
Sitaki kuingilia kazi ya Michuzi ila picha hii ni mojawapo ya picha zinazonivutia sana. Pia picha kama hii huwa inakumbusha mengi. Nadhani hii picha ni tamu na chungu kwa tulio ughaibuni. Hivi unakumbuka siku ulipokuwa unaondoka nchini kwako mara ya kwanza kabisa? Ukiona picha kama hii unakumbuka kisanga chochote? Hebu tupige stori jamani! Wale walinzi walikuambia nini?Wale maafisa wa immigration walikupa lile jicho lao "suspect? Tizama hiyo picha halafu click ili uikuze zaidi uione kwa karibu ili uvute kumbukumbu zako.
Jeff shida yangu ni jina hilo, hivi hakuna uwezo wa kujenga viwanja vingine vikapewa hilo jina. Kuna haja gani kila siku kuwa tunabadili majina. Tena kuna haka kanaitwa Mwalimu Nyerere Foundation kanakoongozwa na mgombea urais ambaye aliwahi pia kuwa Katibu Afrika na Barozi wa Tanzania achilia mbali Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa MSI na vingine sijui... hivi wameshindwa kukaa na kuibuka na wazo la ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere ambacho sambamba na masuala mengine kitahusika kutoa taaluma ya Conflict Resolusion na masuala kama African Studies na Kilimo. Ee bwana hivi, ok nirudi hapo Ea port. Kuna washenzi fulani wanapokuona unakatiza mtoni wanadhani umeshaula, wanataka kukuomba virushwa hapo. Nikiingia hapo rushwa ngo hampati hata mfanyeje, sitoi wala sipokei na tena nadhani itabidi kubadili kushukia uwanja wa Arusha kabisa maana Bongo hapo Majambazi kibao.