VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Sunday, February 26, 2006
UKIONA MWENZIO ANANYOLEWA...........


Kuna msemo wa kiswahili unaosema;Ukiona mwenzio ananyolewa na wewe tia maji.Maana yake ni kwamba na wewe jiandae kwa zamu yako.Wingu la siasa la nchi jirani na Tanzania ya Kenya,mshirika wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki,limejaa moshi wa rushwa.Ni kashfa ya rushwa ambayo ni tishio la kisiasa,kijamii na vile vile kiuchumi kwa nchi ya Kenya ambayo katika miaka fulani ilikuwa ndio Afrika Kusini ya leo hususani suala la uchumi wa Afrika linapotajwa.

Kama umewahi kuona zile sinema za
Al Pacino za GodFather,unaweza kuwa na wakati mgumu kuitofautisha "dossier" ya bwana John Githongo (pichani kulia) ambaye ndiye alikuwa mpuliza kipyenga mkuu wa serikali ya Mwai Kibaki(pichani kushoto) kabla hajajiuzulu akiwa tayari keshakimbilia nchini Uingereza kuepusha roho yake ambayo inaaminika tayari ilikuwa na dau kubwa.Isome dossier nzima hapa. Nina uhakika kabisa watengeneza sinema wa Hollywood watakuwa washaanza kuandika "script" yake ili kufyatua kashfa hiyo kwenye sinema.

Ukiisoma "dossier" hiyo unaweza kujiuliza je Githongo wa Tanzania ataibuka lini?Kuna tofauti kati ya jinsi serikali ya Kenya inavyofanya" biziness" na jinsi Tanzania inavyofanya hivi leo?Nani anashughulika na deal za silaha kwa jeshi letu?Kuna kampuni ngapi hewa nchini Tanzania ambazo zinanyonya uchumi wa serikali huku kina fulani na fulani wanajua kinachoendelea?Je Githongo angeamua kuwa kunguru na kuchukua "kilicho chake" mambo haya yangeendelea mpaka lini na wapi?Je huu ni mwisho?Tutie maji huku tukiomba Githongo wetu ajitokeze mapema iwezekanavyo.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 6:56 PM | Permalink |


Maoni: 2


 • Tarehe: 5:30:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mark msaki

  Kaka Jeff. nimemsoma huyu bwana. githong'o ni mwanamme. alipata appointment akiwa 37 years old! nadhani hapo utanielewa ninaposema ukombozi uko kwa wale vijana waliokuwa pale cafe wanachezea kompyuta na sio wazee! sina maana kuwa hawapo, walikuwapo ila hawakupata support - unadhani mashirika yetu yalikufaje? unadhani mikataba hii haikuwepo? tofauti ya Kenya na tanzania ni kwamba umafia wa tanzania ni mkali zaidi. ona mpaka leo hakuna gazeti linalomjadili mtu..tofauti na Kenya ambapo jamii iko macho, na vyombo vya habari vinafanya kazi inavyotakiwa, pia kuna vyama vingi. tanzania walikuwapo, Moringe hakuchukua raundi tangu atangaze kuwa anaibua kimbembe akirudi DAr, Mrema alijikuta anafutika kazi kwa kutokubali kufacilitate rushwa ya serekali ya Cleopa Msuya! kwa kutofuata collective responsibility !! nilisikia fununu kuwa Jen. Kombe naye alitolewa muhanga kwa ajili ya skando ya mil. 900...cha ajabu Tanzania ni kuwa utaposimama na kujaribu kusema umma utakuzomea na kukuita mpinzani....kwani unadhani kwanini Omari Mahita hajaguswa mpaka leo? watanzania kweli tumelogwa!!...na asubuhi ni mnazi badala ya chai!!wanachosema kinachoifanya Kenya kuonekana kuna rushwa zaidi ni uhuru zaidi walionao kuliko sisi, lakini inawezekana kabisa kuwa iko kubwa zaidi kwetu!

  la pili ni hili la kung'ang'ania madaraka? je unahitaji hizo hela ili upate madaraka? dunia nayo inakwenda kasi...naona watatulazimisha tuombe wazee wafe haraka haraka (kama tusipotangulia sisi) ili uhuni huu uishe!

  siasa za afrika ni uhuni. kabaki mchovu mmoja anaitwa Mugabe! mtu kazeeka anajifanya bado wamo. hakuna lolote pale! mashamba amenyang'aya wazungu kawapa wajomba zake na watu wa karibu, wamefukua mabomba, wamechinja mg'ombe za maziwa wakala nyama, wakaenda bar na matrekta! naye nasikia anaumwa umwa namuombea aishie haraka - kama sitatangulia mimi!

  Wakenya kama wanajua cha kufanya, wamuite Githongo wampe nchi. nasikia Kibaki hapati tena, labda Nyachae wanamfikiria..tatizo la Afrika huja pale ambapo wanataka waone una mvi za kutosha kabla ya kukupa nchi! ukishafika hapo unafikiria benefiti za uzeeni tu!

  umenifanya niandike makala mida hii maana sikuwa kwenye mudi.

  kila la kheri!

   
 • Tarehe: 2:54:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger John Mwaipopo

  U-Githogo wataka moyo. Lazima mtu ajikane na awe jasiri na juu ya yote aipendayo nchi kwa dhati na si kwa muonekano.Pengine Githogo alipata ujasiri kwa kujua kuko kwa kukimbilia, Uingereza.

  Kwa Tanzania suala hili ni time-Bomb maana watanzania wengi hatujui ama tunaogopa kuanzisha suala fulani, mpaka lianzishwe kwingine alakini laonekana li-njiani.Wakenya hawa hawa walianzisha muunganiko wa vyama NARC. Wapinzani wa Bongo nao wakataka kuigiza kitu kama hicho.

  Kwa lugha nyingine, sisi ni waigilizaji. Ila iwapo atatokeza Githogo wa Tanzania hili litakuwa jambo la kheri. Hofu yangu ni njaa na tamaa tulizonazo za mali na fedha. Wakina Sokoine na Mrema siku hizi ni haba, pengine wapo lakini wanalambishwa asali kwanza."Yana mwisho haya" (Shafi A. Shafi-Kuli)

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker