VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Tuesday, March 28, 2006
NANI MENEJA WAKE?
Wakati ndio kwanza tunaanza kufaidi kama sio kufurahia tovuti hii mpya na iliyosheheni vipande vya kutosha vya burudani,habari,maelezo,picha nk jambo moja limenishangaza kama sio kunisikitisha. Lakini kabla sijaendelea sana naomba nimpe pongezi bwana Luca ambaye ndio mmiliki wa tovuti ya kiduka.com kwa jinsi ambavyo ameweza kukusanya picha kutoka sehemu nyingi za duniani ambapo "wabongo" wanaishi na kuishiwa. Hii inaonyesha jinsi gani huyu bwana amedhamiria kuuweka imara mtandao wa wana Afrika Mashariki popote ulipo. Kumuunga mkono ni wajibu wetu.

Kama umepata muda wa kuangalia zile picha kwa makini ni dhahiri utakuwa umeona pia zile za ziara ya mwanamuziki wa kizazi kipya(MR.NICE) huko Ohio,Marekani. Hapa ndipo huzuni yangu ilipoangukia.Jamani hivi kweli kabisa waandaji wa ziara hiyo walishindwa kutafuta mahali muafaka pa huyu jamaa kufanyia maonyesho yake mpaka wampangie meza kwenye jumba ambalo linaonekana kuwa kama gofu kama vile tulivyokuwa tukifanya sisi pale Umbwe?Tofauti ni kwamba hawa hawakuweza hata kufunika zile meza kwa vitambaa ili angalau zionekane kama jukwaa?Nani alidhamini hiyo ziara?Na nani ni meneja wa huyu Mr.Nice ambaye anaweza kumruhusu mwanamuziki wake kuhatarisha maisha kwa kunengua juu ya meza. Tazama picha zenyewe hapa. Hivi ni kweli sisi hatuwezi kufanya kitu kizuri kilichopangwa kwa umakini na sio papara? Heshima yetu,utanzania wetu,unalindwa na vitu kama hivi.Nina mpango wa kumuomba bwana Luca azitoe hizo picha kwani wanaotembelea tovuti yake wanatoka kwingi duniani.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 11:00 AM | Permalink |


Maoni: 7


 • Tarehe: 5:35:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Egidio Ndabagoye

  Nimeziona picha za MrNice ndani ya Kiduka kaka Jeff.
  Aibu!

   
 • Tarehe: 8:11:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Umetazama kwa jicho kali, Jeff. Suala la meneja unajua wasanii wengine wanachukulia kama mzaha. Meneja mara nyingi ndio humjenga au kumbomoa msanii. Au kumwibia.

  Lakini Jeff, safi sana ulivyochomoa kiduka hiki.

   
 • Tarehe: 11:12:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Luca

  Kaka Jeff asante kwa pongezi lako, suala la meneja bado halijafikiriwa bongo. Kazi ya umeneja wa msanii ni kazi kubwa, na inahitaji ujuzi wa vitu vyote vinavyohusika na mambo ya burudani.. kwa sababu mwisho wa siku wewe kama meneja ndio utawajibika. Kuna watu ambao wanafikiri kuwa menja inamaanisha kwamba wew ni bosi na pesa zitakuja ukiwa umekaa ofisini tu...

  Kwa kweli ningekuwa Tanzania ningeanzisha kimanagement agency ya maana...

  Ningependa kuongeza kwamba kiduka kimebadilishwa, sasa hivi linaitwa www.bongo5.com

  Mabadiliko yamesababishwa na maoni kutoka watu wengi kwamba jina la KIDUKA halifai kwa malengo yangu ya kukutanisha jamii ya wabongo duniani katika tovuti moja.

  Naomba msamaa kwa watu wote kwa usumbufu, lakini nadhani hivi lengo yangu itaeleweka zaidi.

  Hivi sasa natafuta information za mabendi za zamani, ili niweke katika tovuti. Kama kuna mtu ambae anaweza kunisaidia bios, picha au kitu chochote ningefurahi sana..

  Asanteni. Luca

   
 • Tarehe: 10:05:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger MK

  Samahani ingawa haya siyo maneno yanayo endana na kichwa cha habari lakini naomba nitoe tangazo langu kuhusu blog.

  TANGAZO:

  Baada ya uchunguzi wa hali ya juu nimegundua jawabu la kuondoa Blogger NavBar (Sehemu ya juu kabisa ya Blog yako inayo onesha search this blog).

  Hii kutokana na ya kwamba watu wengi uwa wanachukizwa na jinsi hiyo NavBar ilipo.

  Jawabu la hili swali unaweza kusoma kwa kubonyeza hapa

  Kama ukipata tatizo au maswali zaidi naomba niandikie na nitakujibu asap.

  Nashukuru,
  ©2006 MK

  Imetengenezwa na kuletwa kwenu na ©2006 MK

   
 • Tarehe: 10:20:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Kaka ni kweli kule ni kuchokana

   
 • Tarehe: 7:56:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger charahani

  Kaka Msangi nimezicheki hizo picha za Mr. Nice kweli ni mchemsho wa hali ya juu, inawezekanaje wataalamu wakakaa na kumwita mtu halafu akaandaliwa maeneo feki namna hiyo nadhani kuna tatizo la msingi.

  Kwanza inawezekana kabisa walifanya mambo ya kibabaishaji kwa maana ya kuepuka gharama, lakini pili Meneja ni mbabaishaji kama walivyosema watangulizi wangu hapo juu.

  Na kwa mtindo kama ulivyosema wadhamini wengine wakiona hii itakuwa kashfa.

   
 • Tarehe: 10:10:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Naam,

  Mabadiliko ya itikadi za kisiasa yamekwenda sambamba na mabadiliko ya mfumo wa kiuchumi na kijamii. Mimi kama msanii wa kipaji hali kadhalika kitaaluma ninasikitishwa sana na mabadiliko katika sanaa ya muziki wa dansi, taarab, ngoma za asili, na tamthiliya/maigizo.

  Nilipata kuzungumza na mwanamuziki mmoja maarufu sana nchini Tanzania kuhusu mabadiliko katika sanaa ya muziki wa dansi Tanzania. Yule mzee akanimbia "..Fidelis, wakati ule tulikuwa na tatizo la vyombo. Sasa hivi vyombo vipo chungu nzima lakini tuna tatizo la wanamuziki! Fani imeingiliwa na watu ambao hawajui kabisa muziki ni nini, lakini wana pesa kwa hiyo wanatengeza studio, wanatengeneza muziki kwa kutumia synthesizer, wanaandika miziki kama wanaandika barua hamna sanaa, wanarekodi, wanauza rekodi, wanatangazwa kwenye tv, magazeti na radio, wanakuwa famous. Wakishakuwa famous wanakuwa wanamuziki..!" Akaniangalia kwa sura ya uchungu sana. Nikamwambia "..Ni kweli yote uliyosema. Lakini mimi na wewe kama wasanii hatuna namna ya kubadilisha hii hali kwa sababu hatuna pesa na serikali haina mikakati ya kudhibiti hali hii kama ambavyo nchi zilizoendelea zinavyofanya.."

  Nikisikiliza na kuangalia video/dvd za kizazi kipya ua muziki wa dansi wa bendi kama African Stars huwa naona kasoro nyingi na makosa mengi sana ya kimuziki, kimaudhui/theme, na kimaonyesho/presentation. Haya yanweza kudhibitiwa ikiwa kama mameneja wa wanamuziki watakuwa na taaluma ya sanaa. Chuo cha Sanaa tulikuwa tunafundishwa somo la Cultural Promotion, sijui somo hili kama bado linafundishwa. Ningependekeza kwamba Chuo cha Sanaa Bagamoyo na Idara ya Sanaa za Maonyesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wangeanzisha somo kamili la Arts Management ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa mameneja wa sanaa.

  Kuanzia Oktoba 2004 na hadi Machi 2006 nilikuwa ninapiga disko la muziki wa Kiafrika mjini Helsinki, Finland. Muziki wa kizazi kipya sikuwahi kupiga miziki ya kizazi kipya. Lakini DJ mwenzangu alikuwa akiipiga. Jana J'tatu 03.04.2006 kuna mtu alinifuta akaniambia "Ray C na mwanamuziki mwingine wa Bongo Fleva watakuwa Sweden, vipi ukiwaleta kwenye disko lako?.." Nikamjibu "..Sasa hivi sipigi tena disko, lakini hata ningekuwa bado napiga nisingewaleta, kwa sababu hawana mashabiki kimataifa. Halafu jumuiya ya Watanzania na Wakenya hapa bado ni ndogo kwa hiyo ingepata loss.." Akanimbia "..Unajua nilikuwa sijawahi kufikiria hilo. Hawa wanamuziki wa Kizazi kipya wakija majuu mashabiki wao ni sisi wenyewe. Hawana mashabiki kweli wa kimataifa isipokuwa Watanzania, Wakenya, na Waganda ambao tunaujua huu muziki.." Nikamwambia "..Halafu Watanzania, Wakenya na Waganda hao ni lazima wawe na miaka chini ya 35 halafu wawe wanaeelewa hip hop.. Washamba washamba watakuja kufuata kampani na siyo kuinjoi onyesho au muziki..Kimaonyesho jamaa hawana maonyesho na kimuziki hakuna kipya zaidi ya kusikia muziki wa Kimarekani kwa lugha ya Kiswahili, au vinanda ambavyo mapigo yake huwa yanachoshwa upesi sana kusikiliza.." Akanijibu "..Duuh noma!.."

  Ninawajibika kushiriki kikamilifu katika kuleta mageuzi ya katika fani ya muziki Tanzania,

  F MtiMkubwa Tungaraza.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker