Sunday, February 12, 2006
USINIUZE KWA DINARI
Hata wewe ulidhani nimeghairi,Wanadamu ndivyo mlivyo, kidogo mnifungulie daawaSijaghairi kama vile mkimbiza baghala anapokutana na kisiki,Tafadhali usije nibagua,nibainike kuwa tofautiNikaja chinjwa kama vile mtusi,Itakuwa rahisi kubainika,wajua pua yangu ni ndefuSiku zote nimekataa balaa hizi,tatizo zenyewe hazijanikataa badoNitabambua lipi ndugu yako?Wenye nchi wanasema mimi baradhuliNabatilisha uongo kuwa ukweli,si wamesema wao jamani?Wakaweka bayana kwenye runinga ya serikali,Eti mimi siachi kupayuka,kijinga cha moto wakadhani kimezimikaLoh! Wamenoa,naogelea kwa kutumia kope sasaNakuwa kama beberu la mbegu,halichinjwi kamweBedola zangu kwapani,sina kingine zaidi ya kichwaMwili mzima ni mabehewa,mwisho wake haujulikaniMioyo yao imejaa beliari, midomo yao myekundu kwa damuEti nafa kwa njaa, dunia imejaa unaaBado wanapeperusha beramu zao, wanakenua kama ngiriYanibidi nianze kukimbia, nisije kuwa kiburudishoNijivike bushuti, nipake na manukatoNisije enda kama buuMafedhuli wakaja nibwaga,mwalimu usinifunze upuuzi!
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 10:27 PM
|
Permalink |
-
Jeff,
Ngoja nikale nije kurudia kusoma ulichoandika. Da! Nikiwa na njaa huwa sifikirii vizuri. Na uliyoandika yanahitaji kufikiri. Jeff, saa nyingine tunataka mambo mepesi mepesi...au hujui sababu gani tunapenda magazeti ya upashkuna na uzabizabina?
Nakutania, kufikiri ni aina ya zoezi fulani la ubongo.
-
Jeff kuna malenga wawili wamesusa baada ya mimi kukaa kimya kujibu. Umenikumbusha sasa kutumia shairi langu la zamani kesho lisome kibarazani kwangu.
-
Ndugu yangu naona hisia kali.
Nahisi uliandika ukiwa mtuliivu.
Nimelipenda shairi.
-
Mstari wa mwisho huo: mwalimu usinifunze upuuzi...
Hiyo ni kauli nzito sana. Hivi nani atamfunza mwalimu?
-
kha hata mie nimechoka sana sasa hivi...nadhani nikapate msosi kwansa halafu nije kusoma upya hii habari...
Jeff, bwana Makene aliuliza pale bloguni kwangu utupe maelezo kuhusu chuo cha polisi Ontario, baada ya kuianika Cv yake pale...maana huku ndiko CV ya bwana Omari Mahita inasema alihitimu...
1. je kipo hiko chuo?
2.je kinafundisha nini siasa au upolisi? na kama upolisi ni huu tunaoujua sie ?
3.je kiko kwenye viwango vya kimataifa?
Jeff,
Ngoja nikale nije kurudia kusoma ulichoandika. Da! Nikiwa na njaa huwa sifikirii vizuri. Na uliyoandika yanahitaji kufikiri. Jeff, saa nyingine tunataka mambo mepesi mepesi...au hujui sababu gani tunapenda magazeti ya upashkuna na uzabizabina?
Nakutania, kufikiri ni aina ya zoezi fulani la ubongo.