VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Thursday, February 23, 2006
URAIA WA NCHI MBILI: TUNASEMAJE?

Fukuto la mjadala wa nani mtanzania,sifa gani awe nazo mtanzania,Tanzania ina matabaka mangapi kijamii ungali moto.Katika kuchangia Michuzi alichomekea na kuomba kutolewa "tongotongo" (maneno yake mwenyewe) kuhusu umuhimu wa kuwa na uraia wa zaidi ya nchi moja kwa wakati mmoja.Kwa kizungu dual citizenship.Aliomba pia kujua kama ni kweli kwamba watanzania wengi tuliopo nje ya nchi(ughaibuni) "tumejilipua"?? na hivyo kuweka kibindoni uraia wa nchi hizi za kigeni huku tukiwa hatutaki pia kuachilia "utanzania" wetu??Kwa maneno mengine,je tumeshatimiza hilo tendo la "dual citizenship? Nilimjibu bwana Michuzi kwa kuandika hivi;

"Michuzi,Kuna umuhimu fulani wa kuwa na uraia wa nchi mbili au zaidi kutegemea na mazingira na kama kuna sababu za kimsingi sana katika kufanya hivyo.Raia wengi wa Canada ni raia wa Marekani pia kama ilivyo kwa wamarekani kuwa wacanada pia.Lakini ukiangalia hizi nchi mbili mambo yao mengi haswa ya kiuchumi yanashabihiana.Tatizo linakuja pale wanaopigia debe Tanzania tuwe na uraia wa nchi mbili wanapokuwa wachache ambao wanachotaka ni kupanua mirija yao ya kudhulumu na kuiba mali ya umma,tunawajua.

Mchambuzi wetu mahiri F MtiMkubwa Tungaraza akaweka pia maoni yake na kisha kuomba wana---------(neno muafaka bado) tulijadili suala hili kwa mapana na marefu zaidi.Alianza kwa kuelezea tofauti za kujilipua na uraia wa nchi mbili.Maoni yake kamili haya hapa

Muhidin,Kujilipuwa na kuwa na urai wa nchi mbli ni masuala mawili tofauti kabisa.Kujilipuwa ni mtindo ynaotumiwa na baadhi ya watu wa taifa fulani kuomba ukimbizi kwa kutumia utaifa mwingine. Kwa mfano, maijeria anweza kujilipua kama Msierra Leone ili aweze kupata vibali vya kuishi kwenye nchi ambayo amejilipulia. Natumaini umenielewa.Suala la uraia wa nchi mbili siyo geni hususani kwa mataifa yaliyoendelea au yaliyotawala nchi zingine. Kwa mfano, mzawa au raia wa Australia, New Zealand, Canada, Marekani wanaweza kuwa raia wa nchi hizo pia nchi yao ya asili kama Uingereza na Ireland. Hii pia inatumika hata katika nchi kama Zimbabwe, Afrika ya Kusini,na Namibia. Kutokana na mchezo huu wa ambao nikirejea sayansi ya shule msingi ninaweza kuuita "litmasi pepa" ambapo unaweza kuwa rangi fulani katika mazingira fulani na nyingine katika mazingira mengine inafaidisha sana. Tukichukulia mfano, wakulima(farmers) na walowezi(settlers) wazungu wa Zimbabwe. Wameweza kuhodhi ardhi na mashamba kwa kutumia urai wa nchi mbili. Wamehodhi ardhi na mashamba kwa kutumia uraia wao wa Zimbabwe na wameweza kutetewa wasinyang'anywe mashamba na ardhi hiyo ya Zimbabwe kwa kujisalimisha kwenye urai wao wa Uingereza. Natumaini umenielewa.Kuhusu Watanzania kuomba kuruhusiwa kuwa raia wa nchi mbili ni suala ambalo mimi binafsi nimelisikia likiwakilishwa katika vikao vingi na viongozi wetu wa kisiasa ambao huwa tunapata nafasi ya kukutana nao wanapokuja ziarani huku ughaibuni. (Nafasi za kukutana na kuongea na viongozi wetu ana kwa ana nadhani sisi tulio ughaibuni ni moja ya mambo (priveledges) ambazo wenzetu waliopo nyumbani hawazipati kabisaaa!). Nakumbuka tulipoonana na aliyekuwa Waziri Mdogo wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Abderkadeer Sharrif, suala hili lilijadiliwa na Balozi Sharrif alisema kwamba kwa upande wake haoni sababu zozote za kimsingi za kumzuia Mtanzania kuwa na urai wa nchi mbili. Hali kadhalika tulipokutana na Rais wa Zanzibar Ndugu Amani Karume katika mkutano naye suala hili lilijadliwa tena. Rais karume alipochangia hoja alisema kwamba urai ni suala la mtu kujiamulia kwa hiyo hakuona ubaya wowote wa Mtanzania kuwa rai wa nchi nyingine na akaongeza kusema kwamba suala hili bado linatathiminiwa na vyombo husika. Kadhalika tulipokutana na Rais Mkapa alisema bado hatujawa tayari kuwa na urai wa nchi mbili lakini hakutupa sababu zozote za kimsingi za kutokuwa tayari kuwa na urai wa nchi mbili.Swahiba wangu Dennis Londo aliwahi kunionyesha tovuti ya Watanzania warufani wa suala la uraia wa nchi mbili akaniambia kwamba yeye binafsi haoni ubaya juu ya hilo lakini akanitahadharisha kwamba wengi warufani hao ni wale wenye asili ya Kihindi na wengi wao anuani zao zinatokea Kanada. Jinginewe ni kwamba tukilikurupukia suala la urai wa nchi mbili linaweza kuleta athari mbaya zaidi ya zile zilizoletwa na suala la soko huria. Ukizingatia kwamba wageni ambao wataweza kuhitimu vigezo vya uraia wa nchi mbili watakuwa na mitaji mingi na mikubwa ya kihali nammali kuliko Watanzania na hivyo kuwa na ukoloni wa wenyewe kwa wenyewe kama ilivyo nchini Liberia.

Naomba kufungua rasmi mjadala huu. Tafadhali changia bila woga.Hii ni tovuti huru hivyo na wewe jisikie huru kabisa. Pichani juu ni katika jiji la Toronto (Makene unapakumbuka hapo?) Je, ni hiyo barafu na michezo ya kwenye barafu inayotia watu wazimu kutaka kwa udi na uvumba kuwa na uraia wa nchi nchi kama hii ya Canada (ni kweli kwamba wapiga upatu wa dual citizenship wengi wapo hapa,mimi siwajui mbona?)na wakati huo huo Tanzania au kuna mengine??
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 7:12 PM | Permalink |


Maoni: 7


  • Tarehe: 1:32:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Jeff mimi ni hiyo picha tu inayonikuna maana nimekumbuka na tulipita hapo tukielekea kupata kahawa na mjadala kuanza. Naweza endelea zaidi lakini kujilipua kunatokana na uwezo pia wa wapi wanaojilipua ughaibuni, je ni watoto wa Matonya, ni nani wanaojua umuhimu wa Dual citizenship! Tunaweza kuitumia hoja hii kwa kuangalia nafasi za kiuchumi kwa walala hoi. Ok kama kuna wageni tunaona wana thamani ya kuijenga nchi yetu kuna kosa gani kuwachukua na kuwaingiza kwetu kama wachezaji wa kulipwa wa soka? Kwa imani yangu niko radhi hata kuona Joji Kichaka anakuwa rais wa Tanzania kwa ahadi ya kutimiza kilio cha mlalahoi wa nchi yetu, kwa kujenga sera bora za kuondoa ubaguzi wa kiuchumi, kujenga mhimili wa utu wetu lakini siwezi kushangilia tu kuwa tuna viongozi wazungu weusi, Not Yet Uhuru alisema Jaramogi na mimi nimekuwa nikizungumzia Afrika kuamka na kupigania uhuru wa uchumi maana mikopo na misaada inaturejesha nyuma, Jeff nadhani utakumbuka mawazo ya mtu kama Ernesto je huyu nikimpa uraia wa Tanzania ni dhambi, vipi kuhusu sTEPHEN lEWIS, mtu mgeni anaizungumzia Afrika kuliko waafrika wenyewe, tena anaijua Afrika kuliko sisi! Sasa hapa niseme nini, uraia nani alileta dhana ya uraia, huyu baradhuli alitufanya kuwa makanda wa mipaka ambayo sijawahi kuitazama kwa macho zaidi ya ramani zilizochorwa kwenye karatasi, dunia haina haja ya kuwekewa mipaka, iwe huru hii mipaka ndiyo chanzo cha vita visivyoisha, tena kuna suala la tamaa na ubinafsi, samahani nitarudi baadaye sitaki mipaka kabisa maana naona wenye nchi wanavyotafuna mali zetu kupitia watoto wao walioko ughaibuni, naona ushenzi wao huku walai bora tuweke hiyo Duo sitizenishipu inaweza kusaidia kubomoa mipaka ya wafalme hawa waafrika wazungu!

    Nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko. Wakatabahu,

    Boniphace Makene

     
  • Tarehe: 8:41:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

    Kwa mtazamo wangu uraia wa nchi mbili kwa Watanzania utasaidia kuondoa tatizo la kuomba viza kwa wale waliochukua paspoti za nchi za ughaibuni wakitaka kuingia tena Tanzania. Vile vile uraia wa nchi mbili utasaidia wananchi wanaoishi ughaibuni kujenga, kununua mashamba au kuwekeza kwenye biashara ndani ya nchi yao ya asili bila mizengwe wanayowekewa wakuja.

    Kwenye lipuli za Mark Msaki na Boniface Makene kuna waraka wa Iddi Simba na Tanzania Economic Forum ambao unawaasa wazawa kujiunga na forum hiyo ili kuongeza kasi ya maendeleo Tanzania, kwa kutumia nguvu za watanzania – wa ndani na wa nje ya Tanzania - kwa ajili ya watanzania wote. Basi mtanzania aliyekuwa na uraia wa Marekani hata kama angetaka kujiunga na asasi hiyo kwa dhati na ukweli wote, atakutana na mizengwe kwani hana uraia wa Tanzania.

    Isitoshe watanzania wa ughaibuni wangekuwa na uraia wa nchi mbili wangeongeza pia hali ya kujisikia watanzania japo hawapo nyumbani tofauti na ilivyo sasa ambapo wamebeba tu ganda la nchi nyengine ambayo wanajua fika si nchi yao.

    Kwa upande wa maendeleo, serikali itakuwa haijafanya busara kuwatelekeza wataalamu waliowasomesha kwa fedha nyingi pindi wataalamu hao wanapochukua paspoti za nchi walizohamia. Kuwatelekeza wananchi kwa mtindo wa kuondoa haki zao kama watanzania ni sawa na kukataa kuwepo kwa sababu za msingi zilizowafanya wananchi hao kuondoka nyumbani, sababu ambazo pengine hawakuzianzisha wao au ni vigumu kwao kuziondoa katika wakati huu. Kwa mfano ubora wa ajira na kipato kadhalika mfumo wa haki wa kuendesha jamii. (Tofauti na mtindo wa kujuana kiukoo ukoo)

    Non Resident Indians wanachangia uchumi wa India kwa hali ya juu sana. Pia wanapokelewa kwa taadhima wakirejea kwao, hata ukiingia nao uwanja wa ndege utaona wanapita mstari mwingine na nyie wageni mtabaki kwenye mstari mrefu na kuhojiwa kwa muda mrefu.

    Suala gumu litakuwa ni la upigaji kura. Mfano ningekuwa nimebeba paspoti na uraia wa uingereza, sidhani kama itakuwa vyema nimpigie kura waziri mkuu wa uingereza mwezi wa tano na mwezi wa desemba nimpigie kura rais wa Tanzania. Hata hivyo kimsingi serikali ikikubali dual citizenship wanasheria watasawazisha hofu kama hizo.

    Kuhusu kujilipua... Najua wengine wetu wamejilipua ki-CUF, wengine ki-kongo, ki-rundi nk. Lakini wengi wa watanzania wamechukua uraia wa ughaibuni kupitia njia ya shule, kazi ama ndoa. Sababu zote hizo hizo haziondoi hoja ya msingi ya kuwa na dual citizenship.

     
  • Tarehe: 11:50:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger MICHUZI BLOG

    tembeleeni mbongo.com na soma intavyuu yangu na Sir JK Chande kuna sehemu kazungumzia uraia mara bee

     
  • Tarehe: 11:51:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger MICHUZI BLOG

    tembeleeni mbongo.com na soma intavyuu yangu na Sir JK Chande kuna sehemu kazungumzia uraia mara bee

     
  • Tarehe: 2:23:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Jeff, bado nataka kurudi kwenye mjadala huu. Kwa sasa nasoma mliyoandika. Nakuta hadithi/visa kabambe. Nitaurudia mjadala huu. Nimegundua kuwa blogu zetu zimekuwa ni chanzo muhimu sana cha habari kwangu na ninapokosa kuzisoma ninapitiwa na mengi.

     
  • Tarehe: 10:55:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Sidhani kama suala la uraia bee lina ubaya katika dunia ya leo. Zipo sababu mbalimbali ambazo zinaweza kufanya badhi ya watu wakataka uraia wa nchi zaidi ya moja. Kwa mfano mimi hivi sasa kwasababu za kifamilia nina nchi mbili. Zote, kwa namna moja, ni zangu. NIkisema kuwa nina nchi moja itakuwa ni ubinafsi na kutaka kupingana na ukweli wa mazingira halisi.

    Lakini nitapenda kusisitiza jambo fulani. Ingawa ninajichukulia kuwa nina nchi mbili, kutokana na nchi yangu mama (Tanzania) kutoruhusu (kwa sasa) urais wa nchi mbili, sioni mantiki ya kuuacha uraia wa nchi mama na kuchukua wa nchi nyingine. Kama ninatakiwa kuwa na uraia mmoja, kutokana na misimamo yangu binafsi, basi uraia huo daima utabakia wa nchi yangu ya kwanza, Tanzania. Huu ni msimamo wangu, wengine najua ni rahisi kuukataa na kuchukua wa nchi nyingine ambazo zinzonekana kuwa na nguvu zaidi ya Tanzania kiuchumi.

    Hivyo,wakati baadhi yetu tunaamini kuwa iko siku Tanzania itakubali kuwa katika dunia-kijiji, uraia bee ni moja ya haki za msingi za wakazi wa dunia hiyo, bado tutabaki kuwa raia wa Tanzania (ingawa tunajichukulia, kwa sababu moja au nyingine, kuwa watu wenye nchi zaidi ya moja).

     
  • Tarehe: 9:10:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Jeff,

    Tafadhali naomba utuletee habari za yule Dada wa Kisomali aliyejilipuwa Uholanzi. Akapanda ngazi mpaka kuwa mbunge wa chama cha mrengo wa kulia. Mwezi huu wakambaini na kumbana wakamwachisha ubunge na kutaka kumnyang'anya uraia. Wazee wa American Enterprise Institute wakamuona potential recruit sasa hivi yuko Washington anakula sahani moja na Hawks e.g Bush Jr, Dick Cheyne, Ronald Rumsfeldt Benjamin Kagan, Paul Wolfowitz, wa American Enterprise Institute.

    Miye yule dada simcondone wala kumcondem. Nasubiri toka kwako.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    PS/Bado nasubiri ule ujumbe wako kupitia barua pepe.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker