VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Monday, March 13, 2006
ETI KWANINI?

Blogu ni kisima changu kipya cha maarifa.Hii ni imani yangu mpya,sijui wewe mwenzangu!Nafikia hitimisho hilo kwa sababu kila kukicha nakuta mambo mapya kwenye blogu za watu,nasoma mapya,nawaza na kupata majibu ambayo pengine nimekuwa nikiyasaka kwa muda mrefu bila mafanikio.

Pamoja na mafanikio yote hayo bado sijapata jibu la kutosheleza kiu yangu ya maarifa kuhusu swali hili hapa;Eti ni kwanini waafrika tunateketea zaidi kwa ukimwi kuliko wenzetu wazungu na mataifa mengine ya kimagharibi? Nina majibu na nadharia chungu mbovu kichwani kwangu lakini kwa kutambua thamani ya maarifa ninayoyapata pindi ninapoweka "mpunga hewani" basi nawaomba wanablogu wenzangu tujaribu kulijadili hili tena.

Kwa ufupi imani yangu ni kwamba kuna kitu hakiko wazi. Kama umasikini huku ughaibuni pia upo,mwingi tu. Kwa kipimo cha umasikini na biashara ya miili(prostitution) dhana hii inakamilika kabisa. Kama biashara ya miili ipo basi umasikini nao upo. Machangu wachache sana wanafanya biashara hiyo kwa sababu za kibaiolojia yaani kama kuwa na nyege zilizozidi kiwango. Wengi wapo lindoni hususani nyakati za jioni kwa sababu ya umasikini.

Viwango vinaweza kutofautiana lakini je kwa kiasi kikubwa namna hii jamani?!! Kama umalaya,ufirauni nk huku ughaibuni ndio usiseme.Ngono ni kama kujikuna tu kwa wengine. Sasa kwanini? Weusi,waafrika hata waliopo huku wanafariki kwa maradhi yatokanayo na ugonjwa huu zaidi ya weupe.Tupo sehemu moja,tunakufa tofauti sana,inakuwaje?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 2:49 PM | Permalink |


Maoni: 7


  • Tarehe: 3:47:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Jeff hapa sijui kama takwimu za ukimwi Afrika ni za kweli. Kuna wajanja wanazitumia hizo kupata fedha za wezi wa ughaibuni. Wanaziita misaada, ufadhili, sijui nini na wanazitumia hizo kugawa ukimwi. Inaudhi sana tabia hii, siamini sana kuhusu vifo vya ukimwi. Naamini kuhusu Malaria lakini si ukimwi. Ukimwi sasa ni biashara kwani hujui ile kashfa TACAIDS kuhusu Reila Sheikh na Lupogo? vIPI FEDHA ZA CHOMBO HICHO KUTAFUNWA HUKU KIKIWA CHINI YA fREDI sUMAYE? Yapo mengi nitarejea baada ya kusoma mawazo ya Mark Msaki

     
  • Tarehe: 6:56:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Indya Nkya

    Jeff Jiunge kwenye mtandao wa watu waitwao AIDS rethinkers. Mimi ni mmojawapo. Utajisomea na kufaidi nadharia mbalimbali na maelezo juu ya ukimwi. pia pia tovuti: www.aidsmyth.net na www.duesberg.com

     
  • Tarehe: 8:04:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger FOSEWERD Initiatives

    ahahaha Makene!! kulikoni? anyway, nadhani kuna kitu hakiko sahihi kama ulivyosema kaka Jeff. kuna nadharia niliwahi kuipata mahali zamani kidogo kuwa HIV ilikuwa ni agenda ya Roosevelt yule Raisi wa zamani marekani, kuwa amalize wanadamu vengine duniani abakie na wale wa kwake..principally weupe, wale wa kisovieti na weuzi waishie! ati vijana wake wakaingia kwenye maabara, wakajituma wakatengeneza huvu virus..wanasema baada ya hapo, wakanza kuchoma sindano wafungwa na kuwachia huru warudi makwao wakaangamize, kwamba wangeenda kuangamiza watu wenye nguvu (adults) hivyo generation hiyo itakuwa wiped, itabaki wa watoto waathirika na wasioathirika, waathirika watakufa, wasioathirika hawatajua hata historia yao..dunia itakuwa moja ta mzungu pekee...wakaendelea kudai kumbe kuna bwana mmoja alikuwa kwenye programu hiyo ana damu ya kimashariki, ikamuuma, akanza kuuzambaza pale marekani, hamadi unavyojua tena ajali, zilivyo nyingi marekani, kupeana damu bila kujua kuwa ngoma iko pale pale kwenye kitovu, nao wakajikuta wanao.....

    wakaendelea kudai kuwa hii kitu waliitengeneza bila kutengenezaa antidot yake, ndio mana wakajikuta nao wanaumia......mwisho wa hadithi!

    inawezekana kwa upande mungine kama historia ya kanisa "katoliki" linalofungamana na magharibi likasisitiza ndomu isitumike.....

    hadithi hii japo nio vigumu kudhibitisha ninaiona ni ya ukweli...kwa nini wenzetu weupe na hasa wamarekani wamekuwa na ari ya kuamua hatima yao wenyewe, kama miungu fulani...mfano, kwa nini uzae kama huwezi kutunza? vivyo hivyo ukifuatilia kanuni za Malthus za population, utaona kuwa desire hiyo ilikuwepo. wakachora population ya afrika kabla na bada ya ukoloni, na kuandika mabadiliko yaliyotokea (ongezeko la watu) kama jawabu la ongezeko la dawa za kisasa na maisha bora.....lakini kuna mpambano wa kushusha polulation....(human intervention)

    wakachora population ya Marekani, ikawa juu sababu ya migration toka ulaya, baadaye ikashuka walipodhibiti migration....(human intervention)

    mwalimu wangu wa Animal Production kipindi fulani alinifundisha kuwa wamarekani weupe waliwageuka wenzao weusi mle mle ndani ya Marekani ili wasizaane sana, wakaanza kuwafanyisha kazi masaa mengi...kumbe kuwa exposed kwenye mwanga masaa mengi kunaongeza sana fertility....wakadurufu kishenzi, kuja kustukia wamechemsha!!!

    kwa sasa hivi ukimwi umeshika chati Afrika, kuna sababu nyingi za kuendeleza ukimwi - msosi usiotosha, uzito wa kazi(nahisi), umasikini, na labda mazingira (ebu fikiria umetembea km 30 kwenda na kurudi kazini na unavuja majasho halafu unakutana na ishu ambayo na wewe ulikuwa unailalia mlango wazi) unadhani ile mikato ya chupi kwenye mapaja itakuachia ukiwa unajinafasi kwenye bustani la maraha?

    Mbeki (mmoja wa model presidents wa Afrika)alikataa kuwa kuna kitu kama ukimwi...japo akapingwa hata na Mandela, lakini alijua anachofanya, alikuwa analilia copyright ya kutengeneza madawa nyumbani kwake kwa kufungia biashara kutoka nje...kwani ukimwi ni biashara pia. kuna juhudi nyingi sana za kupambana na HIV hapa japokuwa kila siku wafa 6,000 by 2010 wa SA 5,000,000 (10 %)watakuwa wamekufa (waliopo na wasiopo nje ya ARV program)! kweli ni pigo kubwa!

    Chuo kikuu muhimbili wamefanya utafiti, wakishirikiana na uingereza, wameona kuwa upatikanaji wa Vitamin A na E na nyengine ambazo husaidia oxidation mwilini kama B huchelewesha ugonjwa kuchanganya na hivyo huvuta muda hadi mtu aanza kustahili kupewa dawa.

    ninaamini kuwa suala la Ukimwi ni agenda nzito, ndio maana hata suala la kupata matibabu (dawa) linachelewa! najua Makene aliponitega (nakubali ni gia ya kunyonya mshiko wa nchi zetu masikini maana wenzetu wako mbele dakika 3)...utashangaa ni hela nyingi zinazoingia kwenye programu za ukimwi lakini ni chache huenda kwenye tafiti...kuna wakati waliwapata wale mafanya biashara wa ngono kule kenya ambao wana ngoma na wanadunda, ilikuwa waangalie kama inawezekana kupata (antibodies) kinga ambazo ni matokeo ya kuwepo (antigen) - ugonjwa kwenye mwili wao...yaani wangetengeneza kama chanjo za magonjwa mengine....wakasema watatafuta copy right halafu research iendelee lakini kimya hadi leo. kuna kijana TZ alipimwa akawa na ngoma, baadae ikaisha, naye alikubali kuwa mashine ya majaribio na utengenezaji wa chanjo, nayo iliishia hewani sijui imefikia wapi!!!

    kutokana na ukweli kwamba ukimwi upo, na unatumaliza, mie hoja yangu ni kwenda kasi zaidi hasa sie tunaoathirika, tuna maprofesa wa kutosha (kama sio wa kugushi vyeti), kodi tunakusanya (kama sio ya kwenda kutalii na kushop france), tuna wagonjwa (wengi tu kila kona).....tuamue tu kama Afrika, tutatue tatizo linalotukabili! tusisubiri maagizo toka WHO! - mbona Marekani walipiga Iraq bila ruhusa ya UN?

    ni hayo tu, sijui nimejibu swali letu bwana Jeff?

    N:B. huku SA waligundua kuwa beet root zina uwezo sana wa kumpa afya mgonjwa wa ukimwi..hata waziri wa afya anashikia kidedea hilo.....sijafuatilia kwa nini ila ninajua kuwa zina karotene ya kutosha ambayo ni Vitamin A. cha ajabu nyumbani sijaona mahala imepandwa au inauzwa! kama unashusha makala basi wasisitizie watu wale beet root kwa bidii inaweza kuwasaidia...

     
  • Tarehe: 11:53:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Ahsanteni kwa kuuanza vyema mjadala.Hebu kabla sijaanza kudondosha mawe mengine tusaidiane mchanganuo huu.Hivi kama kila kitu ndani ya mwili wangu kinafanya kazi sawasawa,yaani figo,ini nk na sina mchubuko wowote mdomoni wala kooni;ikatokea nikachukua glass ya damu ya mtu mwenye ukimwi nitaambukizwa virusi vya ukimwi?Zingatia kwamba mwili wa binadamu ni kama chupa ya chai iliyotobolewa chini.Ukiingiza maji upande wa juu unajua yatakapokwenda.Utaambukizwa ukimwi?

     
  • Tarehe: 7:24:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Frank

    sasa hili swali inabidi tulijibu wana mtandao wote.hivi huu ukimwi ulitumwa kwetu tu au.labda wenzetu wanatumia kondom kwa usahihi.sijui!!.ila tupunguze ngono waafrica kwani sisi ni maskini.

     
  • Tarehe: 9:41:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Christian Bwaya

    Kweli hapa panaitwa thamani ya ubongo. Matumizi ya ubongo.

    Pamoja na kwamba inawezekana takwimu za UKIMWI zinatiwa chumvi kidogo lakini bado ni kweli kuwa Watu wetu wengi wanapukutika kwa ugojwa huu.UKIMWi ni tatizo kikweli kweli.

    Kuhusu hoja yako Jeff, mimi ningependa kuamini kuwa kama utakunywa damu yenye virusi lazima utaukwaa kwa vyovyote. Sababu ni kwamba chembechembe za mwili ndani ya mwili ziko nje nje zaidi ya hizi za nje ya mwili zilizofunikwa na kiwambo kinene.

    Virusi hivyo ni rahisi kupenya kwa kusaidiwa na maji maji yaliyomo kwenye "bomba" hilo unalolizungumzia.

    Ndio maana inasemakana kuwa hata mate tu ya mtu mwenye UKIMWI yanatosha kukuambukiza UKIMWI hata kama hauna majeraha mdomoni.

    Nafikiri hivyo.

     
  • Tarehe: 9:46:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Indya Nkya

    kabla ya kuchangia huu mjadala kwa undani kuna haja ya kusoma na kuchimba sana HIV/AIDS hypothesis. Peter Duesberg kwa mfano ambaye ni guru wa Molecular biology Pale California Berkely amejitolea kuchomwa sindano yenye damu ya mtu mwenye virusi. Yeye anasema kwamba hakuna ushahidi wowote kwamba HIV inasababisha Ukimwi hasa kwa vile hakuna aliyeweza hadi sasa kukitenganisha kirusi hicho. Kwa hivyo UKIMWI Siyo tu husababishwa na HIV kuna sababu nyingi. KUna mjadala mzito kuhusu hili.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker