VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Wednesday, March 08, 2006
UJAMBAZI NI NINI,NANI NI JAMBAZI??

Kamanda Tibaigana(pichani) hivi majuzi kule nchini Tanzania,kwenye lile jiji letu maarufu la Dar-es-salaam ametangaza majina ya watu wanaodaiwa kuwa ndio wanaoongoza mtandao wa ujambazi nchini au kama sikuelewa vizuri pengine alikuwa anamaanisha jijini Dar-es-salaam,Arusha na Kilimanjaro. Nisiposema hongera kwa kazi nitakuwa mnafiki hivyo nasema well done Tibaigana na vijana wako wote . Sitaki kuuliza kwamba walikuwa wapi siku zote na ushahidi dhidi ya watu hao ni wa kiasi gani hivi sasa.Hayo yatafuata baadaye. Listi ya majina ya wana mtandao wa ujambazi haya hapa.
Wakati nikisoma majina ya watuhumiwa jambo moja lilinijia kichwani ghafla kama vile inavyodondoka ile nyota ya jaha. Mbona wote wanatokea maeneo ya watu wenye kipato cha chini? Mbona wengine ni vijana wadogo sana mpaka kufikia hata umri wa miaka 19!!?Je inawezekana Tibaigana na vijana wake wamechanganya kati ya wizi,udokozi na ujambazi?

Hebu jaribu kupiga picha hii kichwani mwako na tafadhali uwe mkweli."Unamuona huyo jamaa aliyeketi hapo??" Eeenh(unaitikia) "Jamaa ni jambazi la kutupwa"! Picha ya huyo jamaa inakujia vipi?Unaona mtu wa aina gani kichwani mwako? Fikiria kwamba mmekaaa kwenye baa moja tuseme pale mitaa ya Sinza(maana Sinza bwana kila baada ya nyumba kuna baa). Je ujambazi hauendani tena na hadhi fulani? Kuna tofauti gani kati ya mla rushwa na mfujaji mwingine wa mali ya umma na "jambazi"? Wale waliowahi kutajwa katika ripoti ya Warioba wakati ndio umewadia?

Ukishapata picha yako tuketi chini tujiulize.Hivi mtandao wa majambazi haupo mitaa mingine kama Upanga,Mikocheni,Oysteybay,Mbezi Beach,katikati ya jiji kwa wadosi nk? Mtandao wa ujambazi unaanzia wapi na kuishia wapi? Kisha ndipo suala la ushahidi litakapokuja kuingia. Vigezo gani vimetumika kuhalalisha kwamba fulani na fulani ni majambazi na wala sio wezi wa simu za mikononi pale Salamander?

Baada ya tafakuri kama hizo tunarudi kwenye nafasi ya jamii yetu katika kulea vijana wetu.Kijana wa umri wa miaka 19 anapoitwa jambazi inamaanisha nini kwetu sisi kama jamii?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 2:32 PM | Permalink |


Maoni: 7


 • Tarehe: 9:45:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger John Mwaipopo

  Urewedi jeff,

  Hao waliowataja ukiona hivyo hawakugawa-ga 'mauzo'.

  Kilichonitisha ni kuwa kumbe majambazi makuu wamejificha katika 'wafanyabiashara'. Tuna kazi kubwa sana ya kufanya Bongo irejee katika amani ya awali.

  Hili mimi nilikuwa nalifahamu zamani. Kwa mfano kule mbeya hawa 'bisnesmeni' wako kibao na tunawatambua. Ujahili wao ni kuteka magari ya safari ndefu halafu asubuhi unamkuta anafungua duka lake kama kawa.'Hatuwasemi tunaogopa mkong'oto'

  Prez Jakaya amesema hiyo list ni fupi mno. Kumbe anawafehemu. Na tusubiti tuone list hiyo anayoijua Prez Jakaya. Pia haitoshi list tu. We want to see justice not only done but also, and most importantly, seen to be done.

  Yasije yakawa tunastaajabu ya filauni, je tukiona ya Musa.

   
 • Tarehe: 1:38:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Boniphace Makene

  Jeff kweli umefungua fikra zangu. Sikupata kusoma kwa umakini majina hayo kwani mimi target yangu ilikuwa kutaka kuthibitisha kuwa wahusika wa ujambazi kweli ni CUF na hapa Tibaigana anaungana na jambazi mwenzake mAHITA. Anataka kutuonyesha kuwa TEMEKE na huko uswahilini ndiko kitovu cha wizi na huko wanaketi wana CUF. Fikiri kwa kina kuna ajenda ya siri katika majina hayo lakini naamini majambazi wa kwanza kabisa ni maRPC WALIOGAWANYWA

   
 • Tarehe: 1:45:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Boniphace Makene

  Mikoa mbalimbali. Jeff ni haya haya ya rushwa na hongo. Mwizi wa kuku anashikishwa pesa za moto za PCB au hakimu wa mahakama ya mwanzo. Vipi kuhusu mikataba feki inayoghalimu fedha nyingi za umma. Tazama tena suala hili la ujambazi, hao wanashikwa hawana uhusiano moja kwa moja na kumiliki silaha, kutambua kama kuna fedha mabenki na inawezekana wasifanane na kuyajua magari. Vipi hapa polisi wetu, mbona wanaonyesha wasiwasi mapema hivi! Tutapata ushahidi kuwa hao wanahusika lakini nani anawapa silaha kama kweli wanahusika? Je watanzania tunahitaji anayetumwa kuiba au huyu anayetuma kuua ili apate anachiokitaka! IPO KAZI LAKINI SAFARI LAZIMA IENDELEE.

   
 • Tarehe: 8:24:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

  Si utani, hivi karibuni kuna washikaji zangu naona wametinga kwenye magazeti kama majambazi tena waliopiga watu risasi. Nilijiuliza sana inakuwaje? Tumekua sote, tumecheza chandimu sote, inakuwaje mtu anafikia hali ya kutumia silaha kwa ujambazi? Na hao washikaji naowazungumzia walikuwa ni watu wenye nafasi nzuri tu, usingeweza kujua kama wana dhiki yoyote ya mali kuwafanya waingie ujambazi.

  Haidhuru, kuna makala nimeiona inayowataja wanaoshukiwa ujambazi.
  Nukuu:

  "Kutokana na kasi ya kusafishwa kwa jeshi hilo, vigogo mbalimbali hivi sasa wameonekana kubanwa mavazi yao kwa hofu ya kuibuliwa na kuunganishwa katika sakata la mtandao wa ujambazi.

  Licha ya habari ambazo gazeti hili imezipata kuhusu RPC mmoja wa mikoa ya Kaskazini ana akauti yenye zaidi ya sh. milioni 200, akaunti hiyo imezuiwa naye kuzirai."

  Fuata kiuongo hiki:
  http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2006/03/09/61705.html

  Majambazi wako kila mahala, haswa kwenye wale wenye nafasi.

   
 • Tarehe: 9:49:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Mwandani, kiungo ulichotoa huenda kimekatika maana hakifunguki. Wakati mwingine viungo virefu huwa vinakatika baada ya kubonyeza "tuma." Kwenye mwongozo wa blogu pale nimeandika jinsi ya kufupisha viungo virefu kwa kutumia huduma ya jamaa wa: http://www/tinyurl.com

  Hivi Msangi, huyu Massawe ni yule mwenye hoteli kariakoo na pia aliyewahi kuwa "mfadhili" wa timu yako ya Yanga?

   
 • Tarehe: 8:20:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mark msaki

  duh kweli prez Jakaya si mchezo! yaani majina kutoka naye akayashukia kama mwewe kuwa list haitoshi! kweli watumishi wa serekali wanafundwa kuwa watumishi wa umma sasa hivi!!

  hawa vijana wenye miaka 19 ambao wanakuwa majambawazi ni wale watoto waliokosa kuendelea na ekimu ya sekondari miaka mitano iliyopita kisa hakuna "madarasa"! walioweka hii mifumo walijua maana yake!

   
 • Tarehe: 12:35:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Ndesanjo,
  Ndiyo huyu Massawe ni yule mwenye Hotel AM pale Kariakoo na pia Arusha pale karibu na uwanja wa Sheikh Amri Abeid.Nadhani ndio pia aliyewahi kuwa mfadhili wa Yanga,sina uhakika.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker