VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Wednesday, March 22, 2006
KITENDAWILI HIKI MPAKA LINI??
Siku chache zilizopita Ndesanjo aliweka kwenye tovuti yake ule mkasa wa serikali kuvamia ofisi za magazeti ya Standard nchini Kenya. Aliufananisha mkasa wa habari zile na jinsi ambavyo mtunzi wa riwaya za kusisimua Elvis Musiba alivyokuwa akimpa akimpa Willy Gamba wake.Kama hukuwahi kuzisome riwaya za Musiba basi ulipitwa na ningekushauri uzitafute uzisome. Pia zipo riwaya nyingine ambazo niliwahi kuzipenda sana na mpaka leo hii nazitafuta. Hizi ni pamoja na zile za jamaa mmoja kutoka Kenya aliyekuwa anaitwa David Mairu pia.Nakikumbuka sana ile ya 'My Dear Bottle"

Leo hii nimekutana na habari kama ile ile ya Standard ila wakati huu ni jirani zetu wa upande wa kushoto Uganda.
Isome hapa habari yenyewe. Uhuru wa vyombo vya habari bado ni kitendawili ambacho aliyekitoa ameshaiaga dunia.Tungali tunahangaika kupata majibu yake. Hivi ni kwanini viongozi wetu wanashindwa kabisa kutambua umuhimu wa uhuru wa habari na mawasiliano? Kwanini tuendelee kuadhibu wengine kwa kutumia sheria kuu kuu ambazo aliziacha mkoloni miaka 40 iliyopita?

Nakubali kwamba kuna wakati waandishi wa magharibi wanapenda kudakia mambo na kuyatafsiri kama wanavyotaka wao kwa nia ya kutosheleza hadhira yao tu. Hili sote tunalikemea.Pamoja na hayo uhuru wa vyombo vya habari haupo kabisa barani mwetu.Tufanye nini?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 3:38 PM | Permalink |


Maoni: 5


 • Tarehe: 9:11:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger frankj

  haya bwana nashangaa hata mimi suala hili limeshamiri sana hasa hapa afrika mashariki,usitake nikumbuke lile la jeshi la magereza hapa tanzania.tupinge hili ili lisiharibu kazi yetu.
  sasa naomba uweke blog yangu kwenye line ups ni www.fglukwaro.com.

   
 • Tarehe: 9:13:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger frankj

  haya hapo nimekosea ni www.fglukwaro.blogspot.com iweke na uitangaze tafadhali.

   
 • Tarehe: 9:21:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Ahsante Lukwaro,
  Karibu sana kwenye ulimwengu wa huu wa mawazo huru na yenye muelekeo wa wajibu.Nitakutangaza

   
 • Tarehe: 3:15:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  We Frank acha ushamba, kwani ni lazima mtu aweke kiunganishi cha Blogu yako, mbona wewe hujaweka yake?

   
 • Tarehe: 3:12:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

  Kila wakati narudi kusoma tafakari yako bwana Msangi. Najiuliza, nataka kutoa majibu ya haraka halafu nasita.
  Kwa mtazamo wangu haki huwa unatwaliwa na yule anayeitaka haki hiyo. When you receive or gain a certain right - its a result of a necessary compromise on the part of the oppressor. Kama vile tulivyopata uhuru, au haki za kina mama zinavyopatikana nk.
  Lakini mkoloni asingetoa uhuru kama kungekuwa hakuna joto ya jiwe, akina mama wasingepata haki kama kina baba wasingepata joto jiwe. Vyombo vya habari kadhalika haviwezi kutendewa haki kama utawala haupati joto ya jiwe.
  People of extreme conviction will lead the way. Waandishi wanaharakati wasiokubali kushindwa ndio watakaosababisha mabadiliko fulani. Nahisi mapambano yao yatakuwa magumu mpaka pale wale wanaohusika na ufedhuli watakapoanza kutiwa aibu na kutahayari, watakapochukuliwa hatua moja baada ya nyingine.
  Kadhalika wale wanaharakati miongoni mwao watakapodai haki ya kutathmini "official secrets act" kwa mfano. Miruko kagusia juu ya hili suala ambalo lilimfikisha mwandishi lupango kwa kuandika jambo la kawwaida tu ambalo wananchi wangepaswa walijue. Sasa kubadili yote hayo inabidi ngangari wachache.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker