni kama mwiko kwa wanasiasa hususani kwenye hizi zama za "upinzani na chama tawala".Mfano huu si kwa Tanzania pekee.Ni dunia nzima,zikiwemo nchi kama hii ninayoishi ya Canada.Hapo ndipo utakapojiuliza,Kulikoni?

Sasa sisi sio wanasiasa.Ninaposema sisi nina maanisha wanablogu,wasomaji wa blogu na wachangiaji wote.Sasa kwa sababu sisi sio wanasiasa naomba leo nitoe sifa kwa IPP MEDIA kwa kujitahidi sana kuwa tovuti muhimu ya habari na ambayo inaonyesha wazi kwamba inafanyiwa kazi.Kila siku hawa jamaa hujitahidi kuwa na habari mpya na angalau picha moja mpya katika ukurasa wao wa mbele.Binafsi nimekuwa sina chanzo kingine kizuri cha habari za nyumbani Tanzania za wakati uliopo zaidi ya kupitia IPP kwanza.Vyombo vingine kama vile Business Times,Daily News,Uhuru na Mzalendo,The Express,Arusha Times nk vimekuwa vinyonga sana kwenye utoaji wa habari.Mara nyingi nimetembelea tovuti zao na kukuta yaliyoandikwa wiki mbili zilizopita bado yamesimama imara.Sifa kwa IPP.Mnajitahidi kwa kweli!
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 1:17 PM | Permalink |


Maoni: 5


 • Tarehe: 8:30:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger John Mwaipopo

  Kwa kweli walau kuegama kwao kwa tabaka tawala kuna mipaka.Au kwa lugha nyingine insignificant. Pili walijitahidi sana kadri walivyoweza kuwa 'impartial' (kiswahili chacke kimeniponyoka) wakati wa uchaguzi. Hakika habari zote nilizohitaji kuhusu uchaguzi nilizipata ippmedia.com

  Sidhani kama wanapata pesa sana katika kutupa habari kila kukicha. Kila siku habari mpya!

  Nawapa rambirambi zao.

  (Nahisi nimezua kamjadala kengine kwa kutumia maneno fulani hapi juu. Nasubiri)

   
 • Tarehe: 5:07:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Reginald S. Miruko

  kwa hili la kuleta habari kwenye tovuti kila siku na kufanyiwa kasi, naungana na wewe mia kwa mia. Inasaidia wengi hawa walioko ughaibuni kupata kujua walau huku nyumbani kinasemwa nini juu ya nani na wakati gani. NI NZURI ZAIDI KWA KUWA HAKUNA CHAGUO JINGINE.

   
 • Tarehe: 9:51:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Uliposema, "...tusiwe kama wanasiasa," mimi nimesoma, "tusiwe kama Mrema."

   
 • Tarehe: 5:02:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Kweli kuweka habari mtandaoni ni jambo zuri sana. Kama mtu aliyeko nyumbani anavyoamka asubuhi na kusoma gazeti, walioko ughaibuni nao vivyo hivyo. Wanapata habari zikiwa za moto.

   
 • Tarehe: 5:04:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Kweli kuweka habari mtandaoni ni jambo zuri sana. Kama mtu aliyeko nyumbani anavyoamka asubuhi na kusoma gazeti, walioko ughaibuni nao vivyo hivyo. Wanapata habari zikiwa za moto.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker