VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Wednesday, February 22, 2006
TUYAONGELEE BILA WOGA,TUPATE MAJIBU
Jana niliibua mjadala ambao kimsingi imekuwa ni kero niliyokuwa nayo moyoni kwangu kwa muda mrefu sana.Mjadala wenyewe ni kuhusu vigezo gani vitumike kumtunuku mtu jina na sifa za utanzania?Nani Mtanzania?Shukrani kwa wote ambao bado wanachangia hoja na hoja,nzito nzito na zenye mantiki makubwa kuhusu tatizo hili ambalo wanasiasa wetu au viongozi wetu wanalipa kisogo kila siku kwa kuchelea tu kutengwa na wenzao kama ambavyo Mheshimiwa Iddi Simba ametengwa.Mojawapo ya watu ambao wamechangia mjadala huu kwa nguvu ni F MtiMkubwa Tungaraza.Tungaraza yeye hana blogu/gazeti tando/ngangwa lakini siku zote amekuwa mchangiaji mahiri sana kuhusu hoja na mijadala inayoibuka bloguni. Jana ametoa cheche akiweka msisitizo katika kile nilichokiandika jana.Sasa kwa sababu najua kuna baadhi ya watu huwa hawachokonoi kwenye maoni nimeona ni vyema nikayaweka maoni yake hapa mbele ili sote tufaidi.Tungaraza ameandika haya;

Hodi!Miye sina blog lakini nina tabia ya kuandika na kutuma maoni yangu juu ya mambo anuai kwenye anuani kadhaa za watu ninaowafahamu. Niliwahi kutuma maoni yangu kufuatia kauli aliyotoa Balozi Ramia kwamba "Urafiki wa Tanzania na India ni wa kidugu" wakati alipokuwa anamuaga aliyekuwa kwa balozi wa India nchini Tanzania.Katika maoni hayo niliuliza maswali kama uliyoliza Ndugu Msangi: Kama tuna udugu na Wahindi mbona hatuoleani nao? Hatusali kwenye majamati yao? Mzungu na Mwarabu tunasali nao. Tunaoleana nao. Machotara wa Kizungu na Kiarabu wapo kila mahali Tanzania lakini wa Kihindi hamna na kama wapo wachache sana tena mno kabisa. Mungu wa Waarabu na Wazungu ndiyo wetu japokuwa upapa hatuupati lakini uburuda, utawa, upadre, uaskofu na ukadinali tunaupata. Hali kadhalika ual haji, uimamu na ushehe miskitini tunaupata. Lakini kwenye majamati ya Wahindi ukimuona Mtanzania kaingia jua boi kaenda kufagia au kolokoloni kaenda kulinda. Ikifika saa ya sala wanabakia wenyewe kina Manoj, Prakash, Sandip na Rajesh.Nikaendelea kusema kwamba hakuna mcheza mpira wa miguu hata mmoja wa klabu yoyote inayojulikana kitaifa nchini Tanzania yenye mchezaji muhindi. Lakini vilabu vikubwa viwili Simba na Yanga na vizee kuliko vyote nchini Tanzania vipo au vimepata kuwa chini ya uongozi wa wahindi kama kina Marehemu Mohamed Virani, Marehemu Muheshimiwa Abdulabass Gulamali, Mohamed Dewji, na Azim Dewji. Pia Tukuyu Stars ilikuwa mali ya Muhindi Patel Kaka. Tena kibaya zaidi kuhusu kuongoza timu za kandanda ni kwa minajiri ya kupata jina ambalo baadaye hulitumia kukwea ngazi za kisiasa hususani kupata nafasi za ubunge ambazo huwasaidia sana katika kulobi masuala yao ya kibiashara na kijamii kuliko kisiasa. Ninakubali kwa dhati kwamba kuna wabunge wengine Watanzania weusi ambao katika kipidi chote cha miaka mitano huwa hawajawahi kutoa maoni au kuuliza maswali lakini nina hakika kitakwimu (kama zipo) wabunge wa asili ya Kihindi ni wengi zaidi ambao hawatoi maoni wala kuuliza maswali kwa kipindi chote wanachotumikia bunge. Wanapata kura zao toka kwenye majimbo na wilaya za mikoani walipojaa Watanzania maamuma. Nimewaita Watanzania maamuma kwa sababu siwezi kuwaita wajinga au waliochelewa. Asilani huwezi kusikia Muhindi anagombea ubunge wilaya ya Ilala au Temeke! Akigombea Dar es Salaam atagombea jimbo la Kawe ambalo lina vitongoji kama Boko, Goba, Wazo, na Tegeta ya zamani ambavyo ni mashamba na vyenye wakazi Watanzania Maamuma ambao hawana tofauti na Watanzania wengine wa vijijini. Naomba tuuangalie ukweli huu kwa kuangalia wabunge wa Kihindi wengi wao japokuwa ni wakazi wa Dar es Salaam huwa wanawakilisha majimbo gani.Baada ya kuangalia ukweli huo sasa twende katika shughuli za ajira za kiserikali. Tuna madaktari na wauguzi wangapi wa kihindi kwenye zahanati na hospitali za serikali? Wauguzi na madaktari wangapi wenye asili ya Kihindi wapo kwenye zahanati na hospitali za binafsi? Pia walimu waliopo kwenye shule za vidudu, msingi, sekondari, vyuo vya ualimu, ufundi, kilimo, vyuo vikuu na taasisi zingine za elimu za serikali. Halafu tuangalie na walimu wenye asili ya kiasia walioajiriwa katika taasisi za elimu za binafsi.Sasa tuangalie Wahindi walioajiriwa kwenye makampuni ya serikali na wale walioajiriwa kwenye makampuni ya binafsi na ya wawekezaji. Halafu tuangalie nafasi walizomo wahindi kwenye makampuni ya wawekezaji na zile walizopo wazawa kwenye miradi na makampuni ya wawekezaji. Mwaka 1999 nilipokuwa Tanzania nilifanya utafiti wa haraka haraka kuangalia nafasi za za Watanzania katika miradi na makampuni ya wawekezaji baada ya kutembelea benki moja ya wawekezaji na kukuta kwamba Watanzania walikuwa katika ngazi za chini ndani ya benki hiyo. Nilishangaa na kusikitika sana tena mno kukuta kwamba katika ngazi nyingi za juu za makampuni au miradi ya wawekezaji Wahindi huwa ndiyo wanaofuata kwa ngazi za vyeo baada ya wawekezaji weupe. Lakini nikakuta kwamba katika miradi na makampuni ya wawekezaji wa Kiafrika ya Kusini Muhindi hakuwa na nafasi za juu kama alizokuwa nazo katika miradi ya wawekezaji wa nchi za Ulaya, Marekani, Canada, Australia, au New Zealand!Jinginewe, ulilozingumzia ndugu Msangi suala la lafudhi. Kuna siku niliwahi kumwambia swahiba wangu mmoja wakati tukitazama habari kutoka BBC iliyokuwa ikisomwa na mtanzangazaji wa Kihindi. Nikamwambia unaiskia sauti Muhindi huyu ni kama ya Muingereza. Swahiba wangu akaniamba "..ni kweli, tena anaongea Kiingereza kama Muingereza." Nikamuuliza "..Sasa kwa nini wakiwa Tanzania hata kama ni wa kizazi cha nne bado anakuwa na lafudhi ya kihindi?.." Swahiba wangu akanijibu "..unajua kule Bongo huwa hawajichanganyi lakini huku yuropu wanajichanganya.." Nikamwambia "..sawa.. " kwa sababu sikutaka tuanzew mabishano kwa sababu huyo swahiba wangu ni mabishano.com ukianzisha naye ubishi ujue hautaisha.Sasa kwa kumalizia naomba ukitua uwanja wa ndege Dar es Salaam uangalie kama kuna ofisa Uhamiaji wa Kihindi? Halafu ukienda Posta Mpya upande wa Mizigo uangalie kama kuna Muhindi, halafu nenda bandari upande wa makonteina uangalie kama kuna Muhindi, Bohari Kuukama kuna Muhindi halafu ukiwakuta jiulize kwa nini wapo huko na siyo Kampuni Ya Mabasi ya Taifa KAMATA?

Bila shaka utakubaliana naye kwamba pana tatizo kubwa.Wengi huchelea kuliongelea hili kwa kuogopa eti kuitwa wabaguzi wa rangi! Nikupe siri moja,uzawa ni suala la kimataifa na wala sio la Tanzania pekee.Dunia nzima mzawa anaheshimika kuliko wakuja.Ukija na kukuta wenzio chongo basi unashauriwa na wewe kufunga jicho moja.Tuyaongelee haya masuala,kinaga-ubaga.Kama kuna mhindi anasoma hizi blogu tafadhali usisite kuchangia.Tunataka kujua tatizo nini? Tumeshalea maradhi vya kutosha,tusingoje kuumbuliwa na kifo.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 7:09 PM | Permalink |


Maoni: 3


  • Tarehe: 7:50:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Huyu mtu Mtimkavu ni hazina ya fikra kwelikweli. Kichwa chake kina kumbukumbu kali na pia anaweza kuhusianisha hoja kwa ushawishi wa mazingira hadi ukakubaliana naye kwelikweli. Kuna mengi ameyatamka na mimi niongeze katika suala alilolizungumza Mwandani na Mark kuhusu kumiliki uchumi wa Tanzania. Kama hatutataka kuzungumza wazi ni kweli tunawauza kwa dinari watanzania weusi ambao ni wengi na sasa wako katika mazingira ya kitumwa katika nchi yao. Nakumbuka Jaramogi Odinga aliwahi kusema katika Not Yet Uhuru! Uhuru wetu haushabihiani na hali halisi ya maisha ya watu wetu. Kuna kazi ya kufanya na tumeshindwa kufika tutakapo kwa miaka sasa.

     
  • Tarehe: 10:07:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Indya Nkya

    Unajua wengine wanajua wazi kuhusu mambo haya lakini pipi na halawa zinawachengua. Wengine ni wanafiki. Ukweli unabaki palepale kwamba hata kama ukikaa mahali miaka mia nne bado unakuwa mgeni tuu kama huna asili ya pale. Wamarekani weusi bado wanaitwa wenye asili ya afrika kwa nini? Hata sisis pale bongo tunasema watanzania wenye asili ya kiasia. Kama tunaweka qualification kwenye uraia wa mtu basi kuna kitu. Kwa hiyo ukweli ni kwamba mhindi hawezi kuwa mtanzania. Mwandani katika maoni kwenye makala ya awali alimtaja mhindi aliyejulikana kama mzalendo lakini kazikwa Canada. Ni Amir Jamal huyu, alizunguka wizara karibu zote akiwa waziri. Mwisho wa mchezo kazikwa alikozikwa. Usishangae hata Shamim Khan akarejea siku moja!! Tuukabili ukweli. Mhindi hawezi kuwa mtanzania

     
  • Tarehe: 10:44:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Nilitaka kumkumbusha Michuzi kwa mfano wa aliyekuwa rais wa Peru, Alberto Fujimori alivyofaidika na urai wa nchi mbili.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker